Ulishawahi kulazwa kituo cha polisi na mkeo?

Ulishawahi kulazwa kituo cha polisi na mkeo?

Nilimwachia hata hako ka baby girl, sihitaji kuunganishwa kwa lolote na huyo mshenzi.
This is very sad.

Hicho kimalaika cha Mungu kina makosa gani? Hata kama mamake ni mshenzi huwa tunachukua damu yetu na kuilea. Hicho kibinti kichukue ukilee mkuu. Utakuja kunishukuru sana huko mbele ya safari!
 
Uliyekuwa ukimuita mkeo awe na chuki binafsi na wewe?
-Ulifanya kosa kisheria kumpiga.
-ulimpiga baada ya kuwa na hasira.
-mngeachwa mrudi wote nyumbani lazima/kuna uwezekano ungemkoyonga tena ndiyo mkatenganishwa.
NB;Kutupwa selo ilikuwa ni njia bora ya kuwatuliza wote wawili hasira ziwatoke akilini na mtafakari upya mambo yenu.Halafu,hukutaka kukubali moyoni mwako kwamba ulikosea kupiga. Na mwishowe ukaikimbia nyumba na kumtwisha lawama mtu unayemwita "mnyiramba" badala ya kulijutia kosa lako.Hadi mke anang'ang'ania umpe hela ambazo kiuhalisia yawezekana haukuwa nazo umeonesha huna uwezo wa kujieleza,kumshawishi mtu akuamini na kusuluhisha mambo kwa amani.
We mpuuzi
 
Mtu yeyote atakayenipeleka polisi na kuniweka ndani basi lazima awe adui yangu wa kudumu. Sina mshamaha na yeyote anayehusisha polisi tukikosana.
 
Kawaida mbona,wanaume kuwekwa rumande na wake zao
Hiyo ndoa itaishia hapo..!! Ingawa inategemea na sababu..!! Yaani kaka yake ajihusishe na nyara za taifa halafu mimi nikamdhamini..!! Angetusua ningehusishwa? Mbaya zaidi jamaa alikuwa hana hela.SI kwamba anazo zimekaa tu sehemu..!!
 
Niliwekwa ndani na mke wangu baada ya mimi kugoma kutoa mchango wa kumdhamini kaka yake aliyekamatwa na pembe za ndovu.

Zilitakiwa milioni 5 kumdhamini kaka wa mke wangu, ndugu zake walijikusanya wakachanga milioni 3. Zile mbili zilizopungua mke wangu alikuja kuniomba nitoe hizo hela ili kukamilisha malipo ya dhamana.

Sikuwa na hiyo hela, nilimwambia wazi kuwa sina hela. Kilichotokea sasa baada ya kumwambia hivyo alinifokea kwa ukali akinituhumu kuwa nina roho mbaya na sipendi kusaidia ndugu zake Ila naweza kuhonga malaya tu huko mitaani.

Sikufurahishwa na hayo aliyoniambia so nilimfata na kumcharaza kwa vibao vitatu vya shavu ili kumshikisha adabu. Alipiga yowe la uchungu na kutoka baru akatokomea sijui wapi huko.

Baada ya kama lisaa limoja hivi nilipigiwa simu na mtu aliyejitambulisha kuwa ni polisi akinitaka nifike kituoni, nilishangaa Ila niliitikia wito.

Nilipofika kituoni mshangao wangu ukawa mkubwa zaidi baada ya kumkuta mke wangu yupo hapo na alifika hapo kuripoti kuwa nimemshambulia kwa kukusudia. Nilishindwa kujitetea maana ni kweli nilimpa Kichapo.

Afande aliyeshughurikia hayo malalamiko ya mke wangu alisema hawezi kulimaliza hilo suala muda huo maana ilikuwa ni saa mbili usiku, atalishughulikia kesho yake asubuhi. Afande alimtaka mke wangu arudi nyumbani Ila mimi sikuruhusiwa kurudi nyumbani bali nilitakiwa kulala hapo kituoni.

Muda mfupi baada ya mke wangu kuondoka niliamriwa na afande wa zamu kuvua viatu na mkanda wa suruali kisha nikasukumwa kwenye kachumba kasiko na dirisha wala taa nikawa nimelala polisi kwa mara ya kwanza.

Nililala kwa usiku mmoja tu, asubuhi tuliyamaliza mambo ya kipolisi kishikaji nikaachiwa huru asubuhi hiyo.

Nikiwa na hasira kali sikurudi home niliamua tu kuachana na huyo mwanamke wa kinyiramba.

Tuliowahi kulazwa polisi na wake zetu tujuane hapa.
Kwanini uliwekewa mtego na wewe ukajaa ,ungetumia akili kuuchenga mtego wake..
 
Back
Top Bottom