Ulishawahi kuumbuliwa kwa kitu ulichokuwa unajifanya kukijua sana?

Ulishawahi kuumbuliwa kwa kitu ulichokuwa unajifanya kukijua sana?

BIG STONE AND CONER STONE

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2023
Posts
421
Reaction score
728
Nirudi kwangu kwanza, kipindi nikiwa nasoma mkoa kama umefika Dar ulionekana bonge la mjanjaa! Sasa nikiwa shule ya msingi chini ya 2000 huko mwalimu yoyote akiuliza swali la nani anajua Dar es Salam, Big stone and coner stone nakuwa wa kwanza kusimama.

Nani anajua maji ya bahari yana ladha gani? Huyo Nasimama! Nani anajua kigambon? Nasimama. Mwalimu akiuliza navuka kwa kupitia nini, najibu Pantoni! Walimu; tena mpigieni makofi👏👏🥰, nikawa ka star ka Daslama.

Ikawa sasa darasani kuhusu Dar huniambii kitu. Sasa akaja mwalimu mmoja wa sayansi akauliza nani amefika Dar, wanafunzi wote macho kwangu, huyooo nikasimama. Ehee mwalimu sasa akauliza simtank Ni nn? Duuh nilikodoa macho 😀😀😀😀

Kipindi hayo ma simtak wala siyajui ni kitu gani. Nikajibu ni simu ya kumpigia Waziri Mkuu 😀😄Mwalimu alicheka sana, karbu nile mboko/fimbo. Jibu ilikuwa ni matanki ya kuhifadhi maji. Kuanzia hapo kiherehere cha kuijuia Daslama. Kiliisha.

Nikapata na marafiki darasani maana kidogo yale madogo yalianza nitenga kisa hayajui Dar😛. Anyways, nilibadilika na kuwa na mtazamo mzuri hadi leo hata kama najua kitu sisemi mpaka niulizwe direct!

Kiburi cha Dar kikashuka nikawa mtu POA kwa namna ninavyojiona sasa!

Waweza funguka nini hususani shule za msingi huko, utotoni?
 
Hahaha
Mm nilikuwa nawawekea madem kipande cha kioo chini ya dawati ili niwachungulie kupitia kiaa bila kujua wala sikuwa naona kitu. Siku moja ilikuwa mchana hivi mwalimu wa kike akawa anakuja kuanza kipindi kioo kika reflect na mwanga wa jua akauliza nani mwenye kioo mtego ukagundulika nilikula mboko sitasahau. Niliishia hapo mambo ya chabo ilikuwa darasa la nne
 
kwa hiyo mkuu unataka turudi kwenye maduka ya ushirika? kilimo kutumisha MFUMAKI (Mfuko wa Maendeleo wa Kijiji) 😀 Vyama vya Ushirika, KNCU; Wakala wa Meli - NASACO nk
 
kwa hiyo mkuu unataka turudi kwenye maduka ya ushirika? kilimo kutumisha MFUMAKI (Mfuko wa Maendeleo wa Kijiji) 😀 Vyama vya Ushirika, KNCU; Wakala wa Meli - NASACO nk
Rudi tu ndio historia yenyewe Sasa.
Kuna nchi wao wanakumbuka Vita Kati kundi hili na serekali wala hakukua na Amani eleza tu! Hayo yote ya tz n Aman tu!
 
Nilikuwa namuongelea mtu fulani mashuhuri hapa Tanzania na kutoa story yake as if ninamjua kiundani halafu pembeni alikuwapo auntie mmoja ambaye anajuana na familia yao yote na wapo group moja la Whatsapp na anajua issue yote from A to Z.

Niliona aibu.
 
Back
Top Bottom