Nimeona sio vibaya namimi nikishea experience yangu kidogo kwenye hili jukwaa.
Miezi 3 iliyopita nilitoka jijini Dar na kwenda Mwanza kwa ajili ya kuwasalimia ndugu jamaa na marafiki wengine pande hizo. Kwakuwa nimewahi kuishi Mwanza miaka ya nyuma, haikuwa ngumu kuayazoea mazingira na kupiga misele maeneo mbalimbali nikienjoy mandhari nzuri ya Mwanza.
Siku moja nilienda kupata break fast katika mgahawa mmoja ambao huwa upo jirani na kampuni moja maarufu jijini Mwanza. Nilizoea kwenda kwenye mgahawa huu kutokana na usafi pamoja na mazingira mazuri ikiwemo ubora wa chakula. Siku hiyo nimefika ndani ya huo mgahawa, nilikutana na wadada fulani warembo ambao wanafanya kazi kwenye ile kampuni iliyo jirani na mgahawa ule, walikuwa wanamalizia kula na baadhi walikuwa wanaanza kuondoka. Nilikuja kufahamu badae kumbe huwa wanakula pale mara kibao na siku nyingine mgahawa huwa unapokea oda za chakula na kuwapelekea wafanyakazi ofisini.
Baada ya kuingia, nilienda kukaa iliyo mbele ya meza ya wale wadada waliokuwa wanamalizia kula. Walikuwa ni warembo hasa ila sikuwa nimewaza chochote juu yao. Wkati wanatoka nilimsikia mmoja wa wale wadada (binti tu wa 20's) akimwambia mhudumu kuwa HAJASHIBA hivyo bado anasikia njaa. Aliongea kwa kutania huku anatabasamu na kutoka nje/kurudi ofisini kwao. Walipoondoka, shetani wa ngono aliniingia na nikaona nifanye kitu kuhusu huyu dada. Nilimuita mhudumu na kujaribu kumpeleleza yule dada aliyelalamika kuwa ana njaaa. Hakuwa pisi kali kivile ila anafaa kwa matumizi ya kibaharia. Baada ya kupeleleza kwa mhudumu, niligundua kuwa yule dada ofisi yao ipo jirani na mchana watapelekewa chakula kutoka kwenye huu mgahawa. Basi, nikaona isiwe tabu, nikaongea vizuri na yule mhudumu nae akanihakikishia kuwa anamfahamu/anamkumbuka vizuri yule dada aliyelalamika kuwa hajashiba. Nilitoa hela nikampa yule mhudumu kwaajili ya kumpelekea lunch yule dada mda wa mchana na nikaandika namba yangu ya simu kwenye kikaratasi ili yule dada akipewa chakula apewe na hii namba. Pamoja na ile namba niliandika maneno machache tu ya kumtaka ale chakula nilichomnunulia kwa maana nilimsikia akilalamika hajashiba na kama hatojali atanipigia kunishukuru. Baada ya kukamilisha taratibu zote, nilimpoza mhudumu elfu 5 ya soda nikasepa zangu.
Sikurudi kwenye ule mgahawa kuulizia kama ujumbe umefika au lah ila muda wote nilikuwa attention kusikilizia simu yangu kama kuna namba mpya itaingia. Sikupokea namba yoyote hivyo nilikaa kinyonge nikiamini labda mhudumu alipuuzia. Baada ya kufikiria sana na kwakuwa nilikuwa nishaifahamu ofisi yao na nimemfahamu jina huyu mtoto (jina niliambiwa na mhudumu wa mgahawa), na kwakuwa home sio mbali na pale ofisini, niliamua kupita pale ofisini kwao, nikakutana na mlinzi kijana kama mimi tena mjanja, nikampanga kuwa nahitaji namba ya yule dada na bila ajizi akanipatia. Baadae jioni kuelekea usiku, nilimpigia yule dada na alinikumbuka fresh na akawa amekubali kuwa alipokea mzigo wangu. Tuliongea pale tukataniana na tukapiga story nyingi sana hadi usiku mrefu. Kwakuwa nilikuwa natumia gari labro sometimes, nilikuwa mara kwa mara namcheki nampitia kumpeleka home na kumrudisha home kwake maana alikuwa anaishi mwenyewe. Baada ya mazoea ya hapa na pale, nilimtoa dinner siku moja na nikajaribu kumueleza hisia zangu, hakutaka kukubali wala kukataa hali iliyonipa kujiamini zaidi. Niliendelea kumjali kwa vitu vidogo vidogo kama salamu, zawadi, lift ya kwenda na kurudi kazini mpaka nikaona mtoto ameniamini na amekolea. Simu zake nyingi akiwa na mimi alikuwa anpenda kwenda kuongelea chooni, sikujali maana niliamini lazima atakuwa na bwana ake.
Hatimae bila vikwazo au ugumu wowote, juzi kati hapa nilifanikiwa kula tunda la huyu binti. Mpaka mda huu bado nipo nae, mtoto amekolea sana na amekuwa addicted namimi. Hapa nilipo najiandaa kurudi dsm maana mission iliyonileta huku Mwanza imekamilika (nilikuja kusalimu ndugu na kufanya project za ofisi). Muda sio mrefu nitamuacha katika mataa japo namhurumia maana yeye amedata kabisa.
Hivyo ndivyo nilivyokula tunda kimasihara. Inaonekana mtoto hajapelekewa moto mda mrefu na nahisi bwana ake amesafiri (hayupo Mwanza) muda mrefu kidogo. Nawashauri wakuu, msiwaache wapenzi wenu bila kuwaona muda mrefu maana mtakuja kuwalaumu bure.
Nawasilisha.