Ulishawahi kutengwa na rafiki yako wa karibu baada ya yeye kufanikiwa? Toa kisa chako ilikuwaje

Nayo inauma sana, loooh!
Inauma nini??? wkt yale ni Maisha yake binafsi! ameyachagua sasa kwani ulimpa ili umgeme?? yaani wewe utumie akili zake kwa faida yako??

kumbuka hapo umetoa hela yeye katoa akili zake na muda aliotumia kukaa huko shuleni!! kwani huko unadhania hakupata shidaaa!! au ulidhania hiyo hela yako ndo kila kitu kwa Maisha yake??

Km ulimpa kiivo ungemwambia nakupa lkn utanilipa!!…..na hata ivo km unataka akulipe mara tano ya ile hela yako muachane salama km hutaki nyamaza!! huawaga mnageuka sana nyie watu!

siyo kwamba mtu amekupa ndo anakupenda!! wengine huwaga mna test zari tu....mnawageuka na kuwafanya watumwa wenu kwa sababu tu li baba lidogo lilikusaidia!...yana masimango km nini!!

Binafsi nitatoa msaada lkn si kwa masharti!! pia lindugu likinipa nitachukua lkn si kwa lengo la kurudi kwako unitumikishe nitakupiga ngumi ukija na hizo!
 
Vizuri mkuu, if you can run your life at your own, just do it..
 
Hapo ni ujobless tu unakusumbua, tafuta hela utaacha kulaumu watu kizembe zembe.
 
Naomba nikupinge.
Sisi tuna wana, washkaji, best friends, mchizi, halafu kuna mshkaji au mwana wa damu. Huyu atambulishi nyumbani yeye anajulikana nyumbani bila kutambulishwa. Huyu wanaweza kukuta namba zako zote hazipatikani hata miezi minne halafu watampa yeye jukumu la kukutafuta na atakupata. Huyu kaka demu wako haeleweki anakuchana the first day amepata habari, akikuta unapigana haulizi sababu anaingia ktk ugomvi...akimkuta demu wako mazingira mabaya anamchana waziwazi...huyu ni zaidi ya baadhi ya ndugu. Anajua uko na msoto kabla ya kusimulia. Anajua vitu vingi kuhusu wewe hata amabvyo hamjavijadili. Huyu ni mwana, mshkaji, best, mchizi anasifa zote....
Iam luck to have one.
 
Malizia ,tulia andika then malizia story usiwe na haraka
 
Kazi ya daraja sio kungoja shukrani. Wakati mwingine tunakuwa daraja la mafanikio kwa wengine, hata wewe ukijichunguza utagundua wapo waliokusaidia nyuma na ujawalipa fadhila. Tusiishi kwa mategemeo ya kujifungamanisha na wengine.
 
Pole japo kwenye maisha mabadiliko ni lazima. Huwezi tegemea marafiki wa udogoni au shuleni mkaendelea mpaka ukubwani.
Majukumu yanabadilika na pia vipaumbele hubadilika, unaweza hisi hakujali kumbe majukumu yake yanamuweka bize sana muda anaokuwa free anahitaji kufanya mambo muhimu kwa mpangilio. Hawezi tena kuwa na muda wa kupiga soga maskani kama zamani. Pia huko anakutana na marafiki wapya ambao inabidi ajichanganye nao, mara nyingi mtu hutumia muda mwingi wa siku na maisha yake sehemu anapofanyia kazi hivyo anahitaji kuweka mahusiano mazuri.

We endelea kupambana tu ukipata jambo la kukuweka bize wala hutamkumbuka jamaa yako.
 
Mimi ndio hua nawaepuka waliofanikiwa ikiwa sioni msaada wa maana kwao... vimisaada vya kunywa bia havina maana... Kama kuna mchongo wa maana nipe ila kuchorana hua sitak.. Tukutane kwenye matukio muhimu ya kijamii tu.. na kama hatuna blood relationship ndio kabsaa... Hua kuna unafiki mwingi sana kwenye urafiki
 
Exactly
 
So akawa na mawenge km yote?
Sio mawenge tu ndio first time kumuona sio kusikia mtu anafanya ngono na wanawake wawili halafu bamdogo anatamba ni yeye na nduli Amini tu ndio wamefanya mambo hayo.Nunua nyumba dogo milioni nane tu kipindi hiko inauzwa akadai kiwanja kidogo mnoo hawezi kununua.Sasa hivi kila rangi anaiona vizuri sema hatuwezi kumtupa ndio mdogo wetu tenaa.
 
Safi[emoji1317][emoji1317][emoji1317][emoji1317][emoji1317]
 
Huyo ndo mtu sasa wa kushikana nae
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…