Ulishawahi kutengwa na rafiki yako wa karibu baada ya yeye kufanikiwa? Toa kisa chako ilikuwaje

Ulishawahi kutengwa na rafiki yako wa karibu baada ya yeye kufanikiwa? Toa kisa chako ilikuwaje

Mleta bandiko nakuelewa sana.

Mara nyingi inakuwa hivyo, tena unaweza ukawa unajitoa kwa hali na mali baadae wenzako/mwenzako akitoboa anakutenga.

Niamini haya maneno ninayokuambia, usihuzunike wewe pambana kivyako utakuja kuniambia siku moja, yaani lazima utoboe.

Sijui kuna siri gani!, ninachokuambia hapa sio cha kuhadithiwa
 
Umenikumbusha mbali, nilikuwa na best yaani tunaendana mpk rangi za nguo nimazopenda nae anapenda. Alienda soma Kenya akarudi bado tunawasilia vizuri tuu, kuna siku aliniambia unajua kula Amini, nikamwambia ndiyo basi miye nataka tufanye hivyo. Nikamwambia usijali miye nakupenda km ndugu yangu baba moja sintakupoteza wewe ndugu yangu. Funguo ya pale kwao alichonga nyingine akanipa mimi maana yeye alikuwa mwenyewe wa Daslam.

Aliporudi Kenya huko alipata kazi sehemu mbali mbali na mimi nilichelewa kuanza chuo kwa hiyo nikiishiwa namfuata namwambia leo sina hela ya kula anaitoa za maana tuu nasogeza siku. Nakumbuka kuna siku Brick&lace alikuja bongo kwenye BSS alikuja chuo akakuta watu wapo bize na safari za huko. Akaniuliza wee vipi huendi nikamwambia sina mshiko akanipa pesa ya kiingilio na nauli alafu akaniiambia utakufa bila mimi wewe shauri zako. Nami nikamwambia kiranga chako cha kupata kazi mapema. Nilienda na kuinjoi vizuri tuu.

Nakumbuka kuna siku alinifuata nilipo na kuniambia unamjua ....... nikamwambia ndiyo namjua ila siyo sana, akasema basi yule mtu wangu bla bla bla duuuh. Nikamwambia utawezana nae maana huyo rafiki wa kishua sana akasema looh yaani bado hujanijua tuu dear siku zoote hizo mimi naweza ishi popote, nika.mwambia najua lkn kwenye mahusiano mmh jaribu tuone.

Hapo kati yalitokea masebeni kibao mimi maisha yangu sipendi kuingilia ugomvi wa wapenzi lkn yule nilikuwa frontline, na ndiyo mwanzo na mwisho. Mwisho wa ndoa ikafungwa wakati huo bado nipo kitaa 1 haisomi mbili haikamati. Ila nilipigani nikashiriki vyoote vinavyohusu harusi.

Advarsities hakuniambia anaishi wapi baada ya harusi, maana km wk tatu mzee wake alifariki nilifika pale kwao, miye teena nikamuuliza vipi ...... hawajambo huko, akasema haaa miye sikai huko teena nikatoa macho duuuh. Nikatulia maana mawasiliano yalipungua sana wkt huo.

Tukazika salama nikasepa zangu kwenye mishe zangu za kitaaa,nipo zangu home naona rafiki yake aliyenitambulisha ananisalimia na kunijulisha kuna ....... ana baby nikasema hongera zake ila anapaswa anijulishe yeye mwenyewe maana mimi na yeye tumekwepa mishale kibweeena. Rafiki umbeya ukamwisha akachoka roho na mwili.

Fast mtoto wa pili, mimi nikapata kazi sasa, wakati hapo sasa nimejitaarisha kwenda kumwambia bize jasho linanitoka kumuelezq rafiki ALLAH kasikia kilio changu, piga simu weee hapokei nikasema ngoja nimfate ofisini kwake. Nafika getini mlinzi ananiambia hivi hujakutana nae hapo road mmepisha eeenhh. Maana ofisi nzima walikiwa wananijua miye ndugu yake siyo rafiki kabisa.

Nikamchan mbona hupokei simu zangu kwani nakudai, hakujibu nikampotezea mazima toka hapo mpk kesho.
Niliona kwenye group ana watoto watatu sijawahi waona wala sijui anakaa wapi ingawa eneo nalijua ila nyumbani kwake sijqkanyaga. Nimempotezea nae kanipotezea na hatujawahi kukutana.

