Nilikuwa natoka Dodoma kwenda Dsm, kwenye siti nikawa na jirani yangu wa kike.
Huyu jirani alinikuta nimeshakaa upande wa dirishani lakini hakunisalimia, Yuko bize na simu yake tu. Na mimi sikuwa na hiana nikauchuna tu.
Tumefika sehemu moja hivi ambayo siiukumbuki, mdada akaanza kuinama inama kuashiria kama ana maumivu tumboni. Basi nikawa namuangalia tu anavyo hangaika. Nikisubiri simu yake impe msaada!
Hali ilivyozidi, roho ikaniuma nikamuuliza vipi dada, una tatizo gani! Aliniangalia tu akanyamaza! Afu akainama Tena. Mashauzi kishenzi. Ikabidi nimgonge tena mgongoni, dada pole! Nini tatizo? Kimya!
Nikamuuliza hilo tumbo ni la period? Akasema nini? Eti unasemaj? Akahamaki! Mi nikamwambia, hilo tumbo ni period? Akanikata jicho balaa!
Nikamwambia wew dada, Mimi ni Daktari nakuuliza hivo makusudi ili nikusaidie! Sasa wew unaleta mashauzi wakati unaumia! Akasema linauma tu, linauma!
Linaumaj! Linauma kwa chini! Nikamwambia pole akasema ahsante. Nikatoka nikaenda kwa konda, nikamwambia, aisee mdogo wangu anaumwa, tukifika Gairo naomba nimchukulie dawa fasta. Akasema poa.
Tumefika Gairo kweli nikachomoka nikamnunulia dawa na maji. Nikafika nikampa, akameza, Safari ikaendelea! Akasema ahsante Dr, nikamwambia poa.
Baadae nikaona kama dawa zimesaidia, maana kule kuinama kukawa kumepungua. Tumefika Kibaha, nikamuuliza. Hilo tumbo lako huwa linakusumbua Mara kwa Mara?
Akasema, ndiyo. Nikwambia basi, kama una muda Dar, ukisettle tuwasiliane, Kuna majani fulani yanaota kule ninakokaa, kwa Kiswahili siyajui nayafahamu kitaalum tu na kilugha! Ukitulia uje uchukue, yatakusaidia Sana. Chukua namba! Akachukua kweli.
Alivyofika tu, Dr.mi nimefika! Dr...sijui nini! Dr. Am happy! Asubuhi, hope umeamka salama. Dr.....! Tukachati chati! Siku ya tatu akanambia naomba location, nikamwambia. Nikachuma majani fulani ambayo hutumika kwa ajili ya kutibia nyongo, nikachemsha na kumwekea kwenye chupa!
Amefika tukakaa kaakidogo, nikampeleka jikoni tukaandae chochote. Huko ndo mambo yalikoanzia. Nilichogundua ilikuwa ni haki awe na mashauzi, maana alikuwa mtamu na anajua kusakata rhumba! Akawa ameliwa.
Alikuja kugundua mi si Dr ni mchumia tumbo tu, lakini mwenye roho ya huruma. Ameshaolewa!
Ahsante sana B!