Khumbu kawa wa kumsaka kwa manati,ngoja turudi kwenye Uzi wetu pendwa.
Nipo zangu arusha,maisha yakazingua balaa,nikawaza kujiua,kwetu ni mwanza.
Ili nisiwape shida ndugu zangu kusafirisha maiti,ikabidi nifunge safari kwenda mwanza afu nilale gest pasipo kufika nyumbani,nitafute pori ninywe sumu nilale,ndo nilikuwa nimepanga hvyo.
Asubuhi nkatoka gest,nikaenda maduka ya dawa za mifugo,nikanunua dawa ya kuonyea mifugo kichupa kidogo mils 50,nikapita duka jingine nikanunua maji nusu lita,nikapita tena kwenye kimgahawa nikanywa chai ya jero,nikatembea kutoka nje ya mji kutafuta pori zuri ambalo sitaonekana nikifanya yangu.Hapo ni wilayani(sitapataja)
Nikapata sehemu iliyotulia,nikachanganya ile dawa(sumu) na maji,ikawa kama maziwa,nilipata shida kuanza kuinywa ila baada ya dakika kadhaa nikajikaza nikainywa yote,nikalala,ilikuwa ijumaa,nimekuja kushituka ilikuwa ni asubuhi kama saa moja nilikuja kugundua baadae kuwa ilikuwa ni jumapili,nahisi njaa sana,hata kutembea siwezi,napepesuka tu kila nikijaribu kutembea,midomo inamagamba,nikajitahid kujivuta vuta toka mule kichakani kwa kutambaa,nikafika sehemu ya wazi nikamuona mama mmoja nikaanza kumuita kwa ishara ya mikono hata hakuja,aliondoka.
Baada ya muda naona watu wengi wanakuja nilipo,waliponifikia wakaanza kunihoji,nimechoka mbaya hata kuongea siwezi,wakanikokota mpaka kwa mwenyekiti,watu wakazidi kuwa wengi,Kumbe yule mama kanishitaki Mimi kama mwinzi wa mihogo,kwahyo anachotaka nichapwe na alipwe,kwanza wakati huo sikumbuki hata hapo nipo wapi,wakaanza kunihoji,nikaficha nikawaeleza kuwa mi nmepotea nimejkuta tu huko porini sijui nilifikaje,mwenyekiti alinitetea sana,mwisho wakaamua wanipeleke polisi na tupite radio ya jamii ili nitangazwe ndugu zangu waje kunichukua.
Zikatafutwa boda boda,safari ikaanza ,tumefika kwenye kituo cha redio wakahitaji hela ya tangazo kwanza,mwenyekiti akakosa,baadae tukatoka nje ili twende polisi,pale nje tulikaa sana,watu wakaanza kuwa wananishangaa pale na mwenyekiti akawa anawaeleza maswahibu yangu,wengine wakawa wananiuliza nyumbani niwapi nikawa nataja ila hakuna anaejua,nikawaekeza mama yangu ni mwalimu anafundsha shule Fulani, wakawatafuta walimu pale,wengine wakaanza kupiga simu,mpaka wakafanikiwa kumpata mama.
Kwenye lile jengo la redio Kuna bank ilikuwa imepanga pia hapo,sasa wakati nipo hapo watu wananiuliza uliza,akatokea binti mmoja mzuri balaa Toto la kisingida kutoka kwenye ile bank alkuwa kaajiriwa pale bank,
Na Yale matatizo yangu,lakini nilivyomuona binti huyo nilijisemea kimya kimya "hili Toto ni zuri hatariii".
Demu akasogea tulipokuwa,akaniangalia kisha akaniuliza kama nimeshakula,nikasema bado,akaagiza chakula cha 1500,nikaanza kula pale kiaina.
Sikumaliza chakula,Mara mama akatokea,akanichukua,Kumbe walkuwa wanafahamiana na mama,maana mama ni mtu wa vikundi kwahiyo wanaaccount kwenye bank hiyo pia huchukua mikopo hapo .
Nikapelekwa hospital, baada ya siku 3 nikaruhusiwa.
Siku moja demu akaja nitembelea nyumbani,akaja na jamaa mmoja n mtangazaji wa redio pale barobaro sana huyo jamaa,
Baadae wakaondoka tukawasindikiza,waliniletea mapocho pocho mengi sana kama vile Mimi ni manzi,
Baadae demu alipata namba yangu akaanza kuwa ananipigia simu kunijulia hali,
Siku moja kaka ake ni mwanajeshi aliwatembelea,demu akamshahuri mama nikaombewe na kaka yake huyo,jamaa n mwanajeshi lakini n mlokole.
Tukaenda na maza mpaka kwao demu,familia ya watu wachache tu,misosi kama kawaida,baadae nikasalishwa sala ya toba.
Ikawa sasa Mara nyingi mama ananiletea habari za kusalimiwa na huyo demu,na siku moja akaniahidi atanitembelea.
Kwel bhana,one day Mtoto huyu hapa katokelezea kinyama,afu nyumbani nipo mwenyew tu.
Akanisifia kuwa mwili umerudi,Kumbe Mimi ni mzuri(handsome).
Ikafika muda anataka tuselfie,Mara tukizaa Mtoto atakuwa mzuri sana,hapa sasa ndo nilipata shoti ilinipga mwili mpaka ubongo,tatizo nimechoka kuandika.
Kifupi nilkula mzigo tena kwa kuuza mechi.
Penzi lilikuwa tamu sana,kifupi binti anasema alkuwa na kazi lakini alkuwa hajayafurahia maisha.
Kumbe alikuwa na certificate baadae akaamua kwenda kusoma diploma penzi likafifia,Mimi siwezagi kulea penzi la mbunye ilioko mbali kwa kutumia simu.