Nakumbuka brother aliambiwa arudishe alipoulizwa umenunua Pete aina gani akasema Dhahabu bi mkubwa akaja juu akamwambia rudisha kachukue silver akarudi kuchukua silver ila hadi leo sijui kwanini alirudishwaPete nilinunua zenye ppt ya dhahabu, kuogopa zisije kupauka.
Huyo Mkeo/Bibi harusi mtarajiwa atakubali kuolewa bila sherehe?Hyo siku ya ndoa nikitoka kanisani(siku hyo hyo ya ibada) namchukua mtoto wa mtu namuweka ndani jioni tunapika ugali na mchemsho wa kuku wa kienyeji na wine 12k
Namuungia bundle la mwezi la 15k ili apost picha ambazo tumepiga kanisani...
nguo atavaa gauni lake analopenda mimi ntavaa kaunda yangu safi...
Gharama ntakua nimemaliza hapo.
Huenda ilifanyika hivyo ili kupunguza gharama.Nakumbuka brother aliambiwa arudishe alipoulizwa umenunua Pete aina gani akasema Dhahabu bi mkubwa akaja juu akamwambia rudisha kachukue silver akarudi kuchukua silver ila hadi leo sijui kwanini alirudishwa
Harusi au sherehe yoyote ile ni PESAAAA kama huna pesa kaa kule kona ,tulia kama moja na kama huna pesa nenda Serikalini na mashahidi wako wa 3 funga ndoa na mchezo kwishaaa.Suala la Kuoa ama kuolewa bado litaendelea kuwa ni hitaji muhimu miongoni mwa Jamii ya watu wengi Ulimwenguni.
Kwa Tanzania, tunazo Ndoa za aina mbalimbali ambazo zinatambulika kisheria ambazo ni Ndoa za Kidini, Kimila na Kiserikali.
Mara baada ya kufunga Ndoa, maharusi wengi Kwa kushirikiana na jamii zao, hupenda kufanya sherehe. Sherehe hizo huambatana na michango Kwa walio wengi kupitisha Kadi kwaajili ya kuomba kuchangiwa kufanikisha sherehe za harusi zao.
Japo baadhi hufanya sherehe za harusi zao pasipo kuomba michango Kwa ndugu/jamaa na marafiki. Wao hugharamia Kila kitu wao wenyewe na hao ndugu/jamaa na marafiki hupewa Kadi za mwaliko kuweza kuhudhuria sherehe tu.
Kwa utafiti usio rasmi, sherehe za harusi hupendwa zaidi na Wanawake kuliko Wanaume. Wanaume wako tayari kufunga Ndoa za kimya kimya lakini sio Wanawake.
Je, ulitumia fedha kiasi gani kufanikisha harusi yako ama umepanga kutumia fedha kiasi gani kwaajili ya harusi yako na mwenzi wako?
Binafsi, nilitumia kiasi cha shilingi milioni 10 kuweza kufanikisha harusi yangu na Bibi yenu miaka kadhaa iliyopita 🤗🙏
Sikuhitaji kuchangiwa fedha kufanikisha sherehe ile, bali niliweza kujipanga mwenyewe Kwa muda wa miaka 5.
Nilifungua akaunti maalumu Benki (Fixed deposit account) ambayo nilikuwa nina ruhusiwa kuweka fedha pasipo kutoa Kwa muda wa miaka 5 hivi, japo nilikuwa napata interest kidogo za Benki.
Baada ya miaka 4 hivi, nilikwenda kuchungulia fedha nikakuta nina milioni 9.35 so nikaanza maandalizi kujiandaa na harusi Mwaka unaofatia.
Mind you, tayari nilikuwa nina Cheti cha Ndoa ya Serikali na mwenzangu lakini yeye Kiu yake ni lazima tukafunge ile ya Kanisani 🙌
Kuna wakati nilikuwa nafanya biashara ya kununua na kuuza mazao ya nafaka. Nilikuwa naenda Mashambani, nawakopesha fedha Wakulima then wakati wa mavuno nilikuwa naenda kukusanya mazao hasa zao la Mpunga.
Kwahiyo kwenye ile harusi, sikuwa na hofu ya Chakula maana tayari nilikuwa nina stock ya magunia ya kutosha ya Mpunga.
Wanasema harusi ni kula na Kunywa. Kwahiyo nilijiandaa kwenye eneo hili.
Kwenye upande wa Chakula niliandaa wali mweupe,Pilau, chips, mtori, nyama za kukaanga, kachumbali
Vinywaji niliandaa Soda na Maji tu.
