Ulishawahi kula tunda kimasihara?
Jaman nimerud nyumbani nikawa busy na homework za watoto Baba P nae yupo wiki hii kwangu hvy nitaendelea kesho na story au jtat nikiwa dukan.
Naona mnaulizia home mama tuliwasiliana nikiendelea na story mtaona jinsi navyoheshimika home na hakifanyiki kitu bila kuambiwa
Kuna mwanaume anayeenda hadi China asiijue Jamii forums na akaaona haya unayoyaandika?

Wewe ni dume na hii ni chai
 
Basi baada ya pale Baba P akawa kama amenisusa hapigi simu hanitafuti kama wiki 3 zilipita, yani nilihisi kuchanganyikiwa na nilivyokua nampenda kila siku nikawa nalia. Shoga angu asha akasema nijikaze kila kitu kitakua sawa tu nimpe mda hapo naendelea kwenda dukan na fund anafanya Kaz vizur tu. Basi siku 1 usiku naona muamala wa laki 5 kwenye simu yang kutoka kwa wakala haikua no, nikabaki nafurah nikafikir amekosea nikasema ngoja nisubir nitajua, nikalala asubuhi nimeamka nakuta missed calls za Baba P na message kuisoma aliandika " hiyo pesa nimekutumia katoe hiyo mimba bila hivyo mm na ww basi" nililia nikampigia da asha alikua ashaenda job akasema wala usitoe mdanganye sawa utaenda. Basi nikaenda kazini kama kawa mteja alikuja kuweka pesa nikawa sina float ikabidi nitoe Ile pesa. nikampigia Baba P nikamwambia sawa nimekubali nitaenda kuitoa akasema jioni atakuja unafunga saa ngapi nikamwambia saa 1. Niliporud nyumbani nikakuta amepaki gar kwa nje ananisubir lakin nilikua nimeongozana na Kaka wa pale (mmoja wa wale wapangaji wa2) alikua ananitongoza mara nying mm nikawa nampotezea. Basi Baba P akashuka fasta akaniuliza mbele ya yule kijana huyu ni nani nikwambia mpangaj mwenzang tunaishi nae huku ndani akanyamaza Yule Kaka akapita ndani na sisi hao tukaingia.
Baba P alikua ameniletea kuku ametengenezwa kabisa nikapokea nikamwambia tule akasema yy ameshiba nikala kias nyingine nikaweka kweny frij. Hapo hatusemeshani mm kimya akaanza kuniuliza mbona una huzun hvy au sababu umeniona mm nikanyamaza akasogea akanishika mikono nikaanza kulia akasema nisamehe sina jinsi mm sikutegemea itakua hv. Nikanyamaza kimya akawa ananitomasa mm kimya wala simpi ushirikiano akawa ananiomba msamaha na kunibembeleza nimkubalie mechi mm nikamwambia hapana mpaka nitakapotoa hii mimba ndio tutaendelea akaniuliza lini utaenda hospital nikamwambia nimemuomba da asha anipeleke sehemu weekend akasema sawa jikaze baby wang ooh mm nakupenda ikifika kipind nataka mtoto na ww tutazaa tu nikamwambia sawa. Akaniuliza kwa hiyo unipi Leo maana mda umeenda nikamwambia sitaki labda ulale huku akasema sitaweza unajua mke wang ashaanza kuona kama nimebadilika hivyo sitak ajue lolote nikamwambia sawa nenda nitakupa siku nyingine ukilala basi akanyanyuka akaondoka. Mm nikaenda kuoga nikawa naangalia TV Hadi saa 4 imefika nikalala zang. Ilipofika saa 5 naona Baba P anapiga simu sikupokea nikahisi labda mke wake, mara kioo cha dirisha langu la chumbani kinagongwa niliogopa nikaamka nikawasha taa nikachugulia namuona Baba P nikafungua dirisha akasema baby wang nimerud tulale nimekumis nimeshindwa kwenda home nifunguliee [emoji23][emoji23][emoji23] nilicheka nikaenda kufungua akaingia kuoga kwanza then mamb shata shata na hv da asha alikua ananifundisha kumhandle mwanaume kitandan nilitumia ujuzi wangu woteeee [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] tulilala hoi kuamka saa 2 Baba P akakarupuka speed akaondoka (sikuwa napenda kumuuliza au kufatilia habar za yy na mke wake hata akitaka kuniambia nilikua namkatisha) da asha ndio alinifundisha nifanye hivyo itanisaidia kuondokana na stress au woga. Basi nilienda kazin kwangu kama kawaida Ila siku hiyo Kuna baadh ya spea zilikua zimeisha kwa mara ya I natakiwa kuongezea mzigo dukani nikamtext Baba P hakujibu Ila baada ya masaa 3 hv alinipigia akasema jitahid uongee na fund akupeleke maduka ya jumla kkoo maana mm sitaweza kukutumia mzigo kila mara jitahid ujitegemee, nililalamika lakin akasema ashanipa mwanga hvy nijiongeze na yy ratiba zake zinambana hawez hiyo Kaz na anahofia mkewe atashtuka hvy nisimtafute mpaka yy aanze. Basi nikamwelewa ila sikupenda nikawa nimenuna join da asha akanipitia dukan nikamwambia akasema huoni ni vizur anajitenga na biashara yako na ukijitegemea ww hatoweza kukupangia pesa yako na utakua huru kufanya maendeleo kweli nikamwelewa.
