[emoji28][emoji28]jamaa kaonyesha tabia za kirembo sana..una zira mbele ya mama mkweSasa ulinunua bastola ya nini? Na kama aihusiki na swala la kumtreat mkeo haikuwa na haja ya kutuambia umenunua hiko chuma.
Hawa ndo wanajiuaga wenyewe hawa! Nikimbie familia kisa mwanamke??? Hovyo kabisa we mjuba[emoji28][emoji28]jamaa kaonyesha tabia za kirembo sana..una zira mbele ya mama mkwe
Mkuu hapa Uliover react kwa kweli unless kuna mengine alikuwa anafanya ukaona hapo ndo pa kumalizia mchezo.....Mimi nilimchapa vibao mke wangu akiwa mjamzito kisa kunitukania mama yangu. Akaenda Polisi, wakanipigia simu, nikachukua zangu karatasi tatu na kalamu nikaandika taraka kabla sijafika kituoni. Nikabeba simu, hela kama fifte zile karatasi.
Kituoni nafika, nimesimama mbele ya meza, naulizwa wewe ndio flani, wewe unamjua huyu, sijajibu zunguka huku, kofi la mhongo, vua mkanda, kiatu, saa wakanitupa sero, nikakabidhi hela, simu na zile karatasi kwenye bahasha.
Mwanamke wakamwambia rudi nyumbani ilikuwa jioni mida ya saa 10 hivi.
Mida ya saa 12 jioni naitwa sero, kumbe mke wangu amekuja kuniletea chakula na amenisamehe eti niachiliwe kimemuuma.
Afande wa zamu akasema, mpaka aje afande alienipigia simu. Ex Wife akawaambia yameshaisha, waniachie. Wakamwambia wewe umeleta mambo polisi kuna utaratibu wake, ungekuwa unataka msamehe huyu bwana usingekuja huku. Huyu atalala ndani mpaka akamilishe dhamana. Wakanitupia tena sero, nikakataa kula nikamwambia Afande hicho chakula arudi nacho huyo mwanamke.
Yule mama akalia sana pale nje, wakamfukuza wakamwambia aje asubuhi. Mtoto wangu wa miaka miwili namsikia analia baba, baba, mi nipo sero.
Kukakucha, Akawahi sana yule mama saa 12, kaleta chai. Polisi wana utaratibu wao, wakachomoa watu wa kwenda mahakamani, badae saa mbili mbili mlango unafunguliwa naitwa mimi, nafika CRO chumba cha mashitaka nawakuta jamaa, washikaji, mshua na wafanyakazi wangu wamekuja kunichomoa.
Basi tukaitwa ofisini kwa mkuu wa kituo, Afande mmoja Mwanamke ndie akasikiliza ishu yetu. Nikaonywa sana kupiga mke, kwamba ni jinai na ile ishu ningefungwa kwa kujeruhi, mambo mengi niliambiwa pale kibabe sana na yule Maza afande.
Wakanirudisha chumba cha Mashitaka, chukua vitu vyako, anataka kunikabidhi zile karatasi nikamwambia mpe huyu ndio zake anafungua kusoma ni taraka, kilio kikubwa mno na kugalagala chini. Polisi wakamwambia kama amekupa taraka nenda mahakamani ili ukapate haki zako.
Wana wakanichukua, wakanipeleka gesti, nikaoga kutoa nuksi nikaletewa nguo zingine nikavaa.
Yule mama akanipeleka mahakamani, na mimi sikurudi home, napigiwa simu na Mwenyekiti kuna samansi ya mahakamani.
Nikaenda mahakamani nikakiri kumpa taraka yule mama, wakaainisha vitu vya ndoa. Nyumba ya ndoa na viwanja viwili. Mimi nikawaambia nyumba ya ndoa ibaki ya watoto, viwanja viwili nampa moja chake moja changu. Nilikuwa na pesa akiba kama 1.5 M nikawambia mahakama nampa laki 7 na vyombo vyote vya ndani aondoke navyo.
Nyumba ikapangishwa, pesa ya mtoto mdogo nikaambiwa nitalipa hamsini kila mwezi. Mtoto mkubwa akabaki shule. Kwisha.
Mali zote nilikuwa naandikisha kampuni ambayo aliikuta yule mama. Nikaokoa mali kibao kupigwa pasu. Gari, trekta, vyote alidai mahakamani vikaonekana ni vya kampuni ambayo kaikuta na nipo mimi, mzee na mdogo wangu hiyo ilikuwa 2019. Mwanamke alikomaa sana kila kitu kiuzwe, kumbe mimi nilikuwa nafanya biashara chini ya Kampuni. Mali zangu ukinitafuta mimi hunikuti unaikuta kampuni. Tukavutana sana mahakamani, ikaonekana nimemuoa kampuni kaikuta na hajawahi kuingizwa kwenye kampuni kwa hisa au kwa kufanya kazi. Ana kazi yake nina biashara zangu. Pia nilipeleka Usia na mirathi ya mama yangu ambae katika mgao wa mirathi ya mama ndipo tulikubaliana mimi, baba na wadogo zangu tufungue kampuni na yeye nikamuoa miaka 10 baadae.
Nikaokoa mali mzee, vinginevyo ilikuwa ni pasu kwa pasu. Chezea mwanamke akiwa mjinga ila akiwa anajitambua ni hatari sana mbele ya sheria jameni. Mwanamke aliweka mpaka wakili kutaka mali zile.
Pole sana Mzee mwenzangu. Mke mbele ya sheria achukuliwi kama mke wako anachukuliwa kama "Separate entity" yaani anakufunga laivu laivu. 😁
Sawa.Unaruhusiwa kuolewa na wanaume wa ulaya Lakin.
Sasa hapo kwa tabia ya kupiga mke selo itakuwa ndio bedroom yako!Dawa ni kuoa polisi mwenye cheo.
Namnyemelea Suzan Kaganda, akijaaa naoa kabisa
Kwani kumpenda mtu na kusema hadharani ni kosa kisheria?Unaye "Kibatala" wa kukutetea? Ni hatari sana kuwataja wakuu hao kwa majina yao kabisa.
Hili huwa halifanyi kazi kwetu watanzania, nyie wakenge ndio mnaweza sababu wake zenu ndio waume zenu. Wanawafumua haswaaSio poa kumpiga mkeo, hamna kisichozungumzika, utajikuta unapiga kila mwanamke usiyeendana naye.
Angalau hata kuna wanaume mko positive.Uliyekuwa ukimuita mkeo awe na chuki binafsi na wewe?
-Ulifanya kosa kisheria kumpiga.
-ulimpiga baada ya kuwa na hasira.
-mngeachwa mrudi wote nyumbani lazima/kuna uwezekano ungemkoyonga tena ndiyo mkatenganishwa.
NB;Kutupwa selo ilikuwa ni njia bora ya kuwatuliza wote wawili hasira ziwatoke akilini na mtafakari upya mambo yenu.Halafu,hukutaka kukubali moyoni mwako kwamba ulikosea kupiga. Na mwishowe ukaikimbia nyumba na kumtwisha lawama mtu unayemwita "mnyiramba" badala ya kulijutia kosa lako.Hadi mke anang'ang'ania umpe hela ambazo kiuhalisia yawezekana haukuwa nazo umeonesha huna uwezo wa kujieleza,kumshawishi mtu akuamini na kusuluhisha mambo kwa amani.
Mdogo wangu wamama watakuua.Mashangazi sometimes wanazingua...
Wanajua watu tuna njaa njaa za kingese sijui [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Nika quit mapema kabisa sinaga mambo mengi [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Mkuu hapa Uliover react kwa kweli unless kuna mengine alikuwa anafanya ukaona hapo ndo pa kumalizia mchezo.....
Hilo ni swali au ni mkazio?We ulisikia wapi
Nilimwachia hata hako ka baby girl, sihitaji kuunganishwa kwa lolote na huyo mshenzi.hamkuwa na watoto?
Hakuna shida ikiwa afande alikwenda kumwonesha choo tu 😂Kufika kituoni anaona mkewe anatoka chooni na afande, afande akatimua mbio.
