Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 98,439
- 145,410
Katika historia ya Tanzania hakuna mtu ambaye amewahi kushinda urais kwa asilimia 97.6 za kura zote zilizopigwa.
Na katika hiyo hiyo historia yetu, hakuna mtu ambaye amewahi kuchaguliwa kwa kura nyingi sana zaidi yako wewe.
Umechaguliwa kwa kura zaidi ya milioni 31. Idadi hiyo ni takriban karibu nusu nzima ya idadi ya Watanzania.
Hakika umeandika historia, si tu nchini wala barani Afrika, bali duniani kote.
Ila cha kushangaza, matendo yako pamoja na kauli zako, haviendani kabisa na kiwango cha ushindi wako.
Uliapishwa uchochoroni. Hukuwapa hao wapiga kura wako milioni 31 fursa ya kufurahia ushindi wako huo mkubwa kwa kuhudhuria uapisho wako.
Tokea ushinde huo ushindi wako, hujaingia mtaani kujichanganya na kuwashukuru hao wapiga kura wako.
Tokea ushinde huo ushindi wako, umekuwa ni mtu wa makasiriko tu.
Kila ukiongea unavimbisha mashavu na kuwashikia kiuno wale wote unaodhani wanakupinga. Mpaka umewaletea jeuri wafadhili wanaokupa hela za kuendesha serikali yako. Na wao wameanza kukujibu. Tuone kama utaendelea na hiyo jeuri yako.
Tokea ushinde huo ushindi umekuwa ni mtu wa kutoa kauli zinazokinzana.
Mara useme wale waandamanaji walikuwa ni raia wa kigeni. Mara sijui walikuwa ni watoto waliokuwa wanafuata mkumbo. Mara hivi, mara vile.
Juzi hapa umekiri kuwa serikali yako ndo iliyoua watoto wa Kitanzania kwa sababu katika akili yako, hao watoto walitaka kukupindua.
Lakini kabla ya hapo uliunda tume yako ya kujichunguza kuhusu kilichotokea.
Yaani kwa kifupi ni hueleweki. Kichwa chako kimejaa mawenge na mazonge.
Kila ukifungua mdomo wako ndo unazidi kujichimbia shimo.
Sijawahi kuona mtu aliyeshinda uchaguzi kwa kiwango chako cha ushindi, kufanya matendo ambayo ni kinyume kabisa na ushindi ulioupata.
Naamini yote hayo ni kwa sababu dhamiri yako inakusuta.
Natamani uendelee kufungua mdomo wako kila siku.
La mwisho, ua tena watoto wa Kitanzania hiyo Disemba 9 ili nawe uharakishe mwisho wako na uepuke kwenda ICC maana kutakuwa hakuna haja ya kukufukisha huko maana mahakama ya Watanzania itakushughulikia haraka sana.