Basi Baba p hakunitafuta tena had baada ya wiki 1 akaniuliza ushatoa Ile mimba nikamwambia bado ni wiki ijayo akalalamika akasema nafanya kusudi nikamwambia lazima nitafute sehemu nzur kwa ulinzi wa afya yangu akasema utajua mwenyew utakachofanya lakin jua sipo tayar kuzaa na wewe kwa sasa. Baada ya kuongea nae nikawa nawazia ila nikajipa moyo uzur biashara ninayo nitapambana niweze kulipia Kodi ya nyumba na kumlea mwanangu. Baba P akawa anakuja kwa wiki mara 2 hv tena usiku usiku na alikua halali mara zote lakin nilihakikisha kwa bed nampa mautamu yoteee ( hapo nimemdanganya mimba nimetoa) basi akawa ana wasiwasi anaulizia kama umetoa mbona unazid kunenepa nikamwambia nimerizika Tu ( Uzuri mimba haikua ikinisumbua hata Ile sijui kutema mate wala sipati). Mimba ikiwa na miez mitatu na nusu Baba P aliniaga anaenda tena China kufata mzigo lakin hakusema anakaa mda gani tukawa tunawasiliana WhatsApp usiku tu.
Mimba ilipofika miezi 4 nikabidi nimwambie ukweli tu kwamba sikutoka na siwez kufanya hvy kama ataniacha ni sawa nitaendelea kumlea mwanangu. Alipaniki akasema mm najidai sio muongeaji kumbe jeuri hvy bas kuanzia Leo nimekuacha na nikija utarudisha kila pesa yangu niliyokupa.
Nilipanic nikawa nalia tu ndan usiku nikawaza akininyanganya mm naelekea wapi nikanyamaza hata sikupata usingizi hiyo siku. Kesho yake nikamwambia da asha akasema achana nae usimtafute anatishia nyau na akija kukufanyia fujo mpeleke police na umkane hujawah kumjua na kweli nikakubali wazo lake. Baba P akawa ananitumia message za vitisho nikamwambia ukiendelea nakuja nyumbana namwambia mkeo kila kitu, akanyamaza akawa ameniblock kila mahali except fb (nilijua hili kwani siku moja nilipost picha nipo na da asha na wababa wawili [emoji23][emoji23][emoji23] tulitoka mtoko na baby daddy wa da asha sasa huyo baby daddy alikuja na rafiki yake ) kumbe Baba P anafatilia post zangu FB nashangaa siku hiyo hata sijafunga duka kaja (hapo mimba ina miezi 5) maana alikua ana zaid ya mwez hajaja. Akasema funga duka twende nyumbani tukaongee basi tukaenda kufika akaniomba msamaha akasema sawa amekubali tulee mimba sababu bado ananipenda na hatak kunipoteza nikamwambia sawa hamna shida. Basi alilala siku hiyo na kama kawaida mapenz motomoto na mimba yangu ilimpenda sana nakumbuka hadi niliendaga kumfanyia shopping kkoo wakat nilikua mbahili wa pesa hata kununua tu nguo zang sitoi pesa yangu [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] Aliendelea kuja mara moja moja kwa wiki had mimba imefika miez 8 akaenda chini tena kufatilia mzigo ( Yani Kuna kipind walikua wanamtumia na mara nyingine alikua anaenda mwenyew kutokana na biashara ilivyo kwa maelezo yake).
Basi nilibidi nimkabidh Yule fund duka anishikie kwa muda hapo bado wiki 2 nijifungue.
Baba P alikua ananipigia WhatsApp kama kawaida akaniomba no za shoga angu asha nikampa akaongea nae akamwomba anisaidie kwa mwez mmoja asiwe anaenda kazin had nijifungue ( nakumbuka da asha wiki 3 nzima alikua na mm bega kwa bega had nikajifungia na Baba P alimpa milioni I kama zawad). Nilitafutiwa hospital fulan ya private nzur na Baba P aliongea na rafiki yake doctor aliyekua anafanya kazi hapo. Nilijifungua mapacha wa kiume [emoji8][emoji8][emoji8] nakumbuka siku hiyo tupo na da asha aliwapiga picha akanitumia Baba P jaman alifurahii ananipigia video call analia anasema tu asante mke wangu [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] wakat sina ndoa nae. Alifurahi akasema atamtuma dada yake aje kuniona na atarud baada ya wiki 1.
Nilikaa hospital siku 3 tu maana nilijifungua kawaida na dada yake Baba P alikuja hospital kesho yake na vitu vya watoto kibao akanipelekà home. Basi nikawa nimezoeana na wifi sasa akawa anakuja na aliwapenda watoto mara ananisifia ooh umempa Kaka angu heshima maana alikua na watoto wa kike tu sasa amepata vidume 2 mm nafurah tu. Niliendelea vizur Baba P akarudi akaja kuwaona watoto alikua analia siku hiyo kwamba angewauwa vidume vyake ( huwa anawaita hvy) basi mapenzi yakarud kama yote on spot akaniambia inabid nikununulie kiwanja nikujengee haraka maana hata mama akija utamlaza wapi au dada wa kazi nikamwambia nipange nyumba kubwa akasema hatak wanae wapate shida Mimi kwangu magoli tu [emoji4][emoji4][emoji4][emoji4][emoji4]
Basi baada ya mwez 1 akaniambia anafanya finishing nihamie mbweni Kuna nyumba alikua amejenga ilikua bado finishing nikamwambia mkeo atajua mm naogopa akasema ni lazima niende na amefanya kwa ajili ya wanae. Duh nilikua na wasiwasi dada asha akasema kubali wala usiogope na wifi akasema lazima watoto wapate maisha mazur kwan Kaka yake uwezo anao.
Jaman watoto wamefika miez miwili tu mm huyo tumehamia mbweni na mama mkwe kaja kuwaona wajukuu zake. Baba P ilibid amwambie mke wake ukweli kipind hicho ila ilikua ugomvi mkubwa had Baba P akahamia kwangu mbweni. Nakwambia wanangu ni wazuriiiii utasema wazungu wamefanana na Baba Yao sema nywele na weupe wamechukua kwangu utasema half-caste yani familia nzima ya Baba P waliwapenda mpaka Leo.

