Ulishawahi kukutana na balaa la FFU? Tupeane mawili matatu

Ulishawahi kukutana na balaa la FFU? Tupeane mawili matatu

Je, hawa jamaa wako juu ya sheria? Maana huwa wanafanya chochote wakati wowote.

Kuna siku nilikutana nao barabarani jioni wanawahi sehemu, wanapita upande ambao sio wao, yaani wanapita ule upande wa magari yaendayo Gongo la Mboto kutoka Tazara. Sasa wao wapo vice versa, nikakataa kuwakwepa, balaa nilipata mimi.

Nilitukanwa matusi na makofi nikala tena jamaa alikuwa amevaa mask usoni. Je, ulishawahi kukutana na mikasa ya FFU?

Share nasi hapa.
FFU hakuna kitu wanaogopa kama mimi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nilikutana nao Posta Mpya miaka ya nyuma nilisahau kabisa kama siku ile tuliambiwa Ile sehemu iwe nyeupe, nafika posta nasikia sauti inatokea Samora "watu wote tawanyika" [emoji3][emoji3][emoji3]wabongo tuna mbio Semenya nyuma, kuchangikiwa nikakimbilia zilipo defender zao natupa jicho nawaona duuh sina jinsi ikabidi niwavuke hivyo hivyo sijui daladala nilipandia wapi nijikuta nipo kwenye daladala [emoji3][emoji3][emoji3]

Sent using Jamii Forums mobile app
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ili uwe FFU unatakiwa uwe yatima kisha kichwa chako kiwe na bangi ya asili kabisa pia uwe na uchizi Kama asilimia hamsini halafu sifa zingine za uaskari zinafuata. Nakumbuka siku moja nipo Town kariakoo nanunua bidhaa nikasikia king'ola chao kinajamba kama Lori kisha kuna mdada anatangaza kuwa watu wote waliokuwa pale watawanyike .Mara wakaruka mijamaa imejifunika usoni maski ikasema kikosi cha virungu shambulia Yaani Nilipigwa rungu ya bega kisha tumbo .Nikaona nyota kisha giza totoro ile nashifuka najikuta nipo mnazimoja hospitali na pingu mkononi imeunganishwa kwenye kitanda na polisi wa kirai amekaa pembeni yangu. Nolipozinduka yule polisi akamwambia nesi nimepona .Yaani nilibebwa mzobe mzobe mpaka msimbazi polisi bahati nzuri akaja mkubwa wao akasema tuachiwe kwa dhamana . Naona mpaka leo bega langu halijaponaga. .NIKIONA KOFIA NYEKUNDU NAPITA MBALI SANA WALE SIYO WATU NI MICHIZI SANA YAANI SIKUWA NAJUA KINACHOENDELEA LAKINI WAKANISHAMBULIA. BAADAE NILIGUNDUA KUMBE HARAKATI ZA WAISLAM NA SHEKHE PONDA.

Sent using Jamii Forums mobile app
Daaaah polee mkuu
Ila nimejikuta nacheka wakati nikiyasoma maelezo yakoo
 
Duh.
 
Morogoro kuna msikiti maarufu kama (Mungu mmoja.Dini moja).miaka ya 90 enzi hizo za shehe sharifu kulikuwa kuna ile mikutano inaitwa mhadhara.sasa hapo mara nyingi ilihusisha propaganda ya kuwa dini ya kikristo si dini na mambo kama hayo ..pia kulikuwa na kubadilisha watu dini ( kusilimu).

Sasa hali hiyo ilipelekea malalamiko kwa wanaoamini kristo .hivyo serikali ikalazimika kuzuia huo mkutano.lakini waislamu wakawa wanakaidi agizo.

Siku moja jioni tukiwa tumekusanyika kwenye mkutano.ikaja difenda moja ya F.F.U ikatangaza kwamba inatupa dakika kumi tu.pale asionekane mtu yeyote.vinginevyo hali itakuwa mbaya.ukiacha yule askari aliyekuwa anatoa amri kwa kutumia kipaza sauti kuna wengine walikuwa wameshika bendera nyekundu.

Tukawapuuza tukawa tunapaza sauti ya kuhamasishana.( takbir..... alah akbar)
Askari walipoona kelele nyingi wakaondoka zao.sisi tukaendelea na mkutano wetu. Kumbe wale askari walienda kupanga ambush la kichapo.

Baada ya dakika kumi tulistukia umati wote umezungukwa na askari wa F.F.U. walipiga mabomu ya machozi .baada ya kuona tumekata network wakaanza kutembeza vipigo vya maana.tulibondwa vibaya sana.hakuna cha mtoto.mzeee.mama .mlemavu yaani wote vipigo tu.

Kuna ambao walikimbilia ndani msikitini.askali waliingia humohumo ndani na buti zao.wakapiga mabomu ya machozi na vipigo vya maana.mimi walining'oa kucha la dole gumba kwa kirungu walipiga vidoleni.halafu nilikuwa kadogo sana 8 years.

Mpaka leo ishu yoyote itakayohusisha hao askari mimi huwa sisogei kabisa.

Siku nyingine tupo kwa babu kijijini .familia kubwa kiasi..mjomba wangu alikuwa likizo yeye ni askari F.F.U.sasa kati ya wajukuu wote na member wa familia .mimi ni mkorofi sana.
Alipofika akapewa mchapo kwanmba fulani jeuri sana na hivi na vile.

Siku moja nikazingua aisee.kwa kuwa kiumri hatukupishana sana nikamvimbia..

Bwana weeh! Hakuna tabu niliyokosa kuipata.nilibondwa vibaya sana .sitosahau.miaka ilikwenda akaja kuacha kazi baada ya kupata masters.yupo sekta nyingine anakula maisha.NAMUHESHIMU kwelikweli [emoji23][emoji23]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nov 10 ,2017
At St. Pauls Liuli High School Nyasa
Tuligoma bwana. Sio kwa kile kisago. Tuliamka kila mtu kavaa ndala au kiatu dongea
 
Nilikutana nao Posta Mpya miaka ya nyuma nilisahau kabisa kama siku ile tuliambiwa Ile sehemu iwe nyeupe, nafika posta nasikia sauti inatokea Samora "watu wote tawanyika" [emoji3][emoji3][emoji3]wabongo tuna mbio Semenya nyuma, kuchangikiwa nikakimbilia zilipo defender zao natupa jicho nawaona duuh sina jinsi ikabidi niwavuke hivyo hivyo sijui daladala nilipandia wapi nijikuta nipo kwenye daladala [emoji3][emoji3][emoji3]

Sent using Jamii Forums mobile app

🤣🤣🤣🤣 umenichekesha snaa na kifungo hiki cha Corona

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Je, hawa jamaa wako juu ya sheria? Maana huwa wanafanya chochote wakati wowote.

Kuna siku nilikutana nao barabarani jioni wanawahi sehemu, wanapita upande ambao sio wao, yaani wanapita ule upande wa magari yaendayo Gongo la Mboto kutoka Tazara. Sasa wao wapo vice versa, nikakataa kuwakwepa, balaa nilipata mimi.

Nilitukanwa matusi na makofi nikala tena jamaa alikuwa amevaa mask usoni. Je, ulishawahi kukutana na mikasa ya FFU?

Share nasi hapa.
Ila jamaa hawa ni waoga sana nakumbuka
Mtwara vurugu ya gesi kati yao wamakonde zilipigwa uso kwa uso

Walivyozidiwa wakakimbia wakaenda kuitwa wanajeshi zikapigwa hatari hadi vifaru vilipelekwa ilikuwa zaidi ya hatari

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom