Uliuza nini kwa bei ya hasara ili utatue shida iliyo mbele yako?

Uliuza nini kwa bei ya hasara ili utatue shida iliyo mbele yako?

Niliuza dressing table yangu nilionunua kwa laki mbili nikauza kwa elfu 40 ili niende Europe
 
Mambo ya kuanza safari kwa hisia mwisho wake ndio huo sasa ha ha ha ha ha [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Wewe unaondokaje mikono mitupu na unajua kuna kulala njiani, kula njiani, na kuna dharula kwann hata usiwe na poketi money na uwe na mchoro hata wa safari yako itakuwa na vituo vingapi hadi ufike mahala unakwenda.
 
Mwaka 2012 niliwekaga bond TV yangu Sony niliyonunua 450k kwa money shark mmoja wa town... siku ya kulipa imefika sina hela, jamaa hakuniongezea hata dakika moja akapita na TV kwa deni la 200k tu. Hadi leo inauma.. halafu nikakutana na ndugu yangu baada ya kumsimulia mkasa mzima akasema bora ningemuuzia hiyo TV kwa 200k kwasababu hata yeye alikuwa anaitamani.
Watu wa hivyo bora wawe wanakaa kimya. Sasa mtu akikwambia hiyo kauli inasaidia nini muda huo upo kwenye majanga
 
Tatizo la ndugu wengi wapumbavu ukitaka muuzia kitu utatue shida yako ataanza tangaza au ataamua kukukopa

Ishanitokea

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
 
Mkuu kuakaa!! Watu wamelala chini ya kiti yaani uvunguni, sehemu ya kuegemea ya kiti mtu kakaa pia, wengine wamekaa chooni. Unaweza kudhani ni story ya kusadikika lakini hali ilikuwa mbaya sana.
Huu ujinga ni TRC wanataka. Kwann shirika wasiwekeze idadi ya mabehewa iwe ya kutosha watu wapate siti na kusafiri kwa usalama.

Aisee nachukia sana kutesa raia kwa kisingizio cha wao kukubaliana na hali yao.

Kwanini raia wanateseka hivyo na serikali ipo mimi siwezi kukubaliana na huu upumbavu wa kutesa raia.
 
Mambo ya kuanza safari kwa hisia mwisho wake ndio huo sasa ha ha ha ha ha [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Wewe unaondokaje mikono mitupu na unajua kuna kulala njiani, kula njiani, na kuna dharula kwann hata usiwe na poketi money na uwe na mchoro hata wa safari yako itakuwa na vituo vingapi hadi ufike mahala unakwenda.
ikishakuwa hivo basi unakuwa utalii huo
 
Watu wa hivyo bora wawe wanakaa kimya. Sasa mtu akikwambia hiyo kauli inasaidia nini muda huo upo kwenye majanga
Ni mapito tu kwenye maisha bro. Wakati wa majanga ndo utawajua walio upande wako na wasio upande wako.
 
Niliuza fridge langu hisense portable hivi, nilinunua 780,000 ilikua on promotion, bei original ilikuaga 1,150,000 pale Game, nikapata changamoto , sitasahau fridge langu nililiuza 350,000 tena lina miezi 8 tu[emoji25][emoji24], hua nikikumbuka nabaki kuhudhunika sana.

Dah shida ikikupata sio poa, unaweza pata uchizi.
 
Niliuza mountain bike gharama yake 150,000 kwa 50000 Ili nipate hela ya kwenda kununua dawa ya kupiga shambani maana wadudu walikua wanamaliza mazao yangu.
 
Niliuza fridge aisee kwa bei ya hasara sana ili kutatua changamoto iliyokua inanikabili
 
Back
Top Bottom