Ulisifika Kwa Lipi Shuleni....

Ulisifika Kwa Lipi Shuleni....

Duh!!
Kwanza nilikuwa mtundu sana,mpaka nikapewa uongozi Ili niwadhibiti watundu wenzangu.
Pili,nilikuwa na some sort of ukorofi nikapewa jina dakika mbili mbele.
Tatu,kuna mwalimu alikosea kusema neno la kiingereza assembly,alisema menyi instead of many,nilitoa kicheko kimoja hiko ambacho kilinigharimu nililambwa bakora za Maana. Majina yote yakafa nikaanza kuitwa menyiii
 
Nilikua nasifika kwa kula ada na kujitetea, ya sekondari o level na a level.
Sasa O na A level nishajitetea nimegewa vyeti, chuo huwezi kula ada ukategemea utetezi hivyo nikawa silipi kwa wakati, sasa hivi nawatafutia ada yao nikachukue cheti.

Nahisi nilikua na hobi hiyo tu kila nikiona ada, halafu ada kama ina laana ukila hadi uje kuipata si mchezo.
 
Utoro. Niite escaper. Nilikuwa mtaalam sana wa utoro.. njia zote master nilikuwa mm
 
ubishi
nilikua naweza hata kubishana hata na darasa zima hata kama ni uongo mi natetea tu sikua tofauti na ccm

mada maarufu ni bahari za ulaya hazina maji ya chumvi
ubishi wa kijinga hadi leo huwa najichekaga
haaahaaahaa eti sikuwa tofauti na CCM
 
1. Utoro, nimeanza utoro toka darasa la kwanza, nakumbuka hadi mtihani wa kwenda darala la pili nilikuja kushtuliwa na mshikaji huku washafanya hisabati, darasa la pili hivyo hivyo, la tatu nilisoma mwezi mmoja kisha nikatokomea kusikojulikana eti nikaibuka kufanya mtihani wa darasa la nne, mwalimu akanigomea ikabidi wanirudishe tena la tatu.

Ilipofika darasa la 6 nikarudia tabia yangu nikaja kuibuka la 7, shuleni walikua wananijua kwa sufa moja tu, utoro sugu ila siku nikiibuka kwenye mtihani namba moja hadi 3 hainikosi.

2. Utorokaji, jamani nilikua natoroka shule balaa, hadi nilipohamishiwa kwa mwalimu bado nikawa natoroka tu kwenda hom, mwalim hakunichapa aliniweka chini akanishauri nikaacha kutoroka ila nilipoenda secondari nikarudia tabia ya kutoroka na kuchelewa..

Sekondari nikasoma shule ya bweni ya serikali iko katikati ya mji, ikawa kila wiki lazima nitoroke kuanzia ijumaa narudi jumatatu alfajiri maana hapo mjini alikuwepo baba mdogo na akawa hanimind maana matokeo yangu hayakua na shida.

3. Kuna tabia nyingine nilikua nazo ingawa hazikua zinajulikana ni wizi wa madaftari na kalam, kila mhula ukianza tulikua tunapewa/kuja na madaftari mapya huko shule ya msingi, sijawahi kukunua daftari, nilikua na hom library yangu ya madaftari ya wizi mapya najaladia tu jalada zuri huwezi kujua ni yako.

Sekondari pia hivyo hivyo, wale waliokua na miandiko mizuri na mpangilio mzuri wa maandishi ilikua ikikaribia tu mtihani lazima niibe madaftari yao nikajisomee, mitihani ikiisha naweza kulirudisha hapo darasani nikalitelekeza au nikaamua kulificha kabisa.

Sure nimeyamisi sana maisha ya shule.
Daah Mkuu Ulikuwa Balaa Salute kwako
 
Kufanya vizuri katika masomo pamoja na kua BAHIRI,kwenye kumpa hela mtu haswa haswa mademu yaani ilikua ngumu sana.Nilikua nikiombwa hela na demu nakasirika sana mpaka natetemeka na mwili unabadilika rangi.
Doh Noma sanaa
haaahaahaa
 
nilikuwa muimbaji maarufu bwenini.....mfano weekend nilikuwa naanza kuimba alfajiri...walikuwa wananiita kiredio......
nahisi kuna ambao nilikuwa nawakera ila kwa sababu nilikuwa na mdomo walinyamaza tu
Haahaa
Ulikuwa kama mshikaj wangu M1 hivi
 
Kucheza draft O-level, tulikuwa ni day, asubuhi unaamka unaenda shule, mkifika mnaweka madaftari mnaenda kucheza draft mpaka muda wa kutawanyika mnafata madaftari mnarudi home kupiga msosi.

Jioni mnarudi tena, sasa ilikuwa inabidi notisi niandike usiku na inabidi nisome some ku-cover magepu, kila pepa likija niko kwenye namba nzuri, wakati tumefanya Mock Form 4 nikawa na div 1 mwalimu (second master) akakataa kabisa, akasema matokeo yangu yasahihishwe upya la sivyo niseme wapi nimeiba pepa.

Baadaye ikawa anawakataza watu kukaa na mimi kabisa, ukikutwa tu ni adhabu, mpaka duka tulilokuwa tunacheza walienda polisi kupiga biti kwamba akitukaribisha tu anafungwa, ndo ikawa nafasi ya mimi kukaa darasani kwa miezi michache ya mwisho form 4.

Uzuri kila weekend nilikuwa naenda tuition.
 
nilikuwa muimbaji maarufu bwenini.....mfano weekend nilikuwa naanza kuimba alfajiri...walikuwa wananiita kiredio......
nahisi kuna ambao nilikuwa nawakera ila kwa sababu nilikuwa na mdomo walinyamaza tu
Mdomo bado unao?[HASHTAG]#Demba[/HASHTAG]
 
Back
Top Bottom