Ulishawahi fanya interview ukaona kabisa hutoboi?

Ulishawahi fanya interview ukaona kabisa hutoboi?

trojan92

Member
Joined
May 18, 2024
Posts
91
Reaction score
276
Wakuu niaje....

Ni mimi hapa kijana wenu Trojan, leo nimeona nishare na nyie kuhusu interview hasa oral.

Ofcourse nimefanya oral interview nyingi sana ila kuna zingine niliboronga kabisa. Kuna wakati uoga unakuingia from no where, kuna wakati maswali ni magumu mno nk.

Je ushawahi fanya interview ukajua kabisa hapa huitwi kazini sababu umeboronga? Ilikuwaje? Share nasi.
 
Zamani wakati natafuta kazi nilienda kwenye Ofisi fulani kuomba kazi,

Mimi "Habari zenu? Nimekuja kutafuta kazi hapa"

Ofisi "Hapa hakuna kazi"

Mimi "Kama hapa hakuna kazi,sasa nyinyi mnafanya nini hapa?"
😂😂😂😂😂😂😂😂
Mwingine aliwajibu hivi """ wakuu mnaweza fanya kazi zote peke enu....""" Baada ya kuulizwa "" unazani kwanini kampuni yetu inakuhitaji""""
 
Wakuu niaje....

Ni mimi hapa kijana wenu Trojan, leo nimeona nishare na nyie kuhusu interview hasa oral.

Ofcourse nimefanya oral interview nyingi sana ila kuna zingine niliboronga kabisa. Kuna wakati uoga unakuingia from no where, kuna wakati maswali ni magumu mno nk.

Je ushawahi fanya interview ukajua kabisa hapa huitwi kazini sababu umeboronga? Ilikuwaje? Share nasi.
Mimi nimefanya interview kadhaa ila interview ambayo sitakaa niisahau ni ya Turing.

Turing ni kampuni ambayo huwa inajihusisha na kuwafaanyia vetting software engineers or developers then inawaunganisha na makapuni yanayohitaji watu wenye qualifications mfanano.

Sasa Mimi nilienda ile vetting process yote nilimaliza bila shida na baada ya kuisett profile yangu vizuri kwenye website yao nilikaa almost miezi sita then nikapata email ya interview ya kazi na kampuni fulani mnaijua wengi tu.

Interview niliambiwa nichague mwenyewe siku ya kufanya na kulikua na slot kadhaa za kuchagua kwenye ile kalenda yao so nikachagua siku na nilijipa wiki ili nijiandae kwaajiri ya hiyo interview.

So siku ya interview ilifika na nilichagua iwe usiku saa mbili basi nikaingia zangu room nikawasha laptop yangu nakutana na kanjibai ananisubiri.

Basi tukasalimiana pale then interview ikaanza, oyaa interview haikua oral wala haikua ya maswali ya abcd ila ilikua ni live coding na sio coding as a coding ilikua ni data structure na algorithms 😆😆😆😆

Kusema na ukweli sikuwa nimejipanga upande huo kwa maana job description niliisoma vizuri na walikua wanahitaji mtu wa reactjs lakini pia ambae anaweza kumanipulate data kwakutumia redux so nikasoma huo upande sana na nikaangalia interview zao zilizopita sana.

Ila yule Muhindi akawa amenitoa kwenye mchezo but swali la kwanza ilikua ni rahisi coz ni if else tu so nikalipiga shwaaaaa na yakabaki maswali mawili hapo ndio tukabaki tunaangaliana mimi na Muhindi.

Nakumbuka nimemaliza swali la kwanza dakika zikiwa zimebaki kama 25 hivi so kila muda ananihesabia namimi kila niliisoma swali nione natokea wapi holaaaaa, Google siwezi maana screen yangu yote anaiona nikabaki natype nafuta natype nafuta then narudi tena kwenye swali mwamba ananiangalia tu hana habari 😆😆😆😆.

Aisee mwili wote ulikufa ganzi wakuu kwa maana ni opportunity ambayo nilikua naisubiria kwa hamu na nilikua nimejipanga kweli kweli kupitia requirements zao ila nikawa nimesahau kwamba ukiwa vitani ukimuona adui hutakiwi kuchagua silaha, wewe weka tu hata kitofa cha kichwa na ndio alichonifanyia yule Muhindi sasa hadi muda ukaisha.

Akaniaga pale then akaniambia next time ukipata nafasi kubwa namna hii make sure unajiandaa vizuri na mchezo ukaishia hapo but the lesson was learned ingawa sitawahi isahau ile interview.
 
Tigo hao na yule hr wao mdada sijui anaitwa maria😀 picha linaanza huwa anakuwa rafiki sana anakupa moyo ila anajua kabisa hapa hautoboi 😀 unakaribishwa interview muda unajichagulia wowote kwenye ile ghorofa hapo mawasiliano, picha linaanza wanaofanya usahili ni vijana tupu alafu wote roho mbaya! Wao wenyewe hawaelewi mambo mengi sana alafu wanagoogle maswali wanataka ujibu hivyo hivyo! Sijawahi kuhudhuria interview ndefu vile! Masaa kama 3 utadhani unahojiwa kituo cha polisi.Inafika stage unachoka unatamani kuwaambia kama hakuna kazi basi! Lakini wao wanaendelea tu🙌 mwisho kale kadada kanakuaga 'we will be in touch' kimoyo moyo unatamani umtukane Ms**ge ww unadhani siwafahamu 😀
 
Back
Top Bottom