Baba Kisarii
JF-Expert Member
- May 7, 2024
- 1,844
- 3,089
- Thread starter
- #241
Sababu?Sijawahi
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Sababu?Sijawahi
Kuna tukio moja lilitokea kituo cha polisi kesi ya wanandoa mume kampiga mke, mke kakimbilia polisi mume nae hakuchukua muda akamfuata nyuma. Kufika kituoni anaona mkewe anatoka chooni na afande, afande akatimua mbio.ukute afande alivyokuweka nguvuni akaenda kulala kwako halafu asubuh ukampongeza na lififte
Kama katosheka na kodi atamchukua, hamkuwa na watoto?Baba mwenye nyumba amchukue tu huyo mshenzi.
Endelea mkuu😂Mimi kuna mmoja aliwahi nipeleke, nikaitwa dawati la jinsia, nikaenda.
Wakaanza ngonjera na vitisho kuwa nimempiga. Nikawaambia aeleze vizuri kosa ni lipi, aksema hakuwapikia watoto alikuwa anajisikia vibaya. Akaulizwa kama alitoa taarifa kwangu, akakataa.
Kimwanamke kimoja kikaanza, hata kama hakupikia watoto, huna haki ya kumpiga. Nikamuuliza unao ushahidi kama nimempiga, akasema mimi nimepokea malalamiko, nina uwezo wa kukuweka lockup. Nikamwambia, majadilianao yameishia hapa, nipelekeni mahakamani.
Basi wakachachamaa kuwa nina kiburi, watamsaidia mke wangu na watanipa fundisho, nikasema nasubiri. Kimbembe ikawa mke wangu hataki niwekwe lockup. Maana anajua jinsi nilivyokuwa na react sikuwa natania, ndoa ingeisha. Wakamwambia aandike maelezo, mimi nawekwa lockup then mahakamani. Wife akawajibu sina ushahidi mahakamani, na sitaki awekwe lockup maana hana kosa. 😂
Kilichoendelea ni yeye kukoswa kofi na kidada kimoja, eti unatusumbua. Kidogo akaja OCD akasikiliza marumbano, akawambia msizunje ndoa za watu, huyu dada anampenda mmewe, waacheni huru.
Kurudi home hana hata nauli, anatembea kwa miguu. Nikampa nauli ya daladala, nikapanda boda boda nikaondoka. Home nikawachukua watoto nikaondoka nao kwenda matembezi bila kumpa taarifa. Jioni hatukurudi, 😂😂 ngoja niishie hapa story ndefu na inachekesha mwishoni.
Huu uzi haujaniacha bure, kwa hizi experience kwa hakika kuna vitu najifunza. Pole mkuu kwa uliyopitia.Mimi nilimchapa vibao mke wangu akiwa mjamzito kisa kunitukania mama yangu. Akaenda Polisi, wakanipigia simu, nikachukua zangu karatasi tatu na kalamu nikaandika taraka kabla sijafika kituoni. Nikabeba simu, hela kama fifte zile karatasi.
Kituoni nafika, nimesimama mbele ya meza, naulizwa wewe ndio flani, wewe unamjua huyu, sijajibu zunguka huku, kofi la mhongo, vua mkanda, kiatu, saa wakanitupa sero, nikakabidhi hela, simu na zile karatasi kwenye bahasha.
Mwanamke wakamwambia rudi nyumbani ilikuwa jioni mida ya saa 10 hivi.
Mida ya saa 12 jioni naitwa sero, kumbe mke wangu amekuja kuniletea chakula na amenisamehe eti niachiliwe kimemuuma.
Afande wa zamu akasema, mpaka aje afande alienipigia simu. Ex Wife akawaambia yameshaisha, waniachie. Wakamwambia wewe umeleta mambo polisi kuna utaratibu wake, ungekuwa unataka msamehe huyu bwana usingekuja huku. Huyu atalala ndani mpaka akamilishe dhamana. Wakanitupia tena sero, nikakataa kula nikamwambia Afande hicho chakula arudi nacho huyo mwanamke.
Yule mama akalia sana pale nje, wakamfukuza wakamwambia aje asubuhi. Mtoto wangu wa miaka miwili namsikia analia baba, baba, mi nipo sero.
Kukakucha, Akawahi sana yule mama saa 12, kaleta chai. Polisi wana utaratibu wao, wakachomoa watu wa kwenda mahakamani, badae saa mbili mbili mlango unafunguliwa naitwa mimi, nafika CRO chumba cha mashitaka nawakuta jamaa, washikaji, mshua na wafanyakazi wangu wamekuja kunichomoa.
