Nilivyokula Tunda Kimasihara na Kuambulia Kipigo cha Mbwa Koko huko Nairobi [emoji1139]
Mwaka 2012 nilijiunga na chuo kikuu kimoja nchini Kenya, ikiwa ni baada ya kukosa course niliyoazimia kusoma katika vyuo vya hapa ndani.
Hii ilikuwa mara ya kwanza kutoka nje ya nchi, na wonderful enough nilisafiri kuelekea jijini Nairobi peke yangu nikiongozwa na instincts za kibaharia. Ubaharia wangu unatokana na kusoma shule za boarding toka darasa la nne! Tena shule zenyewe mbali haswa na nyumbani; anyway story for another day.
Nilifika Nairobi jioni ya saa 12 na kuchukua taxi kuelekea eneo chuo kilipo. Nilipowasili nikapokelewa vizuri na wanachuo wenzangu wa higher levels (orientation crew) kwa ajili ya udahili na taratibu nyingine za usajili. Baada ya hapo tukaelekea dining hall for dinner.
Kesho yake asubuhi tukaamka mapema kujiandaa na siku ya pili ya orientation program. Generally, ukifika chuo especially privately owned, chenye hadhi ya kimataifa, haya ni mambo ya kawaida haswa kwa wanafunzi wanaotoka nchi tofauti.
Tuliendelea na orientation kwa wiki nzima, na baada ya hapo nikaanza kuona watu wanaongezeka kwa kasi ya ajabu, kumbe sisi tulipaswa ku-report wiki moja kabla ya wanachuo wazoefu ili kujua mambo mbalimbali kuhusu chuo ikiwemo sheria, taratibu, mifumo, mazingira na utamaduni wa chuo hicho na nchi kwa ujumla.
Ilikuwa siku ya Jumanne mishale ya saa sita na nusu mchana (ndio ulikua wakati wa kwenda dining hall kwa ajili ya lunch). Na kawaida ukifika dining unakuta mstari wa wanafunzi wenzako, unaunga kuelekea kwenye meza za chakula kwa ajili ya kuserve.
Nilipanga mstari nikiwa tayari nimeshaanza kupata washkaji, nikiwa na mwanangu mmoja (Mkenya) tunapiga story za hapa na pale. Wakati tunaendelea kusonga, nikamuona binti mmoja mdogo mdogo mzuri kweli. Alikuwa akitoka kuashiria ameshamaliza kula anaelekea darasa la mchana. Nilimuangalia toka anasimama kwenye meza yake mpaka akiwa anakaribia mlangoni, kumbe naye ali-notice. (Utajua badae)
Basi mshkaji akaniuliza mbona umemuangalia sana huyo manzi? Umemuelewa nini? Tukacheka, yakapita tukachukua chakula tukakaa kula na kuondoka. Jioni ya siku hiyo hiyo nikawahi kwenda dining kwa sababu nilikua sipendi kukaa muda mrefu kwenye mstari wa chakula na uzuri chakula huwa tayari kuanzia saa 12 kamili jioni.
Wakati naingia tu dining hall, nikaona watu wawili mbele kabisa wakiwa wanapakuliwa, na jinsi walivyo ilikua dhahiri ni wapenzi. Walitaniana, wakashikana mikono, huku wakibebeana chakula kuelekea mezani. Sikutilia maanani sana kwa sababu chuoni nilikua naelewa hayo mambo ya kawaida sana.
Nilipigwa butwaa baada kuchukua chakula, napita kuelekea mezani na kugundua kumbe yule manzi niliyemuona mchana, ndio huyu huyu namuona hapa na jamaa wanakula pamoja. Nikajisemea anyways, it's life. Nikala nikaondoka zangu.
Baada ya kama wiki mbili tatu nikagundua kuna genaral course natakiwa kuanza kuhudhuria kwa sababu lecturer amerudi. Ilikua Ijumaa mchana natoka dining kuelekea lecture room, nikiwa na rafiki yangu mmoja wa kike Mtanzania mwenzangu tunawahi class. Kwa mbali namuona tena yule binti wa dining hall, kwa mara nyingine. Coincidence Hizi!. Wakati tunapishana naye, akamsimamisha yule dada nilikua naye na kuanza kuongea naye. Mi nikaendelea mbele kidogo huku nikiwa nimepumguza mwendo kumsubiri bestie yangu.
