1. Utoro, nimeanza utoro toka darasa la kwanza, nakumbuka hadi mtihani wa kwenda darala la pili nilikuja kushtuliwa na mshikaji huku washafanya hisabati, darasa la pili hivyo hivyo, la tatu nilisoma mwezi mmoja kisha nikatokomea kusikojulikana eti nikaibuka kufanya mtihani wa darasa la nne, mwalimu akanigomea ikabidi wanirudishe tena la tatu.
Ilipofika darasa la 6 nikarudia tabia yangu nikaja kuibuka la 7, shuleni walikua wananijua kwa sufa moja tu, utoro sugu ila siku nikiibuka kwenye mtihani namba moja hadi 3 hainikosi.
2. Utorokaji, jamani nilikua natoroka shule balaa, hadi nilipohamishiwa kwa mwalimu bado nikawa natoroka tu kwenda hom, mwalim hakunichapa aliniweka chini akanishauri nikaacha kutoroka ila nilipoenda secondari nikarudia tabia ya kutoroka na kuchelewa..
Sekondari nikasoma shule ya bweni ya serikali iko katikati ya mji, ikawa kila wiki lazima nitoroke kuanzia ijumaa narudi jumatatu alfajiri maana hapo mjini alikuwepo baba mdogo na akawa hanimind maana matokeo yangu hayakua na shida.
3. Kuna tabia nyingine nilikua nazo ingawa hazikua zinajulikana ni wizi wa madaftari na kalam, kila mhula ukianza tulikua tunapewa/kuja na madaftari mapya huko shule ya msingi, sijawahi kukunua daftari, nilikua na hom library yangu ya madaftari ya wizi mapya najaladia tu jalada zuri huwezi kujua ni yako.
Sekondari pia hivyo hivyo, wale waliokua na miandiko mizuri na mpangilio mzuri wa maandishi ilikua ikikaribia tu mtihani lazima niibe madaftari yao nikajisomee, mitihani ikiisha naweza kulirudisha hapo darasani nikalitelekeza au nikaamua kulificha kabisa.
Sure nimeyamisi sana maisha ya shule.