Ulishawahi kukimbiwa na kuachiwa bili mezani? Ilikuaje?

Ulishawahi kukimbiwa na kuachiwa bili mezani? Ilikuaje?

Ukialikwa na huna hela siku hio unakataa date? Halafu mtu mwenyewe huwezi mdhania kuwa anaweza kukukimbia
RRONDO siwezi enda sehemu bila kuwa na akiba.na pia siwezi agiza kitu ambacho binafsi sitoweza kukilipia.

Kipindi cha nyuma kidogo nilifanya kazi katika sekta ya hotel so ninauzoefu na baadhi ya comments nilizoziandika katika huu uzi
 
Kuna siku mwaka jana saa 12 alfajiri nimekutana na dada mzuri karibu na ofisi za jiji Posta, katoka Harbor view hotel. Mwamba itakuwa hakumpa nauli bibie anauliza wapi anapandia Pantoon.

Nikamuelekeza na kumpa option ya bajaj maana alikuwa kapendeza sana, akaomba aonyeshwe uelekeo wa kutembea.
Wewe hukumuelewa tu,unafikiri kweli hapajui feri? Alitokaje kwao kigamboni?
 
Niko makini Sana kwenye hilo,kwanza naangalia Aina ya kinywaji unachokunywa, speed yako ya unywaji,maongezi yako, comfortability yako, naangalia mazungumzo je tunazungumza lugha moja?hapo naweza kujua game linaendaje...nikiona sikuelewi elewi mie huyo naomba zangu Coca-Cola bariiidiiiiii
Sasa ukiwa na mimi si utakunywa Coca-Cola usiku wote!
 
Mwaka umekuwa na mambo mengi sana, tupunguze stress kidogo.....Ulishawahi kupata aibu hii?

Miaka ya nyuma kidogo nikiwa bado mwanafunzi form 4 nadhani kuna jibaba enzi hizo buzi, likanipa mistari na kuniita mahali jioni, nikajisema si kula tu??? Naenda mie...mida imefika nikachukua simu ya sister nikampigia na kumtaarifu nakuja ila nakuja na sister angu akasema hamna shida njooni.

Haooo tukatinga na viatu virefu jamani halafu mfukoni hatuna hata sh 100, tax tumechukua akaenda kulipa, tukaagiza kitimoto kg 2 na vinywaji, pale mezani yupo na wenzie wanne wakati tunawait msosi uje yule dingi akaanza kunishika shika basi nikawa namind namwambia nipo na sista angu usinishike tuongee tu, akafanya hivo kama mara tatu mi nakataa....bwanaweeeehhh eti akamind akaanza kunifokea na hakuishia hapo akatufukuza bila hata nauli😂😂 vinywaji hatujamaliza wala kitimoto haijafika....ana dhambi yule fala 😁

Hapo mida kama ya saa mbili hivi tukaanza kutembea kwa miguu kutokea kona ya Bwiru hadi mitaa ya rufiji nyie! nyie! tumeomba lift kwenye daladala wapiii tumenyimwa tukavua na viatu tukakanyaga peku moja mbili hadi home make miguu ishachoka ...huwa nacheka nikikumbuka huo mtoko.

Nimemkumbuka hili tukio baada ya kisa kilichotokea juzi, nilikua mitaa flani naendelea kuukaribisha mwaka, meza ya pembeni akaja demu mkare akaagiza wine akaanza kuipiga ile kunywa kulamba mwendo wa kumsubiria sponsor aje, baada ya muda jamaa akatimba, jamaa mapepe hata haendani na yule demu kwakweli japo hayanihusu 😁

Dem kuona mlipa bill kaja akaongeza na spidi na akachangamka, mara ikaagizwa chupa ya pili, jamaa anaagiza Heineken zake pale anapiga na watu offer....imefika saa nne akatoka kama anaenda kuongea na simu daaahhh mtoto kaachiwa bill pale ilibidi aache simu

Epuka aibu, beba pesa yako, happy new year familia
DADA YAKO ALISEMAJE MLIPOFIKA NYUMBANI AU KESHO YAKE😊
 
Back
Top Bottom