Hilo limewahi kuwa pigo takatifu kwangu.
Kuna hiyo demu yangu nilikuwa nayo niliipataga Kwa tabu sana.Yaani mpaka kuipata mpaka nilienda kujitambulisha kanisani kwao.
Sasa penzi lilikuwa Moto Moto yaani full malavidavi, akija geto,anapika,anafua,anadeki, anaongea vizuri na majirani, kama sipo anahuzuria kwenye matatizo ya Nzengo, yaani ana namba ya mwenyekiti wa mtaa mpaka wa jumuiya.
Basi bwana pale Upangajini wakawa wanamuita Mama junior (Kwa jina langu.)
Siku zilisonga rasmi nikatambulishwa kwao na binti.Binafsi azma ya Moyo wangu ilikuwa tamaa tu kwake lakini mpaka kufikia hapo nikahamishia mahaba yote kwake.
Siku Moja akaja na rafiki Ake gheto, akanitambulisha kwake nami nikajitambulisha kwake.
Twende kwenye pigo takatifu Moja Kwa Moja. Huyu rafiki Ake alinisumbua Sana. Mara shemeji nisadie hela ya pedi,mara Hana nauli,mara hiki mara kile,Nika nampa kiroho Safi tu.
Nilipo ona amezidi kuwa omba omba Sana Nika mshirikisha My wife to be.
Hakuonesha kujali zaidi nikasomewa kifungu kwenye kitabu kitakatifu.
Rafiki mtu akaanza kuja gheto Pekee ake nakumbuka siku ya tukio alikuja ,akachukua ndoo bafuni anabadili nguo mbele yangu ( Maisha ya chumba kimoja na sebule) alikuwa haingii chumbani kwetu, sijui nilipatwa na mdudu gani maana hapa shettani Nita msingizia tu.
Aisee ilipigwa shoo pale sebuleni Acha kabisaa. Tulishituka tu My wife to be anagonga mlango. Sa Ile kuchelewa kufungua na kukurukakara ya pale ndani. Alipo ingia alikuwa na wasi wasi na akatamka najua kila kitu lakini nime wasamehe bure.Maana vile vikaratasi vilivyo chanika chanika kwenye ndomu vipisi vidogoo vilikuwa tu hapo Chini.
Chupi na nguo za rafikiake zilikuwa zimesambaa hapo chini.
Wif2be akabeba kila kilicho chake akasepa kimya kimya. Kila nilipo mtafuta aliniambia yupo kwenye mfungo. Imepita miaka 2 nilikuja kutana naye mkoa jirani tuliongee mengi Sana.
Chaajabu huyo rafiki yake namchukia mpka Kesho. Ilinichukua muda Sana huyu manzi kunitoka akilini.
BORA UACHE NA SIYO KUACHWA.
RAFIKI WA MPENZI WAKO MWOGOPE KAMA UKOMA.
MTAKA NYINGI NA SABA HUPATA MINGI MISIBA.
Sent from my Nokia 1 using
JamiiForums mobile app