Yeah....Daah... arra yule jamaa aseeh alipotea mapema.
Hiyo ishu ilikuwa noma
Sipatii picha hizo bakora [emoji3][emoji3]Duh!!
Kwanza nilikuwa mtundu sana,mpaka nikapewa uongozi Ili niwadhibiti watundu wenzangu.
Pili,nilikuwa na some sort of ukorofi nikapewa jina dakika mbili mbele.
Tatu,kuna mwalimu alikosea kusema neno la kiingereza assembly,alisema menyi instead of many,nilitoa kicheko kimoja hiko ambacho kilinigharimu nililambwa bakora za Maana. Majina yote yakafa nikaanza kuitwa menyiii
Na nani tena alikufanyia visa?mchezaji maarufu na muhimu wa netball (GS) ,, kuongea bila bleki lkn kila nitalaloliongea lazima watu mbavu ziwabane kwa kucheka,, kuongoza somo la kiswahili tangu shule ya msingi lakini ajabu necta form 4 nilifanyiwa visa nikapata F
nnao lakini umepunguaMdomo bado unao?[HASHTAG]#Demba[/HASHTAG]
Bado unatabia ya kuiba?1. Utoro, nimeanza utoro toka darasa la kwanza, nakumbuka hadi mtihani wa kwenda darala la pili nilikuja kushtuliwa na mshikaji huku washafanya hisabati, darasa la pili hivyo hivyo, la tatu nilisoma mwezi mmoja kisha nikatokomea kusikojulikana eti nikaibuka kufanya mtihani wa darasa la nne, mwalimu akanigomea ikabidi wanirudishe tena la tatu.
Ilipofika darasa la 6 nikarudia tabia yangu nikaja kuibuka la 7, shuleni walikua wananijua kwa sufa moja tu, utoro sugu ila siku nikiibuka kwenye mtihani namba moja hadi 3 hainikosi.
2. Utorokaji, jamani nilikua natoroka shule balaa, hadi nilipohamishiwa kwa mwalimu bado nikawa natoroka tu kwenda hom, mwalim hakunichapa aliniweka chini akanishauri nikaacha kutoroka ila nilipoenda secondari nikarudia tabia ya kutoroka na kuchelewa..
Sekondari nikasoma shule ya bweni ya serikali iko katikati ya mji, ikawa kila wiki lazima nitoroke kuanzia ijumaa narudi jumatatu alfajiri maana hapo mjini alikuwepo baba mdogo na akawa hanimind maana matokeo yangu hayakua na shida.
3. Kuna tabia nyingine nilikua nazo ingawa hazikua zinajulikana ni wizi wa madaftari na kalam, kila mhula ukianza tulikua tunapewa/kuja na madaftari mapya huko shule ya msingi, sijawahi kukunua daftari, nilikua na hom library yangu ya madaftari ya wizi mapya najaladia tu jalada zuri huwezi kujua ni yako.
Sekondari pia hivyo hivyo, wale waliokua na miandiko mizuri na mpangilio mzuri wa maandishi ilikua ikikaribia tu mtihani lazima niibe madaftari yao nikajisomee, mitihani ikiisha naweza kulirudisha hapo darasani nikalitelekeza au nikaamua kulificha kabisa.
Sure nimeyamisi sana maisha ya shule.
Bwana rudisha jina lakoNdiyo yeye bwana.
Hapana, wizi wangu ulikua ni madaftari tu maana nilikua mvivu wa kuandika notes na mtu ukimuomba daftari ukasome anauliza kwa nini hukuandika notes, sasa kuepuka usumbufu wa kuulizana nilikua naiba daftari.Bado unatabia ya kuiba?
Hujawahi kustukiwa?Hapana, wizi wangu ulikua ni madaftari tu maana nilikua mvivu wa kuandika notes na mtu ukimuomba daftari ukasome anauliza kwa nini hukuandika notes, sasa kuepuka usumbufu wa kuulizana nilikua naiba daftari.
Baada ya kumaliza shule na hayo yakaishia hapo hapo. Huo wizi ulikua shule ya msingi na sekondari ya kawaida, nilipoenda kidato cha tano hakukua na haja ya kuiba madaftari maana hakukua na haja ya kuandika sana zaidi ya kusoma vitabu na vijitabu vya waalimu wa tuition.
π π πTulipokuwa darasa la nne, mwanafunzi mmoja darasani aliibiwa mfutio, mwalimu wetu wa darasa alitupanga mstari ma kuanza kusachi mifukoni mwetu. Bahati mbaya wakati huo wengi hatukuwa tunavaa chupi, na bahati mbaya zaidi mifuko yangu ilichanika kwa ndani, mwalimu alipoingiza mkono wake mfukoni kwangu ukapitiliza ukakamata nyoka. Nilipigajwe siku hiyo.
Wakati tukiwa tunasoma kila mtu alikuwa na sifa zake na tabia ambazo zilifahamika sana kwa wanafunzi wenzako
.
Mfano Mimi nilipokuwa shule nilikuaga mpiga kelele sugu darasan
.Nilikuaga siandiki notes darasani wala kujibu maswali darasani lakini pia
.Nilikuaga fundi wa kujitetea pale napokutwa na kesi yaani mwalimu alikuwa akinipa fursa ya kujitetea basi hawezi niadhibu najitetea hadi ananiacha"
Je wewe ulikuwa na sifa gani Unazozikumbuka wakati ukiwa unasoma?
Mseminary wewe eti!Kusomea ndani ya chumba cha generator la shule, hadi siku moja Gombera akanikamata wenzangu wakiwa kwenye misa ya asubuhi.