Niliwahi kujishikiza katika ofisi moja ya Mtanzania mwenzetu, baadaye nikapata kazi ya uhakika hivyo ila ikabidi nitoe taarifa za kuacha kazi.
Baada ya mazungumzo na mwenye ofisi akaomba nitumie walau wiki mbili kumwelekeza na kumkabidhi kazi mwajiriwa mpya ambaye alikuwa binti.
Zoezi la kuelekezana kazi na kukabidhiana likaanza.
Ijumaa ya wiki ya kwanza binti akashauri kwamba kama nina muda basi tukutane weekend ili tuelekezane vizuri.
Sikuwa na kipingamizi, binti anapendekeza aje kwangu ila nikakataa maana mazingira niliyokuwa naishi huko uswahili ikifika weekend ni muziki tu.. Hivyo tukakubaliana mimi niende kwake.
Jumamosi mapema nikafika alipopanga huyu binti baada ya kuscan mazingira, nikauliza shemeji yupo wapi? Binti akacheka kisha akajibu "hamna shemeji hapa, wanaume wenyewe wa siku hizi majanga tu.
Tukaelekezana pale mpaka muda wa kula, binti akaandaa msosi nami nikakaribishwa mezani. Balaa likaanza kwenye kuninawisha, binti akaninawisha kama mtoto, yaani anakumiminia maji huku mkono mmoja anakuosha viganja vya mikono, nimepigwa na butwaa binti akaniambia "tulia Tanga wanaume wananawishwa hivi"
Baada ya kula nikanawishwa kwa mtindo ule ule. Hapa imani ikanishinda, nikamwambia unanitia majaribuni ujue.
Binti akajibu "usijali nitakutoa majaribuni" huku akipeleka vyombo jikoni.
Tuliporudi kukaa binti Akaniuliza "tunaendelea kufundisha au tukatoane majaribuni. Sikuwa na namna, nikauza mechi kwa binti wa kitanga.