Primary nilikuwa najua sana maarifa ya jamii na historia, nikapewa jina la Kinjekitile.
O level form one nimeingia tu ikawa napenda kujibujibu maswali lakini nilikuwa naenda nje ya mada jamaa wakanipa jina la 'nje ya mada'
Form two na form three jamaa wakanipa jina la Tozi.. Maana ilikuwaga nakuja shule na vibegi vya ajabu ajabu vya kushona coz mama alikuwa fundi cherehani... Mara leo kibegi cha salfeti kesho pazia limefanywa begi.. Basi tu yaani mapigo tofauti tofauti
Advence nilikuwa mpole maana nilikuwa kwenye tension ya hali ya juu. Nilikuwa na msongo mkubwa sana wa mawazo 1) family kulikuwa hakuelewiki na maisha magumu kishenzi, so all two years nilikuwa kama msukule lengo moja tu nisome nifaulu niende chuo.. Sikuwa na mbwembwe nyingi
Chuo pia naingia kama vile advance sikutaka mbwembwe nyingi all i wanted was to make wonders and gladly i did mpaka kesho am proud for that.
But yote kwa yote since primary mpaka secondary na mpaka chuo nimekuwa mchelewaji maarufu.. Mpaka kazini nimekuwa nikichelewa...