Itaendelea
Waishi mbweni sehemu gani mkuu
 
Sentence case: Nakumbuka 2015 nimemaliza kidato cha nne, mama yangu akaongea na mama mdogo nikakae kwake Dar huku nikisubiri matokeo. Basi baada ya wiki nikaja Dar, nikapokelewa vizuri tulikua tunaishi Tabata. Hapo nilikuwa na bf angu wa kijijin alikuwa kinyozi wa saluni ndio niliyeanza nae mambo ya mapenzi. Sasa huku kwa mama mdogo niliishi vizur maisha safi nikanenepa na kunawiri, kusema ukweli mm ni mrembo Sana (umbo la kibantu nywele, rangi na sura ya kiarabu) na inasemekana baba yangu ni mwarabu Ila mama alimsingizia mimba kwa step dad hivyo nilipozaliwa ilibid Bibi anichukue, kunilea na mama alirudi kwa step dad wakaendelea na maisha.

Maisha yaliendelea nikawa namsaidia mama mdogo kuuza genge lake na yeye anakaa dukani hivyo nilikua nameet watu mbalimbali na nilikuwa natongozwa sana lakini mama mdogo alikuwa ananisisitiza sana kuhusu kujilinda hivyo sikuingia kwenye mapenzi na yeyote. Baada ya mwezi hivi matokeo yakawa yametoka bahati mbaya sikufaulu nikawa tu home nasikilizia watanisaidia vipi.

Tumeingia mwezi wa pili shemeji yake mama mdogo alikuja kukaa na sisi pale kwani alikuwa anasomea uwakili. Tukawa famili ya watu sita (mm brina, mama mdogo na mume wake, huyo shemeji ( tumuite D) na watoto wawili).

Nakumbuka siku moja tulifunga mapema dukani nikawahi kurudi home nikapike kwani mama mdogo na mumewe walikuwa wanaenda kwenye harusi na watoto wasingeweza kubaki wenyewe kwani D alikua anachelewa kurudi huko chuo sabab wanasomaga hadi usiku.

Basi tumekula na watoto wakaenda kulala mm nikawa namsubiri D arudi ili nikalale, akaja saa4 nakumbuka ilikuwa Jumamosi nikamfungulia nikamuaga kuwa naenda kulala akasema subiria basi nimalize kula akaweka movie nikawa naangalia si usingizi ukanichikua nakuja kushtuka D yupo ananipapasa kifuani niliruka fasta maana nilikuwa na muda mrefu kweli sija do. Ghafla honi hiyo kina mama mdogo wamerudi huyo nikasepa chumbani kulala.