Basi wakaagana kama baada ya dakika na sekunde kadhaa, tukaendelea na safari yetu kuelekea class. Tukiwa njiani nikamuuliza unamfahamu huyo dada tuliyepishana naye? Akajibu ndio, nilikua naye group moja la discussion last semester. Nikamuuliza Jina akanitajia, na safari ikaendelea.
Nimefika class tumekaa tunasubiri pindi lianze, ikaingia meseji kwenye simu yangu, number ngeni. "Hi, It's Jessy... Judy's friend. She gave me your number. Hope you won't mind. Have a nice class."
Mmmmh nikajisemea kimzaha tu, ila sikujibu ile meseji wakati ule. Lecturer akaingia, piga pindi pale kama saa mbili na nusu, tukachomoka. Nikaenda zangu hostel. Hostel zetu zilikua nje kabisa ya premises za chuo, so we're free after class. Kufika nikamjibu ile meseji. "Hi Jessy. Sorry for late reply, I had a nice class, I'm out now. Thanks for the wishes".
Akaja kujibu jioni kabisa. Tukachati kidogo jioni ile, akaniambia leo haendi kula dining hall, kama sitojali niagize pizza aje tule wote. Nikajisemea Woyooooo mambo si haya sasa. Bila hiyana, nikamwambia limepita hilo. Kweli mida mida nikaagiza pizza (sio hizi za Pizza Hut au Chicen Inn, kuna mwamba mmoja nje ya chuo alikua na fast food restaurant yake local ina aina zote za vyakula vya kisasa ila kwa bei ya wanafunzi).
Nikajitutumua nikanunua pizza ya Kshs 500, kwa kipindi hicho hiyo ilikuwa kama Tshs 8,500 hivi. Na soda mbili. Nikatuma meseji, pizza imekuja, nikatuma na jina la hostel na number ya chumba. Hapo nimepiga maji, unyunyu wangu wa mchongo, kitanda kisafi, ghetto murua kabisa. Nikakaa naangalia movie mdogo mdogo kwenye laptop.
Baada ya kama nusu saa hivi, nasikia mlango unagongwa. Fungua, mtoto huyu hapa. Tukasalimiana vizuri sasa ile face to face. Tukapiga story mbili tatu, nikatenga Pizza mezani tukaanza kula. Tumekula tukamaliza, tukaendelea na story. Tukaanza kuongelea movies, hapo sasa ndio nikajua weakness yake. Movies. Sikupoteza hata sekunde, nikachagua movie tukaanza kuangalia.
Sasa hizi hostel za wanafunzi zilivyokuwa designed ni for one person only. Kitanda ni 4/6, kuna kiti kimoja, meza moja ya kusomea, kasehemu kajiko, sinki halafu kwa pembeni kuna mlango wa kuingia washroom (self-contained).
Kwa hiyo wakati wote huo tunaangalia movie, tulikua tumekaa kitandani.
Mida ikaenda, bado yupo. Sikutaka kuuliza maswali mengi, nikazima taa, vua pensi na t-shirt. Nikamwambia na hii baridi si tujifunike blanketi tu? Hakubisha maana kweli kulikua na baridi, na saa izo ni saa tano kasoro. Ukweli kilichoendelea sina haja kuelelezea, kila mtu anajua.
Baada ya show, mida ya saa saba nikamsihi alale, akasema siku nyingine leo nimsindikize tu. Basi nikaamka nikamsindikiza hadi karibu na kwake. Sio mbali sana, just approximately 5 minutes walk. Nikarudi kwangu, nakuta texts nyingi za sifa. Akaniambia notion kuhusu obsession ya wanawake wa Kenya kuhusu wanaume wa kitanzania, huku akikiri kuthibitisha hilo. Nikapokea maua yangu nikalala.
Asubuhi naamshwa na meseji yake. Ni kama tayari alikua manzi yangu sasa. Nikajisemea moyoni kama wote ni hivi si ntafia huku mimi? Nikajichekea nikaamka kujiandaa na ratiba ya siku. Hakukua na masomo kwa sababu ilikua Jumamosi. Mida ya saa tano asubuhi akaniuliza kama nipo, nikamwambia nipo library chuo, kuna assignment namalizia. Akasema nikirudi nimjuze na nisile popote, amepika.