Basi tukaitwa ofisini kwa mkuu wa kituo, Afande mmoja Mwanamke ndie akasikiliza ishu yetu. Nikaonywa sana kupiga mke, kwamba ni jinai na ile ishu ningefungwa kwa kujeruhi, mambo mengi niliambiwa pale kibabe sana na yule Maza afande.
Wakanirudisha chumba cha Mashitaka, chukua vitu vyako, anataka kunikabidhi zile karatasi nikamwambia mpe huyu ndio zake anafungua kusoma ni taraka, kilio kikubwa mno na kugalagala chini. Polisi wakamwambia kama amekupa taraka nenda mahakamani ili ukapate haki zako.
Wana wakanichukua, wakanipeleka gesti, nikaoga kutoa nuksi nikaletewa nguo zingine nikavaa.
Yule mama akanipeleka mahakamani, na mimi sikurudi home, napigiwa simu na Mwenyekiti kuna samansi ya mahakamani.
Nikaenda mahakamani nikakiri kumpa taraka yule mama, wakaainisha vitu vya ndoa. Nyumba ya ndoa na viwanja viwili. Mimi nikawaambia nyumba ya ndoa ibaki ya watoto, viwanja viwili nampa moja chake moja changu. Nilikuwa na pesa akiba kama 1.5 M nikawambia mahakama nampa laki 7 na vyombo vyote vya ndani aondoke navyo.
Nyumba ikapangishwa, pesa ya mtoto mdogo nikaambiwa nitalipa hamsini kila mwezi. Mtoto mkubwa akabaki shule. Kwisha.
Mali zote nilikuwa naandikisha kampuni ambayo aliikuta yule mama. Nikaokoa mali kibao kupigwa pasu. Gari, trekta, vyote alidai mahakamani vikaonekana ni vya kampuni ambayo kaikuta na nipo mimi, mzee na mdogo wangu hiyo ilikuwa 2019. Mwanamke alikomaa sana kila kitu kiuzwe, kumbe mimi nilikuwa nafanya biashara chini ya Kampuni. Mali zangu ukinitafuta mimi hunikuti unaikuta kampuni. Tukavutana sana mahakamani, ikaonekana nimemuoa kampuni kaikuta na hajawahi kuingizwa kwenye kampuni kwa hisa au kwa kufanya kazi. Ana kazi yake nina biashara zangu. Pia nilipeleka Usia na mirathi ya mama yangu ambae katika mgao wa mirathi ya mama ndipo tulikubaliana mimi, baba na wadogo zangu tufungue kampuni na yeye nikamuoa miaka 10 baadae.
Nikaokoa mali mzee, vinginevyo ilikuwa ni pasu kwa pasu. Chezea mwanamke akiwa mjinga ila akiwa anajitambua ni hatari sana mbele ya sheria jameni. Mwanamke aliweka mpaka wakili kutaka mali zile.
Pole sana Mzee mwenzangu. Mke mbele ya sheria achukuliwi kama mke wako anachukuliwa kama "Separate entity" yaani anakufunga laivu laivu. 😁
Ukipigwa na mmeo kituo cha kwanza ni polisi?.My apologies to him, kumbe hakuwa amempiga mkewe, ila mkewe alikimbilia polisi labda baada ya kugombezwa on why hajawapikia watoto.
Mwanzo nilidhani amepelekwa polisi kwasababu kamkung'uta mkewe na ameenda kuwavimbia makanjo.
majamaa huwaga ni wakwale balaa kwa loose balls ni mashambuliaji hatari hahshKuna tukio moja lilitokea kituo cha polisi kesi ya wanandoa mume kampiga mke, mke kakimbilia polisi mume nae hakuchukua muda akamfuata nyuma. Kufika kituoni anaona mkewe anatoka chooni na afande, afande akatimua mbio.
We ulisikia wapiNiliwekwa ndani na mke wangu baada ya mimi kugoma kutoa mchango wa kumdhamini kaka yake aliyekamatwa na pembe za ndovu.
Zilitakiwa milioni 5 kumdhamini kaka wa mke wangu, ndugu zake walijikusanya wakachanga milioni 3. Zile mbili zilizopungua mke wangu alikuja kuniomba nitoe hizo hela ili kukamilisha malipo ya dhamana.
Sikuwa na hiyo hela, nilimwambia wazi kuwa sina hela. Kilichotokea sasa baada ya kumwambia hivyo alinifokea kwa ukali akinituhumu kuwa nina roho mbaya na sipendi kusaidia ndugu zake Ila naweza kuhonga malaya tu huko mitaani.