Jamaa ni fix huyu. Yuko kwa Mtogole anauza mnazi.Sasa ulinunua bastola ya nini? Na kama aihusiki na swala la kumtreat mkeo haikuwa na haja ya kutuambia umenunua hiko chuma.
Nitakupata tu, ngoja nikipata muda 😀Wewe tena cheupe cheupe😂
Sawa cheupe, ulinifanya nikafanye ujasusi wangu maana nilihisi ni wewe umenshtukia. Ila kumbe badoo niko salama. 😁
Mke wako hana makosa, mwenye makosa ni wewe. Unaonyesha dalili za wazi kabisa kuwa alikuwa ameshajenga tabia ya kukufokea na alikuwa amesahakudharau; mwanamake hawezi akaibuka tu from nowhere kuanza kumfokea mume wake. Pengine hata hakuwa na kisirani cha kufikia kiwango hicho, ila wewe ndiyo ulikuwa umemlea na kumsababisha akajangea taba hiyoNiliwekwa ndani na mke wangu baada ya mimi kugoma kutoa mchango wa kumdhamini kaka yake aliyekamatwa na pembe za ndovu.
Zilitakiwa milioni 5 kumdhamini kaka wa mke wangu, ndugu zake walijikusanya wakachanga milioni 3. Zile mbili zilizopungua mke wangu alikuja kuniomba nitoe hizo hela ili kukamilisha malipo ya dhamana.
Sikuwa na hiyo hela, nilimwambia wazi kuwa sina hela. Kilichotokea sasa baada ya kumwambia hivyo alinifokea kwa ukali akinituhumu kuwa nina roho mbaya na sipendi kusaidia ndugu zake Ila naweza kuhonga malaya tu huko mitaani.
Sikufurahishwa na hayo aliyoniambia so nilimfata na kumcharaza kwa vibao vitatu vya shavu ili kumshikisha adabu. Alipiga yowe la uchungu na kutoka baru akatokomea sijui wapi huko.
Baada ya kama lisaa limoja hivi nilipigiwa simu na mtu aliyejitambulisha kuwa ni polisi akinitaka nifike kituoni, nilishangaa Ila niliitikia wito.
Nilipofika kituoni mshangao wangu ukawa mkubwa zaidi baada ya kumkuta mke wangu yupo hapo na alifika hapo kuripoti kuwa nimemshambulia kwa kukusudia. Nilishindwa kujitetea maana ni kweli nilimpa Kichapo.
Afande aliyeshughurikia hayo malalamiko ya mke wangu alisema hawezi kulimaliza hilo suala muda huo maana ilikuwa ni saa mbili usiku, atalishughulikia kesho yake asubuhi. Afande alimtaka mke wangu arudi nyumbani Ila mimi sikuruhusiwa kurudi nyumbani bali nilitakiwa kulala hapo kituoni.
Muda mfupi baada ya mke wangu kuondoka niliamriwa na afande wa zamu kuvua viatu na mkanda wa suruali kisha nikasukumwa kwenye kachumba kasiko na dirisha wala taa nikawa nimelala polisi kwa mara ya kwanza.
Nililala kwa usiku mmoja tu, asubuhi tuliyamaliza mambo ya kipolisi kishikaji nikaachiwa huru asubuhi hiyo.
Nikiwa na hasira kali sikurudi home niliamua tu kuachana na huyo mwanamke wa kinyiramba.
Tuliowahi kulazwa polisi na wake zetu tujuane hapa.
Ndoto ya mchana😅Nitakupata tu, ngoja nikipata muda 😀
Si mleta mada kasema hivyo, kuwa ugombi na mke wake ni kiasi cha pesa kilipelea cha kuweka dhamana kama milion 2 hivi ndiyo mimi kuuliza swali sasa [emoji1787]Dhamana na pesa taslimu walikuchaji wapi polisi au mahakamani?
Hakuna dhamana ya fedha taslimu polisi, ni mdhamini, barua ya mtendaji/mwenyekiti wa mtaa au Kitongoji na kitambulisho cha Mdhamini kusaini fomu.
Mahakamani ndio huwa dhamana inakadiriwa na just in case Mtuhumiwa akitoroka ndio utalipa kama ni madai au kifungo.