Ulisifika Kwa Lipi Shuleni....

Nilikuwa muongo had leo muongo tu na hata nilichoandika enyewe uongo
 
Primary nilikuwa najua sana maarifa ya jamii na historia, nikapewa jina la Kinjekitile.

O level form one nimeingia tu ikawa napenda kujibujibu maswali lakini nilikuwa naenda nje ya mada jamaa wakanipa jina la 'nje ya mada'

Form two na form three jamaa wakanipa jina la Tozi.. Maana ilikuwaga nakuja shule na vibegi vya ajabu ajabu vya kushona coz mama alikuwa fundi cherehani... Mara leo kibegi cha salfeti kesho pazia limefanywa begi.. Basi tu yaani mapigo tofauti tofauti

Advence nilikuwa mpole maana nilikuwa kwenye tension ya hali ya juu. Nilikuwa na msongo mkubwa sana wa mawazo 1) family kulikuwa hakuelewiki na maisha magumu kishenzi, so all two years nilikuwa kama msukule lengo moja tu nisome nifaulu niende chuo.. Sikuwa na mbwembwe nyingi

Chuo pia naingia kama vile advance sikutaka mbwembwe nyingi all i wanted was to make wonders and gladly i did mpaka kesho am proud for that.

But yote kwa yote since primary mpaka secondary na mpaka chuo nimekuwa mchelewaji maarufu.. Mpaka kazini nimekuwa nikichelewa...
 
Dogo alikuwa mtoro wa kutukuka siku moja karudi home mshua kamuuliza vipi? Dogo pana mwalimu kafariki mdingi mzee wa kamati pale shuleni ikabidi aende kutoa pole cha ajabu akakuta taratibu za shule kama kawaida lakini akaona ngoja aingie ofisini pa mkuu wa shule basi kasalimia pale na kutoa pole ndipo mwalimu akashangaa mbona hakuna mwalimu alie fariki basi mzee akajizoazoa taratibu mpaka home mzee alimkuta dogo kakaa penye kochi hajamstukia mshua kama katinga basi alimpa kibao dogo alinyanyuliwa na lile kofi kufika katikati ya sebule akageuka kisha kuna kochi lingine upande wa pili limetizamana na lile alilokuwa amekalia akajikuta kaenda kukaa hapo hakutoa sauti yoyote kwa muda wa dakika tano na ndio kwa kumbukumbu zangu ilikuwa mara ya mwisho kupigwa na mzee.
 
Nilikuwa muda wa chakula cha walimu Mimi nipo jikoni. Hata kama kuna kipindi
 
niliitwa silent killer ukiniona mpole kumbe huku nyuma nilikua naongoza jeshi langu kwenda kuiba vyakula madaftari peni sabuni za kuogea mpaka namaliza sikuwah kushtukiwa.... nilishaongoza mpaka shambulizi la kuwapiga form five sie tupo six hapo tulivunja vioo vyote vya bweni lao....... jeshi langu lilikua na wanafunzi watano tu kutwa kucha nikuwatuma uhalifu tu ila mie kiongozi wao ukiniona mpole balaaaa ilikua ni ngumu kunijua
 
Mchezaji mzuri wa football. Bila kuwepo timu haiingii uwanjani kucheza
 
Mnanikumbusha mbali sana..
Illegals zote..
Kuandikwa black book mara 4..
Statements za kutosha..
Top 3 sikosekan ila kwa matukio sikosekani..
Chemba yangu ya kusomea ilkuwa juu ya dari sa sita usiku mpk sa nane..
Shivaz..
Kumtongoza mwalimu nilikutana nae bar mmoj mtaa wa shule wikend akanijb atanifikiria ila aliniwekea wambuzi mpka namalza 4 nikaja kukutana nae mkoa flan nikakumbusha kesho yak nikazam chunvin..
Kukunjana na mkuu wa shule(hii sita sahau)altaka kunioshea kwa she wangu tena parade..
Kuuza mabeg na blangeti magorod mapya first term ya form one na wagen..
Troublemaker class clone..
Club zote za chug miaka ile ya 2009 kwend chin nilipita
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…