Kuna siku mtu wa Advance akaniita kwake akaniuliza hivi .... upo sawa na ..... nikamjibu tupo sawa akasema kama kweli mpigie simu nione, nilipiga ile simu nikaongea nae machache lkn haikusidia na pia alishangaa maana alikuwa anaonhea kwa taadhali kubwa sana na siyo kawaida yake kumbe mwenzake nilikuwa anafanyiwa assessment nyoko yule.

Nilipofunga ndoa aliniandikia waraka mrefu wa kunipongeza lkn nilipopata watoto hakuniandikia teeena.
Sina habari maisha yanasongo naona hata namba kabdili sasa maana washikaji zetu wananiuliza tunaomba nambaza ..... nawapa ile ya zamani maana ukiwajibu sina mpya utawapa la kusema wanamtafuta hawampati nawaambia chukueni hiyo ya mdogo wake labda simu mbovu.

Aaah nimeamini kila mtu anakuja kwa wakati wake ili msaidiane na mvushane hiyo sehemu.
Vitu vinavyovuruga urafiki KAZI mmoja akianza kupata, NDOA mmoja akianza kuipata na km hawezi zile marufuku.
 
Umenikumbusha mbali, nilikuwa na best yaani tunaendana mpk rangi za nguo nimazopenda nae anapenda. Alienda soma Kenya akarudi bado tunawasilia vizuri tuu, kuna siku aliniambia unajua kula Amini, nikamwambia ndiyo basi miye nataka
Aisee..
Kutokana na mparaganyiko wa stori yako kutoielewa, nimejikuta nimesoma yote ili nikidhani nitaelewa baada ya mistari kadhaa inayokuja, nimeendelea hivyo mpaka mwisho, duuh...
Haya tunasubiri sehemu ya pili...... 🙃
 
Sasa changamoto imekuja kuonekana baada ya huyu mwenzangu kuwa amebahatika kupata chaka sehemu, yaani imekuwa si yeye ninaemfahamu tena. Kwa ukaribu wangu na yeye sidhani hata kama ni kubanana inaweza kuwa kwa mwenendo huu anaouonyesha. Imekuwa ni mara chache sana siku hizi kuonana tena involuntarily ingawa najua yupo, na baadhi ya watu anakutana nao anapokuwa nje ya majukumu yake ila si mimi tena. Unaweza kumtumia ujumbe usijibiwe kabisa na tangu aanze kazi nakumbuka alinitumia ujumbe siku mbili tu za kwanza tangu alipoanza kazi.
Maisha ni kupanda na kushuka, pambana ipo siku utapanda naye atashuka
 
Wakuu habari za wakati huu! Nina Imani mu wazima wa afya na mnaendelea kupambana na maisha ya Kila siku. Mungu atusaidie sana.

Kama ambavyo title inajieleza, Mimi ni mtu ambae sina marafiki wengi, si kwakuwa ninajiskia sana, hapana ila ni aina ya watu
...Samahani, lakini Rafiki Yako ni Mshamba. Piga Chini...[emoji35]
 
Kifupi mswahili Ni mbwa.
Msaidie Ila usije ukategemea msaada kutoka kwake. Hata salaam sahau.
Ndugu yako ni mke/mume wako na watoto wako tu. Sahau kitu inaitwa dada au Kaka.
Take it from me and thank me later.
I got you mkuu
 
Umenikumbusha mbali, nilikuwa na best yaani tunaendana mpk rangi za nguo nimazopenda nae anapenda. Alienda soma Kenya akarudi bado tunawasilia vizuri tuu, kuna siku aliniambia unajua kula Amini, nikamwambia ndiyo basi miye nataka tufanye hivyo. Nikamwambia usijali miye nakupenda km ndugu yangu baba moja sintakupoteza wewe ndugu yangu. Funguo
Mkuu binadamu tumeumbiwa kusahau pale tunapovuka hatua moja ya maisha. Ila hatma ya maisha yetu anayo muumba. Nafrahi kusikia ulipata kazi pia na maisha yako yanaendelea kama kawaida
 
Mkuu
Mleta bandiko nakuelewa sana.

Mara nyingi inakuwa hivyo, tena unaweza ukawa unajitoa kwa hali na mali baadae wenzako/mwenzako akitoboa anakutenga.

Niamini haya maneno ninayokuambia, usihuzunike wewe pambana kivyako utakuja kuniambia siku moja, yaani lazima utoboe.

Sijui kuna siri gani!, ninachokuambia hapa sio cha kuhadithiwa
Mkuu nashukuru, nitazidi kupambana pia
 
Back
Top Bottom