Baada ya yeye kuja chuo tuliienjoy sana sababu tulikuwa majiran, kwa kifupi alikuwa analala kwangu, na nilimtambulisha kwa demu wangu ambaye sasa ni mke wangu (nimtambulisha kama shemu wangu demu wa rafiki angu). Ilikuwa akipiga simu mchumba wangu inabidi akae kimya kabsa ili tusijulikane.
Kibaya akaanza kumfanyia dharau jamaa yake ambaye ni rafiki yangu, ikawa kitu kidogo tu anazua ugomvi ikafikia jamaa ananiuliza vp au ameshahalibika chuoni, mi nampa moyo tu kuwa akomae mapenzi yanachangamoto, ila ilifikia wakaachana kabsa.
Penzi letu likaendelea vizur sasa akiwa hana mahusiano na my frnd,
Kuna kipind mchumba wangu akafunga safar kuja, nikamjulisha kuwa tusionyeshe mahusiano yoyote ili wyf to asishitukie, kweli akaja na tukawa tunapishana kwa kolido si tunaenda kuoga, siku chache baadae nikawa simuelewi tukikutana hanichangamkii tena, nikamtafuta kibwetani chuo, alinipa jibu na kuniambia namdharau sana na atanionyesha.
Nilihofia nikahisi atakuja kuzingua, so nikafanya mchakato demu wangu akaondoka, alivyoondoka demu hakutaka tena kuongea na mimi, kuna jamaa tulikuwa tumepanga nae nyumba moja na tulikuwa class moja ndo akawa karibu nae, ikawa anafanya ile makusudi kunionyesha mpaka wakaingia kwenye mapenzi, vyumba vilikuwa jiran sana...dogo akawa kila nikiwepo anaingia kwa jamaa na kelele zake anazopiga siyo za kawaida, nilimpotezea sababu sikuwa na future nae,
Kodi yake ilivyoisha, alihamia kwingine, tukaacha kabsa kusemeshana akiniona anachuna tu, ilipita miez sijamuona kuja kuambiwa na rafiki yake kuwa alikamatwa na alidisco....Nilisikia aliomba upya chuo flan na sasa anamalizia ualimu....Najua ukisoma utajijua tu, nakumbukaga unavyocheka my shem.