Ulipokeaje na ulikuwa wapi siku ya tarehe 17 Machi, kifo cha Dkt. Magufuli

Na mamilioni ni vice/versa R.I.P in advance
 
Alifariki Baba, alifariki Mama nilihuzunika sana tu bila kutoa chozi.
Ila kwa JPM chozi lilinitoka kwa huzuni kubwa huku mapigo ya moyo yakiwa juu sana.
Hadi leo bado ninahuzuni.
Mama,Baba[emoji4]..Mtu baki[emoji24][emoji134]
 
Mimi shem wenu alijuta kuniamsha kunipa taarifa. nilimpa show ya hatari, nilimpa yote niliyofundishwa na somo that day...i was happy.
 
Mimi niliacha clouds fm on nikalala kwenye kisita hivi mara nikasikia nyimbo za maombolezo nikastuka sana nikajua kuna kitu nikazima radio ni kaja kuwasha saa nane nikaona bado zinaimba nikabadili tbc mara nikasikia magufuli aliwahi kuwa waziri wa ujenzi nikazima radio, sikulala usiku kucha yaani hamna amani moyo kuuma tu , nilikuja kuwasha tv na radio kesho yake saa kumi baada ya kuona watu wameongea sana nilikuwa natetemeka sana tu sitosahau
 
Mimi shem wenu alijuta kuniamsha kunipa taarifa. nilimpa show ya hatari, nilimpa yote niliyofundishwa na somo that day...i was happy.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] una ufala
 
Usiku kucha nilikuwa napigiwa simu na watu mbalimbali, ila kwa kuwa simu yangu huwa inajiweka don't disturb kila inapofika sa nne usiku hivyo sikuweza kusikia simuzao.

Asubuhi naamka nakuta jirani kafungulia sabufa sauti kubwa,,,. Ule wimbo wa tutaonana tena (Goodluck Gozbert)…..
Kama ilivyo kawaida nikachukua simu nikaanza kupekua mtandaoni......
Dahhh ndo nikakuta taarifa[emoji45]
Aisee sikufichi nililia sana[emoji24][emoji24][emoji24]

JPM amehusika kwa namna fulani kunikwamisha kimaisha but alikuwa mzalendo wa kweli kwa nchi yake
He was a Legend for his country but not all of his citizen

Ukweli kama mimi nilishazoea maisha ya ujanjajanja,,,. Sasa JPM alikuja na mifumo yake. Ilinikwamisha sana aisee,,,,,. Atleast now mambo yameshaanza kurudi kama zamani

Rest Easy Legend[emoji45]
 
Watu tunazika watu wetu kwa corona kila siku halafu yeye anasema Tanzania haina corona! Alistahili sana kufa kwa corona hiyo hiyo.
Msipende sifa na kuitajataja corona hiyo unauhakika kweli hao watu walikufa kwa corona???! Furahia sasa magu hayupo ndio muda wako ila ukikuwa kiakili utamkumbuka baada yakuona mazuri yake, r.i.p mwamba kutokea chato
 
Umelala yoooo

Mchana nilikuwa napiga story na mzee flani kitaa tukawa tunasema kwa kauli za samia kweny hotuba ya tanga
Akuna usalama kabsa,.

Usiku nilistuka midaa ya SAA sita hivi nikaingia insta kila page nikakuta RIP

Sikustuka sana maana kwa uvumi ule nilijua tu jiwe kashaendaa ,nikawa nawazoom tuwanafiki kule insta ,waliokuwa wwanawabishia wambea
 
🤣🤣🤣🤣 Fala wewe
 
Nilihisi ka_relief kamoja kazuri sana rohoni kwangu - niwe mkweli tu... kuna watu wameumizwa sana na huyo jamaa hadi leo bado wanalilia mioyoni mwao.
 
Azoe huko aliko na asirudi tena. Alijaa hamu ya kutoa roho za watu. Ya kwake ikatwaliwa pia...
Msipende sifa na kuitajataja corona hiyo unauhakika kweli hao watu walikufa kwa corona???! Furahia sasa magu hayupo ndio muda wako ila ukikuwa kiakili utamkumbuka baada yakuona mazuri yake, r.i.p mwamba kutokea chato
 
Ilinikuta kama kawaida yangu kuamka 11asubuhi kuomba hasa kumuombea yeye baada ya siku chache kuota ndoto mbaya iliyomuhusu. Nimekaa chumba kingine nisiwapigie kelele waliolala naona meseji inaingia kwenye kisimu cha tochi '' Poleni kwa msiba raisi Magufuli amefariki'' ikabidi nitafute wapi ilipokuwa smartphone yangu naingia facebook nakuta kuna nabii Kasunga karepost ujumbe wa utabiri wa kifo cha Magufuli alioutoa hapo kabla, dah nilichukua dakika kadhaa machozi tu kidume yanatoka, wife akaamka mida hiyo kama 12 akakuta nishawasha na tv kabisa alivyoiona habari machozi yakamtoa japo halikuwa hamkubali kabisa, ilikuwa experience ngumu sana kwangu binafsi.
 
Nlikuwa Hostel nasoma Usiku Dah Nkaanza kuamsha masela huku machozi yananitoka [emoji26]
 
Moja kati ya siku mbaya kabisa maishani mwangu ni hii siku. Nililia kabisa. Ikumbukwe mm huwa hakuna tukio linaloweza kunifanya nitoe machozi. Nina moyo mgumu zaidi ya tatanium.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…