Niliandaa Kadi za Mwaliko za watu 300 lakini walifika watu 358 japo hili nilijua lazima lingetokea maana harusi yenyewe niliifanyia Kijijini kwahiyo wengi ni wale watu mnajuana. Kwahiyo niliweka chakula na Vinywaji Kwa zaidi (excess budgeting)
Pamoja na Wageni waalikwa, usiku ule nilikuwa na Mchungaji pamoja na Mwinjilisti ambao walishiriki kuanzia mwanzo wa harusi hadi tunamaliza tukio majira ya saa 9 usiku.
Gharama za mavazi za Wapambe niligharamia mwenyewe kuanzia mavazi ya Kanisani hadi Ukumbini 🙌
Niliamua kukodisha Ma-MC wawili ili kunogesha sherehe 🤗
Pete nilinunua zenye ppt ya dhahabu, kuogopa zisije kupauka.
Mchanganuo wa Bajeti yangu kufanikisha sherehe ile, nimeambatisha kwaajili ya wengine kujifunza.
Kumbukeni, hata kama umeoa bado unaweza kuja kuozesha watoto wako miaka ijayo. Baadhi yetu mnaweza kuwa Wanakamati kwenye harusi za wengine pia
Kwahiyo Harusi zitaendelea kufanyika hata baada ya kufa kwetu maana tutakuwa tumeacha Kizazi chetu kinaendelea Kuoa na kuolewa.
Umesema sahihi, ukiona huwezi kumudu gharama za harusi mnaweza Kufunga Ndoa yenu kimya kimya na mkamaliza mchezo.Harusi au sherehe yoyote ile ni PESAAAA kama huna pesa kaa kule kona ,tulia kama moja na kama huna pesa nenda Serikalini na mashahidi wako wa 3 funga ndoa na mchezo kwishaaa.
Huo usumbufu ndio siupendi hata kama ni jambo la kijamiiMiezi 6 ya kuwakomalia ndugu na jamaa wakuchangie harusi, wakati huo huo unataka harusi ya shilingi milioni 20 halafu muhusika ana shilingi milioni 1 kama kianzio
Milioni 19 zote zinategemea wadau [emoji119]
Baba, mama, dada, kaka wa both sides, imeisha.....mashangazi sijui ndugu matembele waende wanakwenda. Hii budget mtu hawezi kukosa, la sivyo asioe..!!!Hizo gharama za kuwapeleka maharusi na waalikwa ShishiFood nani atagharamia?
Upo vizuri kwenye BajetiBaba, mama, dada, kaka wa both sides, imeisha.....mashangazi sijui ndugu matembele waende wanakwenda. Hii budget mtu hawezi kukosa, la sivyo asioe..!!!
Mimi pia sipendi aisee huo usumbufu, ni vile tunaishi kwenye jamii ya watu wengi ambao wanadhani michango ya harusi ni haki yako kuchangia ukishapewa Kadi zao za michango ya harusi 🙌Huo usumbufu ndio siupendi hata kama ni jambo la kijamii
Umejuaje babu, hapa ni kutonga na bajeti du, ombehiyokoUpo vizuri kwenye Bajeti
Vipi una Upare ndani yako ama ulienda short course Uingereza 😜
Kwa maana hiyo race wako vizuri sana kwenye kupanga bajeti 🙌
Idea nzuri...na maisha yanaendeleaHyo siku ya ndoa nikitoka kanisani(siku hyo hyo ya ibada) namchukua mtoto wa mtu namuweka ndani jioni tunapika ugali na mchemsho wa kuku wa kienyeji na wine 12k
Namuungia bundle la mwezi la 15k ili apost picha ambazo tumepiga kanisani...
nguo atavaa gauni lake analopenda mimi ntavaa kaunda yangu safi...
Gharama ntakua nimemaliza hapo.
Kwahiyo umeamua kusisitiza ulichoongea Kwa Kipare?Umejuaje babu, hapa ni kutonga na bajeti du, ombehiyoko
Mi nilishasema nataka ndoa ya watu nane tu,ndugu wanne upande wangu na wanne upande wa mumeWewe ukiwa Bibi harusi utaridhia hilo Mjukuu?
Maana ninyi ndiyo huwa mnaongoza Kwa kupenda reception nzuri Siku ya harusi zenu 🙌
Mimi ndio namuoaHuyo Mkeo/Bibi harusi mtarajiwa atakubali kuolewa bila sherehe?
Maana hapo ndipo Mtihani ulipo
Sijawahi fanya sherehe yoyote tangu nizaliwe..Idea nzuri...na maisha yanaendelea
Unaolewa lini sasa ?Sitofanya sherehe ya harusi...
Gauni langu nataka liwe zuri sanaaa... nipige picha za ukumbusho nikitoka kanisani
Baada ya kanisani kila mtu akale kwao!