Najua kuna mitaa unayoitamani mpaka sasa,
Sasa nenda kazungukie huko, lipia pikipiki akuzungushe, uzijue njia, kuna sehem unayoifikiriaga mbali kumbe ni karibu, vuruga vuruga huko.
Afu like a month before, ongea na madalali wa maeneo hayo.. kuwa unatafuta eneo, kuanzia sehem flan mpka flan, kisiwe na mgogoro, kiwe na barabara ya uhakika, nk nk...
bei unawapa chini kdg ya range zako, na unawaeleza kama kitakuvutia Sana utajivuta zaidi.
Jiandae kupigiwa Sana na kuharakishwa kutoa hela, Ila wewe relax, kavione vyote utakavyoitiwa, kama hamna hata kimoja waache waendelee, ukikipenda, anza kuwachekecha, fanya uchunguzi wote kabla, maana Kwanza hela yote huna mpaka mda huo. (Kichaka cha kujificha, "bado nafikiria" , nashauriana na familia,)..
Ila ukianza kutafuta Una hela mfukon, hata hutajua ni sangapi ulishanunua...