Saa sita mchana nikarudi, hata sikumaliza assignment, nikajisemea kesho pia ni siku. Nikamwambia aje, nusu saa huyu hapa na container za chakula. Tukala hapo, tukashiba. Ugonjwa wake ni ule ule, movies. Uzuri nilikua naangalia sana movies nilipomaliza form six. Nilikua na almost 500 GB HDD imejaa movies na series tu, hapo acha zilizoko kwenye laptop.
Ukweli hata movie haikumaliza opening credits (yale majina ya mwanzo kabisa movie inapoanza kama Directors, Producers, Starring etc.) tulikua tayari mbingu ya saba. Movie inaendelea huku, na sisi tunaendelea na yetu. Piga show nyingine ya kibabe mno mchana huu. Tukalala hadi jioni kabisa mida ya saa 12. Tukaamka akaenda kuoga, kajiandaa akarudi kwake.
Mi nikabaki zangu naangalia movie. Mida ya saa tatu, nashangaa mlango unagongwa. Nikasita kufungua, maana sikua nategemea mgeni yoyote usiku ule. Ukaendelea kugongwa tena. Nikasimama kufungua, ile nimefungua tu, nikapokelewa na bonge moja la kibao. Nikakaa kwenye kiti nikiwa na wenge.
Wakaingia jamaa wawili, mmoja kapanda hewani mwingine saizi yangu japo ana mwili kuniliko. Kabla sijaongea chochote wakanikalisha chini kwa nguvu, sijakaa sawa nikapigwa teke la mbavu. Hapo sasa uzalendo ukanishinda, nikataka nianze kupiga kelele kwa sababu ukweli nilikua nimezidiwa.
Kabla sijafanya chochote, wakaniuliza swali moja tu na hapo nikajua nilipoyatimba.
"We ulicome Kenya kut*mba madem zetu ama kusoma msee?"
Nikakumbuka huyu ni yule jamaa nilimuona na Jessy kule dining hall wiki iliyopita. Akaniuliza tena na kibao juu, "Unajua Jessy ni dem yangu?" Kabla sijajibu mwenzake ngumi ya kichwa, huku anamshauri wakanireport kwa Dean of students nifunzwe adabu. Mwenzake anamwambia "wacha kwanza sisi tufunze adabu ghasia hii".
Wadau, nilichezea kichapo sio cha nchi hii, literally [emoji23]. Baada ya yote wakachukua simu yangu wakaniambia nitoe nywila (password), kinyonge nikatoa. Wakapitia meseji zote nilizochati na mrembo. Makosa. Wakafuta kila kitu hadi number ya Jessy, wakanionya siku wakasikia tena nimetoka naye, itakua mwisho wangu. Wakaondoka.
Aaaaaah nikapumua pumzi ndefu sana!. A sigh of relief. Nikakaa pale chini karibu nusu saa, natafakari. Wiki ya tatu tu hapa, nimeshaanza kutoka ngeu ntatoboa miaka minne kweli? Sikutaka hata kutoka nje, nikazima taa, simu, laptop yaani kila kitu nikajifunika. Nikajaribu kulala.
Sikulala usiku kucha, wasiwasi, nipo nchi ya watu, jamaa wanajua hadi kwangu, wakija usiku wa manane wanivunjie mlango wanipige beto?
Nikaamka mapema sana Jumapili, nikajiangalia kwenye kioo, sikuwa nimevimba sana, na uzuri nilikua na miwani na kofia. Nikatoka huyo mpaka chuo, nikakaa library hadi saa nne. Simu bado iko off. Nikaiwasha, meseji ya kwanza "Good morning babe", nilichoka mwili, nafsi na roho kwa sababu zilikuwa number za Jessy. Kumbe jamaa walifuta tu hawakublock.
Sijakaa sawa, simu yake inaingia. Nikajishauri, nipokee au nisipokee. Nikapiga moyo konde, nikapokea. Akawa anashangaa mbona sikua hewani tokea jana usiku hadi asubuhi ile.
Nikafunguka kila kitu kilichotokea usiku wa kuamkia siku hiyo baada ya yeye kuondoka.
Ukweli kabisa, yule binti alikasirika na kuhuzunika mno. Akaniambia tukutane nje ya geti la chuo tuka-report polisi yule jamaa akamatwe. Sikutilia maanani ushauri wake kwa sababu sikutaka mambo yawe mengi, mtu niko nchi ya watu huko nianze kusumbuana na polisi. Nikapotezea. Ila nikamwambia sikuwa tayari kuendelea naye tena.
Bado story ni ndefu ila nimechoka kuandika leo. Ngoja nivute pumzi.