USHAWAHI KUAPA UTAKAA UFANYE MAPENZI?
Ilikua 2014/2015 kama sikosei nilikua nahamu ya kuolewa haina mfano katika pitapita huku na huko nikadondokea jf..huku na huku kusaka mchumba na marafiki,nikampata jamaa mmoja aisee alikua akikutext unaloa yaani..lakini nikiri wazi nilivyoonana nae sikuwa pleased sana ila nilipenda busara zake na ushauri..jamaa alinielewa tu ila nikaanza sasa kumzungusha nahisi hii kitu ilimuuma.
So nikaendelea na mambo yangu nikakutana na jamaa mwingine moyoni nasema hata kesho anipeleke kanisani akanioe hahahha mbaya sana
Kufupisha stori huyu jamaa alinipiga matukio kadhaa lakini kubwa ni kanga yangu ambayo nikiendaga kwake naiacha nikioga nikakuta haipo,tukataguta nae ila baadae alikiri alimpa msichana wake aliyekuja kwake...dah kama siku mbili tena naenda kwake nakuta chanuo la mwanamke..
Nikasema imetosha ngoja nimtafute jamaa yangu rafiki yangu mwingi wa busara...hahaha
Nikawasiliana nae tukakutana sehem tukaenda hadi kwake yule jamaa alinila bila mazungumzo (hakyanani alipanga kunila kimasihara) yaani hakuzungumza ila nakumbuka nilikua na akili timamu alivaa kondomu.
(Ukiwa na stress usiende kwa mwanaume)
Yaani hata maji ya kunywa sikunywa nikarudi home stress kama zote yaani hazijaisha aisee
Mi na mshikaji alienila hatuchat tena yaani kama hatuhawahi kukutana.hata umefika salama hakuniuliza.
Maisha yakaenda kama miezi kadhaa hivi nakumbuka siku napigiwa simu na fundi wa maji kwa alipokua anakaa jamaa yangu maana siku wanakuja kufunga maji nilikuepo kwamba kuna bomba humo ndani la kufunga wanatengeneza maji...huyo jamaa alikua kasafiri ,so nikawaambia mimi siwezi fika muda huu niko mbali(ukweli sikua hata nafunguo maana tulishagombana sana)
Akakata baada ya dakika kadhaa akanipigia simu "kuna binti yule wa kazi tumemuona usijali ngoja tumwambie afunge"
Huyo binti wa kazi nilikua nahis jamaa anapiga nikamwambia mrudishe..kumbe kaenda nae karudi nae...duh nililoa maji,nikaomba lift kwa kaka mmoja kwamba najisikia vibaya anipelke home (NDO AMEKUJA KUWA MUME WANGU) .
Aisee ile siku nilihisi dunia inanilemea ila nikajipa moyo yatakwisha....huyu kaka alienipa lift nilikuna kumweleza scenario siku mbili baadae kwa hiyo akawa ananifariji fariji hahaha nae ananitege nijae.
Tukaanza urafiki wa karibu na huyu ambae ndo mume wangu miezi kama mitatu minne ikapita hapo jf naingia kwa kubip sana...eeh siku hiyo nachek sm nakutana na meseji kulikua na rafiki yangu humu wa kike ambae nilia na namba yake (anajijua) akanitext kwamba FLANI KAANZISHA UZI KWAMBA NI MUATHIRIKA WA UKIMWI NA HUMO NDANI UNATAJWA
Huyo aliyenanzisha ndo yule aliyenila kimasihara.sikujibu msg ila niliikaa kama masaa nafikia jamaa alivaa kondomu au akuvaa nilivuta hisia mpaka nikakumbuka alivaa tena ya pink alitoa kwenye begi jeusi kuukuu hapo chumbano
Hahahahahahah aiseee niliapa mimi kuna kumpa mtu uchi labda anibake...
Nilikaa takribani miaka miwili siingii jf kwa uoga uliotukuka.
Uzi wenyewe sikuusoma nimekuja kuusoma mwaka huu hahahaha
Nilikaa kama miezi 8 hivi sina nyege yaani sinaaa kabisa..
Ki ukweli sikwenda kupima mpaka nikaolewa japo jamaa alikuwa anapima mara kwa mara kulingana na kazi yake so nikawa na kuwakika inavyotaka mpaka kuja kupata mimba ile ya kupimwa clinic kwa lazima hahahahhaa ndo nikajua sina kitu.
Nilikuja kumuuloza jamaa mwaka huu akasema aliandika kufurahisha genge
Ila jamani
Kama una stress bora ufunge kwa maombi na maombezi usipeleke papa kwa baharia utajuta..