Mzurulaji
JF-Expert Member
- Sep 25, 2021
- 283
- 639
Habari wa JF.
Mwezi wa tatu unakimbia kwa kasi sana.
Hivi ulishawahi kuwa kwenye mahusiano na mtu usiyempenda kabisa tena kwa muda mrefu. Au hata kuingia naye kwenye ndoa.
Binafsi ishanitokea nilikuwa kwenye mahusiano na mwanamke ambaye sikuvutiwa naye. Kama ilivyo slogan yangu huwa nahuruma sana. Usumbufu wa mwanamke unaweza kunifanya nibadiri jibu hapana kuwa ndio sababu tu ya huruma.
Nakumbuka nilishawahi kumtongoza mwanamke ambaye tuseme nilimtamani kwa muda mfupi. Ila nilikuja kugundua sikuwa nimempenda. Nimedumu naye kwenye mahusiano miezi miwili tu. Mwisho wa siku nikaona kama namuumiza na kumpotezea muda. Nikaamua nimweleze ukweli japo aliumia sana.
Aliniomba nimpe muda atanifanya nimpende na niwe na hisia naye. Lakini nilimsihi yakuwa sitaki kuendelea kumuumiza.
Ndipo ukawa mwisho wa mimi na yeye.
Je, nawe ishakukuta au kukutokea hii..?