Equation x
JF-Expert Member
- Sep 3, 2017
- 33,679
- 49,841
Kila mmoja kwa namna moja ama nyingine ametapeliwa kwenye mapenzi:-
Kuanzia January 2021 mpaka leo hii December 2021, umefanyiwa utapeli gani na mpenzi wako?
- Kuna aliyelazimisha kuzaa na mtu akitegemea apate ndoa, mambo yakawa tofauti
- Kuna aliyetuma nauli akitegemea mwenzake afike, mambo yakawa tofauti
- Kuna aliyesomesha akitegemea waje waoane waishi pamoja, mambo yakawa tofauti
- Kuna waliotoana kijijini na kuja mjini wakitegemea waishi vizuri, mambo yakawa tofauti
- Kuna aliyeshindia mihogo huku akimpendezesha mpenzi wake akitegemea waje waishi pamoja, mambo yakawa tofauti
- Kuna waliojinyima kufanya maendeleo yao binafsi kama kujenga, kufungua biashara n.k na badala yake kuwekeza kwa mpenzi wake akitegemea kuna ndoa, mambo yakawa tofauti
- Kuna aliyejituma kutoa shoo za kibabe akitegemea mwenzake atatulia, mambo yakawa tofauti n.k
Kuanzia January 2021 mpaka leo hii December 2021, umefanyiwa utapeli gani na mpenzi wako?