Ulishawahi kutengwa na rafiki yako wa karibu baada ya yeye kufanikiwa? Toa kisa chako ilikuwaje

Ulishawahi kutengwa na rafiki yako wa karibu baada ya yeye kufanikiwa? Toa kisa chako ilikuwaje

Nayo inauma sana, loooh!
Inauma nini??? wkt yale ni Maisha yake binafsi! ameyachagua sasa kwani ulimpa ili umgeme?? yaani wewe utumie akili zake kwa faida yako??

kumbuka hapo umetoa hela yeye katoa akili zake na muda aliotumia kukaa huko shuleni!! kwani huko unadhania hakupata shidaaa!! au ulidhania hiyo hela yako ndo kila kitu kwa Maisha yake??

Km ulimpa kiivo ungemwambia nakupa lkn utanilipa!!…..na hata ivo km unataka akulipe mara tano ya ile hela yako muachane salama km hutaki nyamaza!! huawaga mnageuka sana nyie watu!

siyo kwamba mtu amekupa ndo anakupenda!! wengine huwaga mna test zari tu....mnawageuka na kuwafanya watumwa wenu kwa sababu tu li baba lidogo lilikusaidia!...yana masimango km nini!!

Binafsi nitatoa msaada lkn si kwa masharti!! pia lindugu likinipa nitachukua lkn si kwa lengo la kurudi kwako unitumikishe nitakupiga ngumi ukija na hizo!
 
kuna Rafiki angu alikuwa anafanya kazi kampun moja ya vipodozi yeye kama maneger wa.ile kampuni kwa hiyo magari yao yalikuw yanaenda mikoani yeye alikuwq anawapa mizgo na hesabu zote anafunga yeye. dahha Jamaa alianza kubadilika.ukimtumia sms hakujibu na anajibu baada ya week moja mbeleee ,alikuwa anajua unataka msaada wake hadi nikaacha sikumtafutaga tena hadi leo....
Vizuri mkuu, if you can run your life at your own, just do it..
 
Rafiki sijui bff wamakuaga nao madem, sisi tuna wana, washkaji na machizi hawa huwa hatutupani.

Kuna wanangu huwa hatuwasiliani hata mwaka/miaka hata aje na dinga bado mimi ni mwanae, kuna time atakuja na life limemchapa bado ni mwanae.

Wanaume wengi hatuna ile kuwasiliana mara kwa mara, ni pale upate shida au kumpa hi tu ila sio kama mleta uzi, hiyo labda ndio maana unaumia.

Ulikua unategemea rafiki yako akupe furaha kitua ambacho si rahisi kwa muda wote.
Naomba nikupinge.
Sisi tuna wana, washkaji, best friends, mchizi, halafu kuna mshkaji au mwana wa damu. Huyu atambulishi nyumbani yeye anajulikana nyumbani bila kutambulishwa. Huyu wanaweza kukuta namba zako zote hazipatikani hata miezi minne halafu watampa yeye jukumu la kukutafuta na atakupata. Huyu kaka demu wako haeleweki anakuchana the first day amepata habari, akikuta unapigana haulizi sababu anaingia ktk ugomvi...akimkuta demu wako mazingira mabaya anamchana waziwazi...huyu ni zaidi ya baadhi ya ndugu. Anajua uko na msoto kabla ya kusimulia. Anajua vitu vingi kuhusu wewe hata amabvyo hamjavijadili. Huyu ni mwana, mshkaji, best, mchizi anasifa zote....
Iam luck to have one.
 
Matokeo ya darasa la saba yametoka,jina langu linaonyesha natakiwa niingie mbeya sec(mbeya day) ....nachelewa kidogo maandaliz ya kwenda shule kama mjuavyo maisha ya singlemom,mama hakuwa vyema kiuchumi ila ndo ilitakiwa nisome....

Sikuchelewa sana nilikata kama mwez Ivo nikaanza class mwez February katikati.....baada ya mambo yote kukamilika mapokez mwalimu anaenda nionesha darasa napokelewa,darasa limefull kiti Cha kukaa hakuna...natoa macho nao wananishangaa....nikasikia sauti ya binti mbele kidogo ya darasa ikiniita "njoo ukae hapa" [emoji15]kiti kimoja nakaaje(kimoyomoyo)....kainuka kaniachia kiti nikae then kaondoka,katoka darasani(Kumbe anaenda tafuta dawati lake)[emoji26][emoji26](sometimes I miss you cute Jay).....kiufupi tulikaa pamoja yeye Karibu yangu mpaka form four(was my real truly best friend).......

Nakumbuka uliacha comb ya science uliyochagua kisa Kuogopa kutengana nami maana I told you nakupenda nimeumia kutengana nawe darasa....ulistop science ukaja art.....ulipenda kupika nilipenda kuchora.....nilikuwa mkali but mshauri kwako,ulikuwa mlokole but mshauri kwangu.....nilikuwa na mwonekano wa maisha duni lakini niliishi home maisha ya kawaida.....ulikuwa na mwonekano mzuri wa kimavaz lakini uso usio na furaha(alikuwa yatima,alipoegeshwa alikuwa ananyanyaswa sana)....

