Ulipokua Sunday school pambio gani unakumbuka?

Nimetembea kote kote
Nimezunguka kote kote
Nimetafuta kote kote

Hakuna na hatakuwepo
 
Shangilia Yesuu analeaaa
Yesuu analeaaa...
Baba na mama waliniliea mimi sasa ni zamu ya Yesu
Ambaye atalea roho yangu
Yesu analea
Nakumbuka tulipokua tukiimba huo wimbo ssa kile kihere here cha kushangilia yesu analea tukaporomoka na benchi puuuu
Hahahah
 
Sunday school kweli inaangaza x2
Inaangaza nuru ya Bwana Yesu,
Waalimu wetu wanaangaza x2
Wanaangaza nuru ya Bwana Yesu............
 
Yesu ni maji yaliyo hai
Maji ya uzima, yaliyo hai...
Uzima wangu, uzima wako,........maji maji maji....yaliyo hai!
KKKT Kariakoo hiyo 1973...
 
Asanteeeni mnenikumbusha mbali sana , huu uzi unaweza kuwa msaada kwa walimu wa sunday school wanakuwa na pambio nyingi na sio kurudia rudia kila jpili

Ila kwa upande mwingine zinaleta simanzi maana kuna wengine tulisali wote sunday school saivi wapo mbele za haki , tuseme Amen kwao!!!
 
Toa sadaka injili ifahamike,
Kazi ya Bwana Ipate kuendelea,
Usifiche nyingine mfukoni mwa nguo,
Kwani yeye hatakupa nyingine za maisha......



Duuuh way back
 
Kashetani kadogo kadogo
Kashetani kadogo kadogo
Kashetani kadoooo goooooo!

Bwana yesu mkubwa mkubwa
Bwana yesu mkubwa mkubwa
Bwana yesu mkuuuu bwaaaa!
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] umenikumbusha mbali sana Wewe itakuwa tulisali wote
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…