Sikufurahishwa na hayo aliyoniambia so nilimfata na kumcharaza kwa vibao vitatu vya shavu ili kumshikisha adabu. Alipiga yowe la uchungu na kutoka baru akatokomea sijui wapi huko.
Baada ya kama lisaa limoja hivi nilipigiwa simu na mtu aliyejitambulisha kuwa ni polisi akinitaka nifike kituoni, nilishangaa Ila niliitikia wito.
Nilipofika kituoni mshangao wangu ukawa mkubwa zaidi baada ya kumkuta mke wangu yupo hapo na alifika hapo kuripoti kuwa nimemshambulia kwa kukusudia. Nilishindwa kujitetea maana ni kweli nilimpa Kichapo.
Afande aliyeshughurikia hayo malalamiko ya mke wangu alisema hawezi kulimaliza hilo suala muda huo maana ilikuwa ni saa mbili usiku, atalishughulikia kesho yake asubuhi. Afande alimtaka mke wangu arudi nyumbani Ila mimi sikuruhusiwa kurudi nyumbani bali nilitakiwa kulala hapo kituoni.
Muda mfupi baada ya mke wangu kuondoka niliamriwa na afande wa zamu kuvua viatu na mkanda wa suruali kisha nikasukumwa kwenye kachumba kasiko na dirisha wala taa nikawa nimelala polisi kwa mara ya kwanza.
Nililala kwa usiku mmoja tu, asubuhi tuliyamaliza mambo ya kipolisi kishikaji nikaachiwa huru asubuhi hiyo.
Nikiwa na hasira kali sikurudi home niliamua tu kuachana na huyo mwanamke wa kinyiramba.
Tuliowahi kulazwa polisi na wake zetu tujuane hapa.
Huu uzi haujaniacha bure, kwa hizi experience kwa hakika kuna vitu najifunza. Pole mkuu kwa uliyopitia.
Ni hatari sanamajamaa huwaga ni wakwale balaa kwa loose balls ni mashambuliaji hatari hahsh
Kama mambo ndio hayo endelea tu kusikilizia mkuu. Ila wanawake akili zao wanazijua wenyewe.Nimepoa na sijaoa tena mzee. Nasikilizia kwanza.
Hivi dhamana ya pesa taslimu huwa inarudi punde mtuhumiwa akiaachiwa
Wewe tena cheupe cheupe😂Somehow the end is funny 😂😂😂
Ila tunawapenda hivyo hivyo tu. 😁Na kweli tuna viherehere sana.
Post ya 128 mkuu.Endelea mkuu😂
Sahihi kabisa...tamaa ya afande kupata 50k ...ilivunja hii ndoa....haya mambo yanahitaji busara na hekimaHata hao polisi waliokuweka ndani nao ni wajinga. Ingekuwa Ulaya ningeelewa, ila Bongo kitendo cha namna hii kinaweza kusababisha ndoa kuvunjika haraka sana.
Sasa ulinunua bastola ya nini? Na kama aihusiki na swala la kumtreat mkeo haikuwa na haja ya kutuambia umenunua hiko chuma.Kwanza kabisa hakunaga mwanadamu mwenye uzoefu wa ndoa humu dunian wazee hilo msijidanganye. Watu wana uzoefu wa wanawake sio ndoa. Kuna mwanamke ukiwekwa nae chumba kimoja utavunja ukuta. Na Kwasababu kila mtu ana mke wake na Style yake ya kuishi nae pia. Ukipewa mke wa huyu hata kama umeishi na mkeo miaka 40 utaweza kukimbia vivyo hivyo na wewe mkeo ni wewe unaweza kuishi nae na kuna watu kuna wazee na ukongwe wao wanakuonea huruma. Mimi nilivyooa tu nikanunua bastola. Miaka kadhaa mbele akazingua nikapotea home wiki tatu hawakujua nilipo nilizima CM zote. Tangu cku hizo na leo kukwaruzana. Maana nilimwambia mbele ya mama yake, Cku ukizingua tena hata maiti yangu hutaiona. Ila cjawah kumpiga wala kumtukana. Mi ukiongea sana nateleza tu kama kitimoto narudi ukiwa umelala na naondoka ukiwa umelala.
Eeh mnyiramba. Sasa makabila mengine hawa kutaki mnyirambaKwa hiyo ukiniita mnyiramba ndiyo muda huohuo nakuwa mnyiramba?Sasa inabidi niachane na kabila langu na nimebadili kabila kuanzia sasa!Happy now?