Nilipofahamu uhalisia wako nilikutambulisha Kwa mama Ivo mama nilikuwa nikimwambia ulichopungukiwa alikuwa mwepesi kukusaidia hata Kwa kukuahidi.(nakumbuka Kaz Yako mojawapo ya kulisha kuku Asubuhi na jioni home kwenu ulikuwa huachi kunifichia mayai ukipata nafasi)[emoji26][emoji26] I miss you darling.....daaa ....ni kisa kirefu sana nitaandika nitatachoka then nitafia hapahapa[emoji24][emoji24][emoji1751]
Malizia ,tulia andika then malizia story usiwe na haraka
 
Kazi ya daraja sio kungoja shukrani. Wakati mwingine tunakuwa daraja la mafanikio kwa wengine, hata wewe ukijichunguza utagundua wapo waliokusaidia nyuma na ujawalipa fadhila. Tusiishi kwa mategemeo ya kujifungamanisha na wengine.
 
Pole japo kwenye maisha mabadiliko ni lazima. Huwezi tegemea marafiki wa udogoni au shuleni mkaendelea mpaka ukubwani.
Majukumu yanabadilika na pia vipaumbele hubadilika, unaweza hisi hakujali kumbe majukumu yake yanamuweka bize sana muda anaokuwa free anahitaji kufanya mambo muhimu kwa mpangilio. Hawezi tena kuwa na muda wa kupiga soga maskani kama zamani. Pia huko anakutana na marafiki wapya ambao inabidi ajichanganye nao, mara nyingi mtu hutumia muda mwingi wa siku na maisha yake sehemu anapofanyia kazi hivyo anahitaji kuweka mahusiano mazuri.

We endelea kupambana tu ukipata jambo la kukuweka bize wala hutamkumbuka jamaa yako.
 
Mimi ndio hua nawaepuka waliofanikiwa ikiwa sioni msaada wa maana kwao... vimisaada vya kunywa bia havina maana... Kama kuna mchongo wa maana nipe ila kuchorana hua sitak.. Tukutane kwenye matukio muhimu ya kijamii tu.. na kama hatuna blood relationship ndio kabsaa... Hua kuna unafiki mwingi sana kwenye urafiki
 
Exactly
 
So akawa na mawenge km yote?
Sio mawenge tu ndio first time kumuona sio kusikia mtu anafanya ngono na wanawake wawili halafu bamdogo anatamba ni yeye na nduli Amini tu ndio wamefanya mambo hayo.Nunua nyumba dogo milioni nane tu kipindi hiko inauzwa akadai kiwanja kidogo mnoo hawezi kununua.Sasa hivi kila rangi anaiona vizuri sema hatuwezi kumtupa ndio mdogo wetu tenaa.
 
Umenikumbusha mbali, nilikuwa na best yaani tunaendana mpk rangi za nguo nimazopenda nae anapenda. Alienda soma Kenya akarudi bado tunawasilia vizuri tuu, kuna siku aliniambia unajua kula Amini, nikamwambia ndiyo basi miye nataka tufanye hivyo. Nikamwambia usijali miye nakupenda km ndugu yangu baba moja sintakupoteza wewe ndugu yangu. Funguo ya pale kwao alichonga nyingine akanipa mimi maana yeye alikuwa mwenyewe wa Daslam.

Aliporudi Kenya huko alipata kazi sehemu mbali mbali na mimi nilichelewa kuanza chuo kwa hiyo nikiishiwa namfuata namwambia leo sina hela ya kula anaitoa za maana tuu nasogeza siku. Nakumbuka kuna siku Brick&lace alikuja bongo kwenye BSS alikuja chuo akakuta watu wapo bize na safari za huko. Akaniuliza wee vipi huendi nikamwambia sina mshiko akanipa pesa ya kiingilio na nauli alafu akaniiambia utakufa bila mimi wewe shauri zako. Nami nikamwambia kiranga chako cha kupata kazi mapema. Nilienda na kuinjoi vizuri tuu.

Nakumbuka kuna siku alinifuata nilipo na kuniambia unamjua ....... nikamwambia ndiyo namjua ila siyo sana, akasema basi yule mtu wangu bla bla bla duuuh. Nikamwambia utawezana nae maana huyo rafiki wa kishua sana akasema looh yaani bado hujanijua tuu dear siku zoote hizo mimi naweza ishi popote, nika.mwambia najua lkn kwenye mahusiano mmh jaribu tuone.

Hapo kati yalitokea masebeni kibao mimi maisha yangu sipendi kuingilia ugomvi wa wapenzi lkn yule nilikuwa frontline, na ndiyo mwanzo na mwisho. Mwisho wa ndoa ikafungwa wakati huo bado nipo kitaa 1 haisomi mbili haikamati. Ila nilipigani nikashiriki vyoote vinavyohusu harusi.

