Ulishawahi fanya interview ukaona kabisa hutoboi?

Ulishawahi fanya interview ukaona kabisa hutoboi?

Mimi nimefanya interview kadhaa ila interview ambayo sitakaa niisahau ni ya Turing.

Turing ni kampuni ambayo huwa inajihusisha na kuwafaanyia vetting software engineers or developers then inawaunganisha na makapuni yanayohitaji watu wenye qualifications mfanano.

Sasa Mimi nilienda ile vetting process yote nilimaliza bila shida na baada ya kuisett profile yangu vizuri kwenye website yao nilikaa almost miezi sita then nikapata email ya interview ya kazi na kampuni fulani mnaijua wengi tu.

Interview niliambiwa nichague mwenyewe siku ya kufanya na kulikua na slot kadhaa za kuchagua kwenye ile kalenda yao so nikachagua siku na nilijipa wiki ili nijiandae kwaajiri ya hiyo interview.

So siku ya interview ilifika na nilichagua iwe usiku saa mbili basi nikaingia zangu room nikawasha laptop yangu nakutana na kanjibai ananisubiri.

Basi tukasalimiana pale then interview ikaanza, oyaa interview haikua oral wala haikua ya maswali ya abcd ila ilikua ni live coding na sio coding as a coding ilikua ni data structure na algorithms 😆😆😆😆

Kusema na ukweli sikuwa nimejipanga upande huo kwa maana job description niliisoma vizuri na walikua wanahitaji mtu wa reactjs lakini pia ambae anaweza kumanipulate data kwakutumia redux so nikasoma huo upande sana na nikaangalia interview zao zilizopita sana.

Ila yule Muhindi akawa amenitoa kwenye mchezo but swali la kwanza ilikua ni rahisi coz ni if else tu so nikalipiga shwaaaaa na yakabaki maswali mawili hapo ndio tukabaki tunaangaliana mimi na Muhindi.

Nakumbuka nimemaliza swali la kwanza dakika zikiwa zimebaki kama 25 hivi so kila muda ananihesabia namimi kila niliisoma swali nione natokea wapi holaaaaa, Google siwezi maana screen yangu yote anaiona nikabaki natype nafuta natype nafuta then narudi tena kwenye swali mwamba ananiangalia tu hana habari 😆😆😆😆.

Aisee mwili wote ulikufa ganzi wakuu kwa maana ni opportunity ambayo nilikua naisubiria kwa hamu na nilikua nimejipanga kweli kweli kupitia requirements zao ila nikawa nimesahau kwamba ukiwa vitani ukimuona adui hutakiwi kuchagua silaha, wewe weka tu hata kitofa cha kichwa na ndio alichonifanyia yule Muhindi sasa hadi muda ukaisha.

Akaniaga pale then akaniambia next time ukipata nafasi kubwa namna hii make sure unajiandaa vizuri na mchezo ukaishia hapo but the lesson was learned ingawa sitawahi isahau ile interview.
🤣🤣🤣🤣🤣🤣 ahsee huu n uuaji kweny Data structure hapo
 
Wakati ndio nimemaliza Chuo tu nilipata usahili pale U.S Embassy kwenye usahili nilikutana na dada anaasili ya kiarabu sijui kihindi ana accent nzuri ya kiamerica aliniswetisha sitasahau nikawa najiuliza Hawa wamarekani kila mtu ni CIA. Alikua anajua vitu vingi Hadi akaanza kunipa ushauri kama Mimi ndio mwenye Nchi
 
Tare 03 hivi nikikua na interview, Position ilikua Senior sales mahali fulani, sasa kufika nikakuta tuko watu wa5. Nika screen watu watatu nikaona wote na wamudu ila huyu wa nne nikagundua yuko na experience 3 times ya kwangu 😁

Nikasema hapa ni pamoto, Uzuri mimi hua siogopagi watu/Scenario zozote nikatune mindset kua hapa bikifika kur ndani ni kuwapiga lecture tu na kusocialize na majamaa hata wasipo nipa kazi basi wawe wananikumbuka tu.

Majibu yalitoka, ile nafasi alipata jamaa, mimi nikatafutiwa nafasi nyingine kulingana na CV yangu 😁
 
Wakuu niaje....

Ni mimi hapa kijana wenu Trojan, leo nimeona nishare na nyie kuhusu interview hasa oral.

Ofcourse nimefanya oral interview nyingi sana ila kuna zingine niliboronga kabisa. Kuna wakati uoga unakuingia from no where, kuna wakati maswali ni magumu mno nk.

Je ushawahi fanya interview ukajua kabisa hapa huitwi kazini sababu umeboronga? Ilikuwaje? Share nasi.
😂😂😂😂sitasahau nilifanya interview duce walah nilivotoka nilisema sitoboi mambo yalikuwa mazito
 
Back
Top Bottom