Ulishawahi kutengwa na rafiki yako wa karibu baada ya yeye kufanikiwa? Toa kisa chako ilikuwaje

Hapo kakosea sana, tena sana.

Yaani hakuwaona wote hawa mpaka kwenda kuvunja ndoa ya aliyekufadhili.

Msaada wenu umewaponza.

Poleni sana WADAU
 
Haya maisha ya wanaofanikiwa kujitenga nami yamekuwa msisha yangu kila mara. Watu wa namna hii wana tabia zinazotofautiana. Kuna waliofanikiwa na kusahau kwamba tulitaabika wote. Hata nikijaribu kuwtafuta, wanajifanya kuwa na shughuli nyingi. Wengine wanakata kabisa mawasiliano, kiasi kwamba siwezi kuwafikia. Wengine wakishindwa kunikwepa, wanazusha zengwe la kunichafua. Wengine hata kujaribu kunifanyia kitu kibaya ili kuniondoa endapo kuna kitu wanaficha ambacho nakijua. Hayo yote ni maisha. Kikubwa ni kutengeneza mwelekeo wa maisha mwenyewe bila kuwategemea. Hii imesababisha kusonga mbele bila kutetereka na kuyaona ni ya kawaida.
 
Kinachosababisha urafiki uwepo kikibadilika au kufa na urafiki unabadilika au kufa. Usisahau hiyo pointi ukiwa kwenye urafiki na yeyote.

Mkiwa hamna kazi wote, mtakuwa marafiki kwa sababu mtafanana vitu vingi, ili urafiki uendelee ni labda mbaki hamna kazi au kila mtu apate kazi na zisiwe na tofauti kubwa. Mkiwa matajiri, mbaki matajiri, mmoja akifilisika, urafiki utaishia hapo. Mkiwa wanafunzi, uanafunzi usiishe, ukiisha na urafiki unaishia hapo, labda mpate kingine kitakacho sababisha urafiki uwepo.
 
Na hii ni kwa sababu kinachowaunganisha kikibadilika au kutokuwepo, mahitaji yenu ya kisaikolojia yanabadilika. Kuna mmoja atabaki toleo la zamani lenye mahitaji ya zamani, na mwengine amekuwa mpya hivyo ana mahitaji mapya. Na kila mmoja atamuona mwenzake kituko, japo aliyeachwa nyuma kimaendeleo atahisi anaonekana kituko zaidi.
 
Mi bado muangaikaji ambae siijui kesho yangu inakucha vipi ila naamini Mungu atanionyesha mlango pia. Tusiwapuuze watu tunaokuwa nao kwenye kipindi kigumu pindi tunapofunguliwa njia za mafanikio. Japo kuna ubize lakini si mbaya tukajuliana Hali tu..
Kweli kabisa
 
Kuna mwamba A level tulikia karibu mnoo na nimempa tag sana aisee bila kujisifia, sehem alipokua anakaa jiran kuna dogo anafanya kibarua cha usafi kwenye hizi ngo's wana deal na volunteers wa nje mambo ya kijamii...bas alikuja dem mzungu pale akatokea kumzoea yule dogo mfanya usafi akawa anamtembeza maeneo mbali mbali hadi kwao ndo kukutana na mwamba huyu niliesoma nae! picha linaanza jamaa english inampa tabu kuongea na kuandika dem alivorudi U.S nikawa namuandikia mimi barua kwa maneno yangu mwenyewe nachombeza kinoma had kuna muda dem alitaka waachane kisa distance aisee nilijifanya shakespear hatari 😁 niliandika batua za kum please sana yule bambadi... doooh jamaa kuja kupata invitation ya kwenda mbele picha linaanza wakaandaa sherehe kwako ya kumuaga! Mimi na dogo msafisha n.g.o wote hatujaalikwa yan nilifabya kupigiwa simu na mshkaj mwengne tena kuniuliza vp tunaenda sa ngap kwa flan kumuaga, hua najuta kwenda kwenye ile sherehe mpaka leo mana sikuitwa! anyway mpaka leo mwamba yuko USA zaid ya miaka 8, kuna kipindi nyuma alinichek alikuja dar kutembea ila hatukuonana m, daah tunamind kichizi me na dogo wa usafi aliesababisha mchongo. 🤣🤣 on a serious note, me nishampuuzia aisee
 
