Ulishawahi kuingia msalani/chooni kujisaidia na simu yako mkononi.?

Ulishawahi kuingia msalani/chooni kujisaidia na simu yako mkononi.?

mimi mara nyingi sana.

kuna siku nimemaliza kujisaidia sijui nilikuwa nawenge gani, wakati na flash ile nashusha simu ikaponyoka kufika kwenye sink maji nayo yamefika.yani ile speed iliyotoka nayo ni balaa. na simu ilikuwa mpya haina ata week.

ila bado naingiaga na simu chooni mazoea yanatabu yake.
 
Ukiingia na simu chooni unastarehe zaidi wakati napitia pitia mambo kwenye simu huko mzigo unazidi kishuka bila wewe kuwa na taarifa baadae ndiyo unashituka heeee! Kumbe Nipo chooni unajisafisha unaondoka.
 
Nikazama chooni nikapiga mbizi kutafuta simu yangu
Inanikumbusha nikiwa mdogo simu ndiyo zimetoka jamaa kanunua Philips kaingia nayo toi kaiangusha chooni na choo chenyewe ni chashimo
Ikabidi choo kivunjwe lile tundu liwe kubwa ili simu itolewe lakin haikuonekana

Ndipo sa ikabidi shimo litobolewe kwa nje ya choo na shughuli ya kuchota mavi na kuyamwaga mpaka simu itakapoonekana

Lakini haikuwa bahati na simu haikuonekana badala yake hasara zikawa tatu
Simu,choo na shughuli ya upakuzi wa mavi ambayo kama ingekuwa na malipo ingekaribia kununua simu nyingine
 
Back
Top Bottom