Uliuza nini kwa bei ya hasara ili utatue shida iliyo mbele yako?

Uliuza nini kwa bei ya hasara ili utatue shida iliyo mbele yako?

Niliuza Radio yangu aina ya LG ambayo nilinunua 500,000 (laki tano) kwa sh 80000 ( elfu themanini) ili nipate pesa ya kujikimu kwa siku ile aisee niliumia karibia miez miwili nawaza jambo nililolifanya...

Sent from my TECNO KB7j using JamiiForums mobile app
Daah mkuu pole sana yaani hapo parefu mnoo bora hata ungeweka bondi duuh
 
Mwaka 2012 niliwekaga bond TV yangu Sony niliyonunua 450k kwa money shark mmoja wa town... siku ya kulipa imefika sina hela, jamaa hakuniongezea hata dakika moja akapita na TV. Hadi leo inauma
Jamaa alijipanga khaa 🤓
 
Niliuza gesi mtungi mkubwa, fryer yake, kabati la vioo, rice cooker, jagi la umeme, kitanda, sabufa na sofa kwa laki 500,000 ili nipate ada nashukuru now nimtumish japo nikikumbuka naumia sana
Unatumikia serikali,kanisa au msikiti?
 
Kuna majamaa town wamejipanga kwa mikopo ya dizaini hiyo.. full dhuluma. Kule Arusha kuna jambazi mwandamizi anaitwa Alex Masawe ndo ilikuwa ishu zake.
Sasa hapo inabidi na wewe uwe mtata mtata an...
Au kama mnajua tabia yake mnamtegea mchezo akiingia 18 mnaye😂😂
 
Katika harakati za utafutaji nakumbuka niliamua kutoka Singida kwenda Mbeya na baiskeli, nilikuwa sina hata mia mfukoni.

Nilipofika Itigi baskeli ikapata pancha, jumlisha njaa nikauza simu yangu niliyo inunua 70,000 kwa 10,000, power bank niliyoinunua kwa 20,000 nikauza 7,000, nikapata pesa ya kula na kununua tube nyingine ya tairi, maana hiyo ilikuwa ni siku ya pili ya safari yangu.

Nikapotea ramani nikajikuta nakutana na kibao kimeandikwa karibu Tabora, hapo ndio nilipochanganyikiwa, ikabidi niiuze baiskeli niliyoinunua kwa 80,000 nikaiuza kwa 23,000 ndio nikapata nauli ya kwenda mpaka Kigoma kwa treni ya kupandia Tabora mjini.

Maisha yana mambo mengi, nikikumbuka nasema asante Mungu.
Duuuh kama kweli umepitia mengi yasiyoeleweka
 
Kusema hakuna nafasi ya kukaa ata chini..?
Mkuu kuakaa!! Watu wamelala chini ya kiti yaani uvunguni, sehemu ya kuegemea ya kiti mtu kakaa pia, wengine wamekaa chooni. Unaweza kudhani ni story ya kusadikika lakini hali ilikuwa mbaya sana.
 
Kikubwa si ulienda afrika kusini mkuu.. huoni kwenda kule ni bahati pia..
Nazani ulikuja kupata zaidi ya vile
South hakuna ishu mazee, watz wengi ni mateja na wapiga michomoko, wengi hawana maisha hata kulala kwao ni kwa mateso
 
Samsung ya 200,000/= na bado na deni la 30,000/= nikaweka bond kwa 40,000/= ikaisha hiyoo.

Sumsung min-laptop Tsh 350,000/= kwa Tsh. 30,0000/= bond ikawa kalagabao.

Ama kweli njaa mwana malegeza.
 
Friji la laki nane nikauza kwa laki tatu tisini, roho iliumaje?
 
Julius’s timz zangu nlikua nmezivaa mara tatu tu nlinunua 120k nkauza 50k na laptop nkauza 100000
 
Niliuza gesi mtungi mkubwa, fryer yake, kabati la vioo, rice cooker, jagi la umeme, kitanda, sabufa na sofa kwa laki 500,000 ili nipate ada nashukuru now nimtumish japo nikikumbuka naumia sana
Kwahiyo na jitihada zote hizo bado ww ni mtumwa dah maisha hayako fair kabisa
 
Back
Top Bottom