Kesho yake Jumapili nikamuita D nikaongea nae nikamwambia sijapenda ulichokifanya nilimind kweli akasema mara ooh mimi nakupenda fungua moyo wako nikubalie mm nikakataa. Tumeenda baada ya wiki naona D kila akirudi ananiletea zawadi mara anipe pesa mimi nikawa nazitunza tu kwenye mpesa yangu. Alijitahid kunispoil na kunibembeleza sana maana yeye alikuwa ana mshahara pale alikuja tu kuongeza masomo. Mimi nikawa namkazia nahofia mama mdg akijua itakuwa noma.

Ikawa imepita mwezi D ananisumbua tu na hachoki na mimi nilikuwa nasubiria kuenda chuo cha mapishi coz ilikua ianze mwezi wa 6.

Sasa kumbe baba mdgo alikuwa ameshaanza kuhisi D ananitaka akawa anatufatilia. Siku moja wakatoka out yeye baba na mama mdogo na watoto, D aliambiwa aende akagomesha akasema ana kazi za chuo, mm kama kawaida nikabaki dukani. Jioni saa 1 nikafunga nikarud ili nipike. D mara aje jikoni aanze kunibembeleza mara anivute na kunishika dah nikawa nawaza nimekula pesa zake nyingi kwa muda mfupi asa leo nimepatikana. Nilijaribu kujitoa lakin nikashindwa kutokana na D alinizidi nguvu plus nyege [emoji23][emoji23][emoji23]

D kanibeba huyo mpaka sebuleni tukawa tupo kwenye romance na ashk ashk hatari na nilikuwa natoa miguno kwa saut ya juu. Kumbe mama mdg aliwah kurud home kuja kupokea mizigo ya dukani kwani ilikuwa iletwe kesho na pesa hakua ameacha wala maagizo yoyote.

Duh alikuja speed na geti lilikua wazi tumerudishia tu mpaka ndani akatufumania katikati ya mechi [emoji849][emoji849][emoji849] ilikua patashika nilipigwa makofi D akawa ananitetea mama mdogo akaanza kulia na kumlaumu kwamba ananiharibu wakati tayari yeye ni mme wa mtu nilibaki nimetoa macho sikujua kama D ameoa na sikutaka sana kumchunguza coz sikumpenda and it was unexpected sex.

Baada ya lisaa baba mdgo karudi ulikuwa ugomvi mkubwa na kelele nyingi hadi majirani walikuja ikabidi niingie ndani D akaondoka basi nikajifungia nikalala nikawa nawaza naenda wapi na nimefanya nini ilikuwa aibu nalia tu kwani mama mdogo alikua anampigia simu ndugu zangu mama Bibi akasema ameshindwa kukaa na mm hizo msg nilizokua natumiwa nililia.

Asubuhi ilipofika kila mtu aliondoka bila kunisemesha mm huyo nikapaki nguo zangu chache nikasepa hadi Mbagala kwa shoga angu nilikuwa nimemzoea pale dukani yeye alikuwa anauza pharmacy. Nikamuelezea kila kitu akamwambia usirudi huko kijijini, tulia nikutafutie kazi hata za ndani, nikakubali basi nikawa nasubiria.

Wiki mbili zilipita nikapata kazi ya housegirl huko Masaki. Kuna mama jirani wa shoga angu aliniunganisha. Mshahara ulikuwa 50 nikaenda huko. Aise, kuna watu wana maisha! Yani matajiri haswa, familia ya kichaga, baba, mama, na watoto watatu.

Huyo baba tumuite Baba P na mama P. Watoto wao watatu wote ni wakike. Baba P ni mfanyabiashara mkubwa Kariakoo na mke wake alikuwa ni mhasibu taasisi nzuri tu ya serikali.

Mimi huyo nikaanza kazi, mama P akawa anashangaa binti mrembo kama mm kwanini nafanya kazi za ndani. Mimi kimya na nilivyokua mpole, akaongea na yule mama aliyeniunganishia. Akawa ananihoji kuhusu mimi, akamwelezea tu natokea familia duni na nimefeli kidato cha nne, ndio maana.

Muda wote mm nilikuwa napenda sana kujistiri majuba kwa sana na nilikua sivai nguo za wazi au za kubana.

Niliendelea vizuri na kazi na nikazoeana na familia ile, lakin Baba P mara nyingi alikua akiniangalia kwa kuibia na kwa wasiwasi hata akirudi home mama P hayupo, alikua hakai anaondoka...

Nitaendelea baadaye kusimulia kuhusu Baba P mpaka maisha yangu yamekua bomba!
Mi ni baba P mbona unamwaga kuku kwenye mchele mwingi
 
Back
Top Bottom