Ulipuaji mabomu wakati wa mazoezi ya kijeshi unaofanywa na polisi kikosi cha kutuliza ghasia FFU manispaa ya Musoma udhibitiwe ni hatari kwa afya za w

Ulipuaji mabomu wakati wa mazoezi ya kijeshi unaofanywa na polisi kikosi cha kutuliza ghasia FFU manispaa ya Musoma udhibitiwe ni hatari kwa afya za w

mackj

Member
Joined
Jul 25, 2023
Posts
84
Reaction score
98
Kambi ya jeshi la polisi kikosi cha kutuliza ghasia FFU kilichoko mtaa wa uwanja wa ndege kata ya kamunyonge manispaa ya Musoma kinaendesha zoezi la ulipuaji mabomu na silaha za kivita ovyo bila utaratibu wakati wa mazoezi yao bila kutoa tahadhari kwa wananchi jambo ambalo limekuwa kero na kuzua taharuki kwa wananchi wa kata hiyo na kata jirani hasa kwakuzingatia kuwa kambi hiyo iko katikati ya makazi ya watu na pia imezungukwa na taasisi mbalimbali za kijamii kama vile mahospitali, shule, na nyumba za ibada

Kambi hiyo inapakana na shule ya msingi kamunyonge pamoja na shule ya awali ya kanisa la PAG na upande wa hospitali kambi hiyo iko jirani na zahanati ya kamunyonge, na hospitali ya OMEGA na hospitali ya AIC

Watoto ni waathirika wakubwa wa kadhia hii wanakuwa na hofu sana katika shule hizo ziko jirani na kambi hiyo kipindi wanapolipua mabomu na kufyatua risasi zao bila kutoa tahadhari kwa uma jambo ambalo ni kinyume na sheria ya mazingira sura ya 191 kifungu cha 106 (5na 6) na kanuni za udhibiti wa kelele za mwaka 2015

kundi lingine lililoko kwenye hatari kutokana kadhia hiyo ni wagonjwa mahospitalini ni hatari sana kwa afya zao hasa wale wenye shinikizo la damu na magonjwa mengine yanayohitaji utulivu

Kwa mujibu wa Sheria ya Mazingira Sura ya 191, Kifungu cha 106 (5 na 6)
kinakataza kupiga kelele kuzidi viwango vilivyoruhusiwa na vilvile ni kosa
kupiga kelele kinyume na viwango vilivyoruhusiwa. Kanuni za udhibiti wa
kelele na mitetemo za mwaka 2015, zimeainisha viwango vya sauti
vinavyoruhusiwa kwenye maeneo ya makazi, biashara, viwanda na hospitali
ili kulinda afya ya jamii.
Viwango hivyo vinatofautiana kwa usiku na mchana (Mchana ni kuanzia saa
12 asubuhi mpaka saa nne usiku) na usiku ( saa nne usiku hadi saa kumi na
mbili asubuhi.

Usiku viwango viko chini zaidi kwa kuwa ni muda ambao jamii
inahitaji kupumzika.

Inasikitisha kuona vyombo vilivyokabidhiwa kusimamia sheria ndivyo vinavunja sheria bila haibu

Tunaomba mkuu wa mkoa Mara kwakuwa yeye ndiye mwenyekiti wa kamati ya usalama ya mkoa aingilie kati jambo hili linalokiuka sheria ya mazingira

Imeandikwa na mimi makiwa jumanne kabasa
 
Si nasikia huo mkoa wote ni askari shida inaanzia wapi!?
Anyway kwa ninavyojua kamunyonge siku za nyuma yalikuwa mapoli ndio maana kambi ikawekwa hapo ni kama TU hapa goms ilivyo makazi ya raia yalifata kambi ya jeshi so wavumilie hizo kero
NB.
Kambi ya kijeshi UTAH au Sandhurst hazijawahi kukaribiwa na makazi ya watu kwa zaidi ya miaka 100 Sasa mipango miji Wana fail sana
 
Mkoa mzima wa mara ni wanajeshi kwa mujibu wa takwimu za nchi na ajira hizo zipo utumishi? Na mishahara inalipwa hadi kwa hawa watoto na pia miaka ipi lilikuwa pori hapo kamunyonge? Then hivi ukiona makazi ya watu yanaongezeka ni kwanini usitafute maeneo nje mji kwaajili ya range na mazoezi mengine ya vifaa vya kijeshi? Tusifuge uoxo kwa kauli za kihuni🤫
 
Kati ya kambi na raia(makazi) nani kamfuata mwenzie?
 
Kama nawaona wanavyolipua hovyo😁.Wenzao mazoezi wanafanyia porini wao wameganda town...sababu zao Kuna fujo zaidi mjini.
 
Mkoa mzima wa mara ni wanajeshi kwa mujibu wa takwimu za nchi na ajira hizo zipo utumishi? Na mishahara inalipwa hadi kwa hawa watoto na pia miaka ipi lilikuwa pori hapo kamunyonge? Then hivi ukiona makazi ya watu yanaongezeka ni kwanini usitafute maeneo nje mji kwaajili ya range na mazoezi mengine ya vifaa vya kijeshi? Tusifuge uoxo kwa kauli za kihuni🤫
Uoxo hapo ndio sijakuelewa lugha inakuwa kubwa
Wanaoshindwa ni mipango miji kambi zote za jeshi hazikupaswa kusogelewa hata kidogo
Poli miaka ya 1998 ndio mda nimekaa hapo
 
Baada ushukuru mungu unalalamika wengine tunatamani hiyo milio kuisikia we unalalamika au ww sio mkulya ni mzaramo
 
Kama ni kweli hii sio sawa, nimewahi kutembelea hiyo kambi, ipo karibu na makazi ya watu, shule, airport na soko pia kambi ina eneo dogo sana.

Mkoa wa mara unamaeneo mengi wanayoweza kufanyia mazoezi kuliko kusababisha usumbufu hapo mtaani.
 
Uoxo hapo ndio sijakuelewa lugha inakuwa kubwa
Wanaoshindwa ni mipango miji kambi zote za jeshi hazikupaswa kusogelewa hata kidogo
Poli miaka ya 1998 ndio mda nimekaa hapo
Haya bwana hakuna shida ila huwa naamini kuwa kuna suala la fidia kwa wale wanaosogelea kambi ili wahame kwakweli ni changamoto mipango miji
 
Kama ni kweli hii sio sawa, nimewahi kutembelea hiyo kambi, ipo karibu na makazi ya watu, shule, airport na soko pia kambi ina eneo dogo sana.

Mkoa wa mara unamaeneo mengi wanayoweza kufanyia mazoezi kuliko kusababisha usumbufu hapo mtaani.
Ni kweli kabisa maana ukiangalia mkoa wa mara 3/4 ya ardhi yake haijatumika kabisa hivi wamekoswa eneo la kuweka uwanja wao wamazoezi?
 
Iringa tumeshazoea.

Kila jumatano mara nyingi ni miungurumo ya mabomu ya machozi.
 
Kama nawaona wanavyolipua hovyo😁.Wenzao mazoezi wanafanyia porini wao wameganda town...sababu zao Kuna fujo zaidi mjini.
MAzoezi ni uwanja halisi.
Wafanye mazoezi porini wakati kazi ni mjiniiii.
Tena ingefaa wangefanyia mitaani kabisa
 
MAzoezi ni uwanja halisi.
Wafanye mazoezi porini wakati kazi ni mjiniiii.
Tena ingefaa wangefanyia mitaani kabisa
Ooh sawa sasa tuanzie mazoezi ya jeshi pale posta katikati ya jiji
 
Back
Top Bottom