Uliuza nini kwa bei ya hasara ili utatue shida iliyo mbele yako?

LA7

JF-Expert Member
Joined
Aug 26, 2019
Posts
655
Reaction score
2,369
Katika harakati za utafutaji nakumbuka niliamua kutoka Singida kwenda Mbeya na baiskeli, nilikuwa sina hata mia mfukoni.

Nilipofika Itigi baskeli ikapata pancha, jumlisha njaa nikauza simu yangu niliyo inunua 70,000 kwa 10,000, power bank niliyoinunua kwa 20,000 nikauza 7,000, nikapata pesa ya kula na kununua tube nyingine ya tairi, maana hiyo ilikuwa ni siku ya pili ya safari yangu.

Nikapotea ramani nikajikuta nakutana na kibao kimeandikwa karibu Tabora, hapo ndio nilipochanganyikiwa, ikabidi niiuze baiskeli niliyoinunua kwa 80,000 nikaiuza kwa 23,000 ndio nikapata nauli ya kwenda mpaka Kigoma kwa treni ya kupandia Tabora mjini.

Maisha yana mambo mengi, nikikumbuka nasema asante Mungu.
 
Nilipokuwa mdogo nilitembelea kwa dada daslam nikapewa vile viredio ambavyo kulia mpaka uchomeke earphones aisee sio siri kesho yake nimeenda kutembea mtaani mtu akaniaomba nikampa maana nilijua kibovu... nikikumbuka mpaka leo naumia sana bora hata nyie mliuza kwa hasara😭😭😭😭😭
 
Katika harakati za utafutaji nakumbuka niliamua kutoka Singida kwenda Mbeya na baiskeli, nilikuwa sina hata mia mfukoni.

Nilipofika Itigi baskeli ikapata pancha, jumlisha njaa nikauza simu yangu niliyo inunua 70,000 kwa 10,000, power bank niliyoinunua kwa 20,000 nikauza 7,000, nikapata pesa ya kula na kununua tube nyingine ya tairi, maana hiyo ilikuwa ni siku ya pili ya safari yangu.

Nikapotea ramani nikajikuta nakutana na kibao kimeandikwa karibu Tabora, hapo ndio nilipochanganyikiwa, ikabidi niiuze baiskeli niliyoinunua kwa 80,000 nikaiuza kwa 23,000 ndio nikapata nauli ya kwenda mpaka Kigoma kwa treni ya kupandia Tabora mjini.

Maisha yana mambo mengi, nikikumbuka nasema asante Mungu.
Nimecheka sana mkuu, dah hatari sana
 
Niliuza siti ya treni Dar to Tabora ili nipate pesa ya starehe (nilisimama hadi nikaanguka/kuzimia kwa uchovu), na peaa zote zikaibiwa.
We jamaa hauko serious, dah nakumbuka niliwahi simama from Tabora to Dar enzi hizo, mhuu aisee treni ilikuwa inajaza hatari sana na ni safari ya zaidi siku moja na kuna ishu ya sekenke
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Katika harakati za utafutaji nakumbuka niliamua kutoka Singida kwenda Mbeya na baiskeli, nilikuwa sina hata mia mfukoni.

Nilipofika Itigi baskeli ikapata pancha, jumlisha njaa nikauza simu yangu niliyo inunua 70,000 kwa 10,000, power bank niliyoinunua kwa 20,000 nikauza 7,000, nikapata pesa ya kula na kununua tube nyingine ya tairi, maana hiyo ilikuwa ni siku ya pili ya safari yangu.

Nikapotea ramani nikajikuta nakutana na kibao kimeandikwa karibu Tabora, hapo ndio nilipochanganyikiwa, ikabidi niiuze baiskeli niliyoinunua kwa 80,000 nikaiuza kwa 23,000 ndio nikapata nauli ya kwenda mpaka Kigoma kwa treni ya kupandia Tabora mjini.

Maisha yana mambo mengi, nikikumbuka nasema asante Mungu.
Ahahahahah lazima ujutie sio leo tu mpaka kesho
 
Niliuza gesi mtungi mkubwa, fryer yake, kabati la vioo, rice cooker, jagi la umeme, kitanda, sabufa na sofa kwa laki 500,000 ili nipate ada nashukuru now nimtumish japo nikikumbuka naumia sana
Yaani ulimwachia chumba kabisa🤓🤓😂
 
We jamaa hauko serious, dah nakumbuka niliwahi simama from Tabora to Dar enzi hizo, mhuu aisee treni ilikuwa inajaza hatari sana na ni safari ya zaidi siku moja na kuna ishu ya sekenke
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Kusema hakuna nafasi ya kukaa ata chini..?
 
Mwaka 2012 niliwekaga bond TV yangu Sony niliyonunua 450k kwa money shark mmoja wa town... siku ya kulipa imefika sina hela, jamaa hakuniongezea hata dakika moja akapita na TV kwa deni la 200k tu. Hadi leo inauma.. halafu nikakutana na ndugu yangu baada ya kumsimulia mkasa mzima akasema bora ningemuuzia hiyo TV kwa 200k kwasababu hata yeye alikuwa anaitamani.
 
Back
Top Bottom