Advarsities hakuniambia anaishi wapi baada ya harusi, maana km wk tatu mzee wake alifariki nilifika pale kwao, miye teena nikamuuliza vipi ...... hawajambo huko, akasema haaa miye sikai huko teena nikatoa macho duuuh. Nikatulia maana mawasiliano yalipungua sana wkt huo.

Tukazika salama nikasepa zangu kwenye mishe zangu za kitaaa,nipo zangu home naona rafiki yake aliyenitambulisha ananisalimia na kunijulisha kuna ....... ana baby nikasema hongera zake ila anapaswa anijulishe yeye mwenyewe maana mimi na yeye tumekwepa mishale kibweeena. Rafiki umbeya ukamwisha akachoka roho na mwili.

Fast mtoto wa pili, mimi nikapata kazi sasa, wakati hapo sasa nimejitaarisha kwenda kumwambia bize jasho linanitoka kumuelezq rafiki ALLAH kasikia kilio changu, piga simu weee hapokei nikasema ngoja nimfate ofisini kwake. Nafika getini mlinzi ananiambia hivi hujakutana nae hapo road mmepisha eeenhh. Maana ofisi nzima walikiwa wananijua miye ndugu yake siyo rafiki kabisa.

Nikamchan mbona hupokei simu zangu kwani nakudai, hakujibu nikampotezea mazima toka hapo mpk kesho.
Niliona kwenye group ana watoto watatu sijawahi waona wala sijui anakaa wapi ingawa eneo nalijua ila nyumbani kwake sijqkanyaga. Nimempotezea nae kanipotezea na hatujawahi kukutana.

Kuna siku mtu wa Advance akaniita kwake akaniuliza hivi .... upo sawa na ..... nikamjibu tupo sawa akasema kama kweli mpigie simu nione, nilipiga ile simu nikaongea nae machache lkn haikusidia na pia alishangaa maana alikuwa anaonhea kwa taadhali kubwa sana na siyo kawaida yake kumbe mwenzake nilikuwa anafanyiwa assessment nyoko yule.

Nilipofunga ndoa aliniandikia waraka mrefu wa kunipongeza lkn nilipopata watoto hakuniandikia teeena.
Sina habari maisha yanasongo naona hata namba kabdili sasa maana washikaji zetu wananiuliza tunaomba nambaza ..... nawapa ile ya zamani maana ukiwajibu sina mpya utawapa la kusema wanamtafuta hawampati nawaambia chukueni hiyo ya mdogo wake labda simu mbovu.

Aaah nimeamini kila mtu anakuja kwa wakati wake ili msaidiane na mvushane hiyo sehemu.
Vitu vinavyovuruga urafiki KAZI mmoja akianza kupata, NDOA mmoja akianza kuipata na km hawezi zile marufuku.
Safi[emoji1317][emoji1317][emoji1317][emoji1317][emoji1317]
 
Matokeo ya darasa la saba yametoka,jina langu linaonyesha natakiwa niingie mbeya sec(mbeya day) ....nachelewa kidogo maandaliz ya kwenda shule kama mjuavyo maisha ya singlemom,mama hakuwa vyema kiuchumi ila ndo ilitakiwa nisome....

Sikuchelewa sana nilikata kama mwez Ivo nikaanza class mwez February katikati.....baada ya mambo yote kukamilika mapokez mwalimu anaenda nionesha darasa napokelewa,darasa limefull kiti Cha kukaa hakuna...natoa macho nao wananishangaa....nikasikia sauti ya binti mbele kidogo ya darasa ikiniita "njoo ukae hapa" [emoji15]kiti kimoja nakaaje(kimoyomoyo)....kainuka kaniachia kiti nikae then kaondoka,katoka darasani(Kumbe anaenda tafuta dawati lake)[emoji26][emoji26](sometimes I miss you cute Jay).....kiufupi tulikaa pamoja yeye Karibu yangu mpaka form four(was my real truly best friend).......

Nakumbuka uliacha comb ya science uliyochagua kisa Kuogopa kutengana nami maana I told you nakupenda nimeumia kutengana nawe darasa....ulistop science ukaja art.....ulipenda kupika nilipenda kuchora.....nilikuwa mkali but mshauri kwako,ulikuwa mlokole but mshauri kwangu.....nilikuwa na mwonekano wa maisha duni lakini niliishi home maisha ya kawaida.....ulikuwa na mwonekano mzuri wa kimavaz lakini uso usio na furaha(alikuwa yatima,alipoegeshwa alikuwa ananyanyaswa sana)....

Nilipofahamu uhalisia wako nilikutambulisha Kwa mama Ivo mama nilikuwa nikimwambia ulichopungukiwa alikuwa mwepesi kukusaidia hata Kwa kukuahidi.(nakumbuka Kaz Yako mojawapo ya kulisha kuku Asubuhi na jioni home kwenu ulikuwa huachi kunifichia mayai ukipata nafasi)[emoji26][emoji26] I miss you darling.....daaa ....ni kisa kirefu sana nitaandika nitatachoka then nitafia hapahapa[emoji24][emoji24][emoji1751]
Huyo ndo mtu sasa wa kushikana nae
 
Back
Top Bottom