Ulisifika Kwa Lipi Shuleni....

Ulisifika Kwa Lipi Shuleni....

Daah... arra yule jamaa aseeh alipotea mapema.

Hiyo ishu ilikuwa noma
Yeah....

Kuna kipindi walinunua mfuko wa kg 50 za sukari na mkopo Nido .

Member wa chai wote tulihamia kwao.... Tatizo daby ulikuwa Mzee wa misuli saana hizo mambo zilikupita
 
Duh!!
Kwanza nilikuwa mtundu sana,mpaka nikapewa uongozi Ili niwadhibiti watundu wenzangu.
Pili,nilikuwa na some sort of ukorofi nikapewa jina dakika mbili mbele.
Tatu,kuna mwalimu alikosea kusema neno la kiingereza assembly,alisema menyi instead of many,nilitoa kicheko kimoja hiko ambacho kilinigharimu nililambwa bakora za Maana. Majina yote yakafa nikaanza kuitwa menyiii
Sipatii picha hizo bakora [emoji3][emoji3]
 
1. Utoro, nimeanza utoro toka darasa la kwanza, nakumbuka hadi mtihani wa kwenda darala la pili nilikuja kushtuliwa na mshikaji huku washafanya hisabati, darasa la pili hivyo hivyo, la tatu nilisoma mwezi mmoja kisha nikatokomea kusikojulikana eti nikaibuka kufanya mtihani wa darasa la nne, mwalimu akanigomea ikabidi wanirudishe tena la tatu.

Ilipofika darasa la 6 nikarudia tabia yangu nikaja kuibuka la 7, shuleni walikua wananijua kwa sufa moja tu, utoro sugu ila siku nikiibuka kwenye mtihani namba moja hadi 3 hainikosi.

2. Utorokaji, jamani nilikua natoroka shule balaa, hadi nilipohamishiwa kwa mwalimu bado nikawa natoroka tu kwenda hom, mwalim hakunichapa aliniweka chini akanishauri nikaacha kutoroka ila nilipoenda secondari nikarudia tabia ya kutoroka na kuchelewa..

Sekondari nikasoma shule ya bweni ya serikali iko katikati ya mji, ikawa kila wiki lazima nitoroke kuanzia ijumaa narudi jumatatu alfajiri maana hapo mjini alikuwepo baba mdogo na akawa hanimind maana matokeo yangu hayakua na shida.

3. Kuna tabia nyingine nilikua nazo ingawa hazikua zinajulikana ni wizi wa madaftari na kalam, kila mhula ukianza tulikua tunapewa/kuja na madaftari mapya huko shule ya msingi, sijawahi kukunua daftari, nilikua na hom library yangu ya madaftari ya wizi mapya najaladia tu jalada zuri huwezi kujua ni yako.

Sekondari pia hivyo hivyo, wale waliokua na miandiko mizuri na mpangilio mzuri wa maandishi ilikua ikikaribia tu mtihani lazima niibe madaftari yao nikajisomee, mitihani ikiisha naweza kulirudisha hapo darasani nikalitelekeza au nikaamua kulificha kabisa.

Sure nimeyamisi sana maisha ya shule.
Bado unatabia ya kuiba?
 
Bado unatabia ya kuiba?
Hapana, wizi wangu ulikua ni madaftari tu maana nilikua mvivu wa kuandika notes na mtu ukimuomba daftari ukasome anauliza kwa nini hukuandika notes, sasa kuepuka usumbufu wa kuulizana nilikua naiba daftari.

Baada ya kumaliza shule na hayo yakaishia hapo hapo. Huo wizi ulikua shule ya msingi na sekondari ya kawaida, nilipoenda kidato cha tano hakukua na haja ya kuiba madaftari maana hakukua na haja ya kuandika sana zaidi ya kusoma vitabu na vijitabu vya waalimu wa tuition.
 
Hapana, wizi wangu ulikua ni madaftari tu maana nilikua mvivu wa kuandika notes na mtu ukimuomba daftari ukasome anauliza kwa nini hukuandika notes, sasa kuepuka usumbufu wa kuulizana nilikua naiba daftari.

Baada ya kumaliza shule na hayo yakaishia hapo hapo. Huo wizi ulikua shule ya msingi na sekondari ya kawaida, nilipoenda kidato cha tano hakukua na haja ya kuiba madaftari maana hakukua na haja ya kuandika sana zaidi ya kusoma vitabu na vijitabu vya waalimu wa tuition.
Hujawahi kustukiwa?
 
Nidhamu ya uoga iliyo tukuka. form 1 mpka 4 bila kuchapwa bakora hata moja na shule ya bweni ya serikali enzi hizo 90's
 
Tulipokuwa darasa la nne, mwanafunzi mmoja darasani aliibiwa mfutio, mwalimu wetu wa darasa alitupanga mstari ma kuanza kusachi mifukoni mwetu. Bahati mbaya wakati huo wengi hatukuwa tunavaa chupi, na bahati mbaya zaidi mifuko yangu ilichanika kwa ndani, mwalimu alipoingiza mkono wake mfukoni kwangu ukapitiliza ukakamata nyoka. Nilipigajwe siku hiyo.
😀 😀 😀
 
Mtu mwenye surname/jina la ukoo linalo chekesha kuliko wote, wakati wa kuitwa majina darasani ikifika zamu yangu lazima watu wacheke

Ila nilikuwa nawakomesha kila mwisho wa term wananipigia mokofi kwa kuwaburuza

Listi ya watu wenye Fujo nipo, team ya mpira wa miguu nipo, team ya basketball nipo, kwenye riadha nipo halafu mwisho wa term ni wa kwanza au wapili.
 
Wakati tukiwa tunasoma kila mtu alikuwa na sifa zake na tabia ambazo zilifahamika sana kwa wanafunzi wenzako
.
Mfano Mimi nilipokuwa shule nilikuaga mpiga kelele sugu darasan
.Nilikuaga siandiki notes darasani wala kujibu maswali darasani lakini pia
.Nilikuaga fundi wa kujitetea pale napokutwa na kesi yaani mwalimu alikuwa akinipa fursa ya kujitetea basi hawezi niadhibu najitetea hadi ananiacha"

Je wewe ulikuwa na sifa gani Unazozikumbuka wakati ukiwa unasoma?

Ufupi aloo.

Nilikuwa mfupi mpaka wakawa wananiita Mrefu. Chaaa!
 
Walikua wananiita opong weah maana nilikua naingia nazo nyavuni zile K za kijijin kama sina akili ..jioni kwenye bondo natoa maziwa niliopewa na wameru daah aisee
 
ujanja ujanja tokea primary mpaka chuo kikuu,hii ni kutokana na muonekano wa sura yangu,ongeaji na ujuaji mwingi.
nilipokuwa chuo kikuu niliwahi kuingia chumba cha ma waalimu wakiwa zaidi ya 6,mwl moja akaniambie ujeu ww umekaa kiujanja janja sana hata mtu kuamini kitu filani juu yako si rahisi
 
Back
Top Bottom