Ulishawahi kumchukia member wa JF pasipo kumjua

Kuna mtu alishasema ukitaka kumpata mwanamke aliyefunga pm humu gombana naye kisha atakuja pm kuomba msamaha.. akishakuja unaanzia hapo hapo.

Like nimekupa bwana shemeji. Nitakunyimaje wakati unataka ziwe nyingi uwe maarufu kama naniii
Embe tugombane basi na mimi. [emoji16][emoji16][emoji16]
 
Sijawahi na siwezi ila nimewahi kuchukia baadhi ya kauli zao (nachukia kauli si mtoa kauli) iwe inanilenga Mimi au hata members wengine, kuna watu wanakauli chafu sana hawawezi eleze mawazo yao kwa ustaarabu
Hapo ndio ujue kwamba binadam tupo tofauti sana, unachowaza wewe sicho anachowaza yeye,na sicho anachowaza mtu mwingine inabidi tuvumiliane tuu hakuna namna.
 
Kuchukia hapana ila inafika mahali ukiona the way mtu anatoa comment juu ya topic inayojadiliwa, unashindwa kuelewa anamatatizo gani kwenye ufahamu wake.
Wengine bangi, si unajua Bangi,za kuvutia chumbani zinawachanganya mno
 
Tuache unafiki kila mtu ana namna yake ya kumchukia mtu hata kama humjui..

Mfano: Huwa nachukia mtu wale wanaojiona ni manguli wa jukwaa fulani, na hao wanapatikana sana sana MMU, unakuta mtu kaanzisha uzi wake wa kuomba ushauri au msaada wa jambo fulani, mwisho wa siku wanatoke wale vihere here wanakuja kupindua mada husika na kuleta stori zao binafsi za kipuuzi ambazo kiuhalisia halikuwa dhumuni la mada husika..

Kiujumla wanawakwaza na kuwakasirisha watu kwa tabia zao za kilimbukeni.
 

Mkuu kwenye hii thread hutakiwi kusema ukweli, jibu ni moja kwamba huchukii mtu sawa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…