Mmenitonesha kidonda mwanangu Mirambo milioni 29 uliipeleka wapi? Leo upo kwangu unanipa IDEA za kipumbavu eti bro unajua hutu tubiashara twa kuuza mafuta ya vibaba na nyanya chungu tunalipa watu hawajui tu .Sijui ndio umedata mwanangu.Sema sio case utaishi mdogo wangu .Simu ni moja tu tukutane benki.
 
Pole sana mkuu, kitu nilichojifunza kwenye haya nikujifunza kujipenda mwenyewe Kwanza. Iwe mke, mtoto, Ndugu, rafiki, mchumba wapende Ila jipende mwenyewe Kwanza . Hata ikitokea Hali kama hiyo hutaumia Kwa kiasi kikubwa Bali utachukulia ndio maisha Kwa sababu wewe binafsi ndio furaha yako ya Kwanza.


Usaliti upo na umetuzunguka katika Jamii hili lazima ulitambue

Huyo ni rafiki, kuna MTU kazaa mtoto kamlea, kamsomesha na Leo ni MTU mwenye maisha yake na Hana mpango na wazazi wake utaweza kuvaa viatu vya hao wazazi?

Kuwa na Tabia ya kupuuzia Mambo kama amekuona wewe wa nini na wewe muone WA kazi gani! Jeuri rafiki yake ni kiburi . Endelea na Mishe zako za kutafuta ridhki achana nae.

Usijipe umuhimu kwenye maisha ya watu, jipe umuhimu Kwanza wewe.
 
Mwanaume mwenzako anakutenga unalalamika, Vijana wa siku hizi sisi dah! sasa ukitengwa na Ukoo kama mimi?
Balaa, Kuna mzee mmoja alitengwa na ukoo, halafu katika huo mtaa wanaishi watu wa ukoo wake tuu karibu familia( 200) wote ni ukoo wake, mzee anafanya baishara zake hapo kwenye mtaa, sasa ukoo ulivyomtenga wakawaambia wanaukoo wote hakuna kununua kitu kwa mzee huyu kuanzia sasa, Yule mzee alifunga biashara maana hakuna mtu wa kununua bidhaa yake tena.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Mtafute mweleze hiyo ni kawaida.

Kwani si alikuwa anakuambia kuhusu wapenzi wake 2. Alikukimbia kwasababu gani sasa?
 
Nilishawahi kukimbiwa na rafiki* niliomchukulia kama mdogo wangu) nilikuwa nimeachana na mme, sina income, sina savings, nimehamia sehemu mpya. Nilikuwa sijui mwisho wa mwezi bills nazilipaje.
 
Ya kweli hii?
 
Mtafute mweleze hiyo ni kawaida.

Kwani si alikuwa anakuambia kuhusu wapenzi wake 2. Alikukimbia kwasababu gani sasa?
Eti Kwa sababu nilitumiwa nione video za uchi anavyosex na mchepuko mwingine....Ivo wote tulioona tukio hatutaki maishani mwake
 
kuna Rafiki angu alikuwa anafanya kazi kampun moja ya vipodozi yeye kama maneger wa.ile kampuni kwa hiyo magari yao yalikuw yanaenda mikoani yeye alikuwq anawapa mizgo na hesabu zote anafunga yeye. dahha Jamaa alianza kubadilika.ukimtumia sms hakujibu na anajibu baada ya week moja mbeleee ,alikuwa anajua unataka msaada wake hadi nikaacha sikumtafutaga tena hadi leo....
 
Nilishawahi kukimbiwa na rafiki* niliomchukulia kama mdogo wangu) nilikuwa nimeachana na mme, sina income, sina savings, nimehamia sehemu mpya. Nilikuwa sijui mwisho wa mwezi bills nazilipaje.
Maisha yametulia sasa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…