Kuna mteja wangu mmoja ni Pisi ya maana (Shombe shombe) amesomea nje ya nchi Maswala ya Interior Design chuo cha Oklahoma University, mimi nimesomea hapa hapa Bongo Land maswala ya Ukadiliaji gharama za ujenzi. Hapo mwanzo Dingi yake ndio alikuwa mteja wangu sana, ila baadae mtoto alivyomaliza chuo, Mdingi akanitambulisha kwa Mtoto wake nikaanza kupiga nae kazi hivyo alikuwa ananiletea michoro yake ambayo amesha design mimi kazi yangu ikawa ni kukokotoa gharama za ujenzi nakabidhi kazi then navuta mshiko wangu nasepa.
Nilikuwa sina mazoea sana na yule binti maana Uzungu ulikuwa mwingi sana na kujifanya smart nadhani labda kwa kuwa alikuwa amesomea Chuo chenye adhi kubwa sana, maana icho chuo kipo vizuri usipime, ila kiukweli PISI ilikuwa smart sana, Mabaharia tutafute fedha tupeleke watoto wetu shule za maana aisee.
Kama ujuavyo Wabongo na asa mtoto wa kiume lazima ukomae, hivyo ile PISI mwanzoni iliniwia vigumu sana kufanya nae kazi maana alikuwa ananipa challenge za kutosha kwaiyo nami nikabidi nijiongeze nifanye kazi zake kwa uhakika na umakini mpaka mwisho akakubali ufanisi wa kazi yangu japo kiukweli wenzetu wanaupeo mkubwa sana ya maswala ya Ujenzi na ishu za Real Estate.
Mimi nipo Kanda ya Ziwa so wakati mwingine ananitumia kazi kwa Email au kwa Ems au wakati mwingine nakuja Dar napiga kazi week, anaikagua kama kuna marekebisho tunafanya nakabidhi narudi zangu Rock City.
Jamani acheni ile PISI ilikuwa inajua kuvaa na kupangilia nguo na isitoshe nadhani ata akivaa matambala bado angeendelea kuonekana mrembo... Kuanzia mguu, Paja,midomo, Kiuno ndio usisemee, rangi sasa ni hatari maana ni Shombeshombe ila sio mweupe saana yaani kama wale Shombe Shombe wa Tabora, nadhani wale mliofika Muscat Fisi kule Nzega mtakuwa mmenipata, yaani wana kaweusi fulani cha mbaaali we acha tu.
Cha ajabu na uzuri wake wooote na nimepiga nae kazi miezi nane sijawahi msifia hata siku moja kama amependeza au amenukia manukato mazuri,japo kila akikutana na mimi lazima avunje kabati (Apendeze) Mzee Baba.Isitoshe nilihofu kumpiga sound kwa sababu nilikuwa naogopa nisinyee kambi maana yule Mzee alikuwa ananilipa Fedha nzuri sana na nilikuwa naheshiamana nae sana.
Sasa siku moja nikawa nimetoka Rock city nimedondoka JNIA (Airport) kipindi kile Fast jet kwa ajili ya kuja kukabidhi kazi kesho yake, wakati nipo Airport akanitumia ujumbe kesho hatakuwepo kazini ana safari ya kwenda Zanzibar akaniambia niende moja kwa moja Ofisni kwao Posta Mpya nimkabidhi kazi nikasema sio ishu maana kama nitamkabidhi siku ileile ina maana kesho yake nitakuwa free kupiga Tungi(Bata) na masela.
Nikachukua Uber mpaka Posta nikamkuta Pisi Ofisini nikamfanyia presentation ya ile kazi yangu, akakubali kazi akafurahi sana. Ila Ofisi za wenzetu zina tofauti sana na sisi wa Bongo maana huwa zina Wine na wakati mwingine hata Whisky Mzee Baba sio kama zile Ofisi za umma hata Friji tu ni mgogoro. Akaniambia umepiga kazi kubwa kwa muda mfupi ila umefanya kwa umakini mkubwa sana.
Hakafungua kabati akamimina Whisky kwenye Glass akanipatia kidogo.... akasema najua hii unatumia hiki kiasi kidogo hakita kulewesha mpaka usahau kufika Hotelini ulipofikia.... Nikazuga kihaina nikaichukua nikasema sio mnywaaji saaana kivile uku natabasamu... Yeye akamimina Wine kiasi akaanza kunywa.... akaniambia ana dakika 5 itabidi awai home kwa ajili ya Safari ya kesho.
Sasa cha ajabu kwa zile dakika tano za kupiga Story japo sijazoena nae saanaa akaniambia....Kwa jinsi ulivyobobea na fani yako ya ukadiriaji Majengo, Je mimi P... naweza kufikia kiasi gani za gharama za ujenzi?Akaanza kuucheekaaa.......
Mzee Baba nikajikuta nimeropoka tu..... Hivyo ulivyo pamoja na nguo au bila kuvaa Nguo?...... Pisi ikachekaa mpaka Wine ikampalia kooni... Akaniambia najuaga siku zoote uko Serious sana kumbe ni Charming hivyoo...... Akasema Nataka nijue gharama nikiwa na nguo na pia nataka nijue gharama bila kuvaa nguo?.....
Nikajikuta nimeropoka tena ... Nitafurahi kama ningekukaridia gharama hizo ukiwa huna nguo...(Nikajilaumu kimoyomoyo sana na ule ulopokaji wangu kwa mtu ambae sijazoeana nae)..
Ila cha ajabu Akacheeka tena..... na kutoa tabasamu bashasha akasema, muda umeisha nahitaji kurudi Nyumbani kujiandaa kwa safari ya kesho... Nikajibu Pouwa safari .. Njemaa mimi nikasepa zangu Sinza....
SOON NAMALIZIA NGOJA NIKABIDHI KIMEO CHA WATU KWANZA .......