Ulipataje kiwanja chako?

Upo sawa sipingani nawe,
 
Najua kuna mitaa unayoitamani mpaka sasa,

Sasa nenda kazungukie huko, lipia pikipiki akuzungushe, uzijue njia, kuna sehem unayoifikiriaga mbali kumbe ni karibu, vuruga vuruga huko.

Afu like a month before, ongea na madalali wa maeneo hayo.. kuwa unatafuta eneo, kuanzia sehem flan mpka flan, kisiwe na mgogoro, kiwe na barabara ya uhakika, nk nk...

bei unawapa chini kdg ya range zako, na unawaeleza kama kitakuvutia Sana utajivuta zaidi.

Jiandae kupigiwa Sana na kuharakishwa kutoa hela, Ila wewe relax, kavione vyote utakavyoitiwa, kama hamna hata kimoja waache waendelee, ukikipenda, anza kuwachekecha, fanya uchunguzi wote kabla, maana Kwanza hela yote huna mpaka mda huo. (Kichaka cha kujificha, "bado nafikiria" , nashauriana na familia,)..

Ila ukianza kutafuta Una hela mfukon, hata hutajua ni sangapi ulishanunua...
 
Ahsante sana kwa mchango wako nitafanyia kazi.
 
Sijui uko wapi, na utaratibu huko ukoje!

Huku kwetu maviwanja yamepimwa na "Halmashauri", unaenda unachagua kwenye ramani unapewa gharama kwa Sq.meter, unaendelea na malipo. Wakati wa kujenga, unapeleka ramani yako kupitishwa ndiyo unajenga.

Ukitaka kujinunulia tu na kujijengea, toka nje ya mji kabisa (yaan kimbilia porini hukoooo), la sivyo mjini unagongwa X
 
Ahsante nitafuatilia pia almashauri.
 
 
 
Hakuna formula, kikubwa usalama wa kilipo kiwanja isijekuwa kigogo madimbwini... Na uhalali wa kiwanja isijekua na migogoro pesa ikapotea. Kwenye ununuzi mwanasheria ahusike na majirani pia muhimu japo si lazima
 
 
 
Habari ?
Kiwanja unaweza kupata namna nyingi siku hizi Kuna Tausi portal unaweza kuingia humo na kujipatia kiwanja,
Lakini pia kiwanja kinahitaji kufahamiana na watu sahihi, yaan upate sehemu nzuri inayofikika na hakuna shida, ningeandika mengi hapa ila ....
 
Salama ahsante kwa ushauri nilishapata.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…