Nina kama wiki nne nipo bush kwa shughuli za kilimo. Mwenyeji wangu hapa ni mdogo wangu ambaye ni daktari kwenye hospitali ya Kijiji. Maisha hapa ni mazuri, Kijiji kimechangamka Sana. Nilikuwa nahitaji vibarua wa kunisaidia kazi za shambani ndipo mdogo wangu akanikutanisha na binti mmoja na akaniambia nikihitaji vibarua niongee na huyo huyo binti ana connection zote za hapo kijijini.
Mambo yalienda vizuri, mwanzoni binti aliniletea vibarua kumi Mara ya pili ishirini na kazi ya shamba ilienda vizuri Sana! Taratibu Yule binti akaanza mazoea ya kupenda Sana kuchati na Mimi hasa wakati wa usiku na nikichelewa kujibu au nisipojibu analalamika sana. Kwa kuwa yeye ndio msaada wangu niliamua kutokumkwaza nikaamua kuwa nae tu karibu, sikuona shida katika hilo. Akawa anakuja hata nilipofikia anapiga story na kurudi kwake.
Taratibu story zikaanza kuzagaa kijijini kuwa Mimi natafuna yule binti na mtu wa Kwanza kuniletea hizo habari ni binti mwenyewe. Akasema anakosa raha maana anasemwa Sana na kinachomuuma ni kwamba Jambo lenyewe sio la kweli. Nikamwambia huwezi kuwazuia watu kuongea chochote wanachoona kinafaa, fanya mambo yako kama kusemwa huwezi kumzidi diamond ila umewahi kumuona analalamika?
Basi binti akaelewa maisha yakaendelea. Hazikupita siku tatu kaja gheto usiku na hoja zile zile eti hali imezidi kuwa mbaya anasemwa Sana! Yaani anakosa raha, moyo unamuuma. Nikamuuliza kama utani tu au tufanye kweli ili wafurahi? Binti hakujibu. Nikasema huyu atakuwa anataka mashine huyu, leo simuachi!
Mzee nikamsogelea karibu mithili ya Mithuni Chakaroboti, nikamtazama usoni kwa macho ya matamanio, nikamshika paja! Nikakohoa kikohozi kisichosikika, muda huo binti anahema juu juu kama kinda la ndege. Muda huo najiona kama Akshey Kumar kwenye kuchi kuchi hotahe, nipo serious kichiz na Jambo langu. Hatimaye binti akanipokea, akazungusha mikono yake shingoni kwangu huku anatazama chini kwa aibu, mambo mseto!!
Sinaga busara kabisa kunako sita kwa sita, nikamfungua kanga aliyokuwa amevaa, nikakutana na sketi, nikaifungua kifungo dadeki mtu anatafunwa leo! Nikapekenyua chupi nikataka nianze kuichezea nanii yake ghafla mlango ukagongwa!
Ndio nikakumbuka nilikuwa na miadi na mdogo wangu (daktari) Kuna hela aliniazima akasema atakuja kuichukua usiku, basi akawa amefika akagonga hodi nikatoka kumpa hela yake. Akashangaa Sana maana hakuzoea kuishia mlangoni akifika pale gheto. Nikatoka kumsindikiza kidogo katika story story ndio nikamwambia gheto nipo na yule binti uliyeniambia nimtumie kupata vibarua.
Akashangaa Sana. Akaniambia yule binti kaathirika na yeye ndio aliyempima Mara ya Kwanza na huwa anampa ARV Mara kwa Mara pale hospitali. Akasema kama siamini kesho yake niende hospitali atanionyesha udhibitisho. Nilitoa macho kinoma! Kwa hiyo nilikuwa nakonektiwa kwenye grid ya taifa kirahisi namna hiyo yaani.
Sikutaka kupaniki niliporudi nikamwambia bi dada nimepata dharura kama vipi aje kesho maana Mimi mwenyewe natoka. Basi nikatoka naye, yeye akaenda kwao Mimi nikaenda zangu bar nikaagiza Serengeti light nne nikanywa weeeh... Nikalewa nikarudi kulala huku nikisali sala ya baba yetu uliye mbinguni.