Uliuza nini kwa bei ya hasara ili utatue shida iliyo mbele yako?

Daah mkuu pole sana yaani hapo parefu mnoo bora hata ungeweka bondi duuh
 
Mwaka 2012 niliwekaga bond TV yangu Sony niliyonunua 450k kwa money shark mmoja wa town... siku ya kulipa imefika sina hela, jamaa hakuniongezea hata dakika moja akapita na TV. Hadi leo inauma
Jamaa alijipanga khaa 🤓
 
Niliuza gesi mtungi mkubwa, fryer yake, kabati la vioo, rice cooker, jagi la umeme, kitanda, sabufa na sofa kwa laki 500,000 ili nipate ada nashukuru now nimtumish japo nikikumbuka naumia sana
Unatumikia serikali,kanisa au msikiti?
 
Kuna majamaa town wamejipanga kwa mikopo ya dizaini hiyo.. full dhuluma. Kule Arusha kuna jambazi mwandamizi anaitwa Alex Masawe ndo ilikuwa ishu zake.
Sasa hapo inabidi na wewe uwe mtata mtata an...
Au kama mnajua tabia yake mnamtegea mchezo akiingia 18 mnaye😂😂
 
Duuuh kama kweli umepitia mengi yasiyoeleweka
 
Kusema hakuna nafasi ya kukaa ata chini..?
Mkuu kuakaa!! Watu wamelala chini ya kiti yaani uvunguni, sehemu ya kuegemea ya kiti mtu kakaa pia, wengine wamekaa chooni. Unaweza kudhani ni story ya kusadikika lakini hali ilikuwa mbaya sana.
 
Niliweka bond kitabu changu cha research nilichonunua 80k kwa kitimoto kilo 2 na valuer kubwa moja hahahah dahhh
 
Kikubwa si ulienda afrika kusini mkuu.. huoni kwenda kule ni bahati pia..
Nazani ulikuja kupata zaidi ya vile
South hakuna ishu mazee, watz wengi ni mateja na wapiga michomoko, wengi hawana maisha hata kulala kwao ni kwa mateso
 
Samsung ya 200,000/= na bado na deni la 30,000/= nikaweka bond kwa 40,000/= ikaisha hiyoo.

Sumsung min-laptop Tsh 350,000/= kwa Tsh. 30,0000/= bond ikawa kalagabao.

Ama kweli njaa mwana malegeza.
 
Friji la laki nane nikauza kwa laki tatu tisini, roho iliumaje?
 
Julius’s timz zangu nlikua nmezivaa mara tatu tu nlinunua 120k nkauza 50k na laptop nkauza 100000
 
Niliuza gesi mtungi mkubwa, fryer yake, kabati la vioo, rice cooker, jagi la umeme, kitanda, sabufa na sofa kwa laki 500,000 ili nipate ada nashukuru now nimtumish japo nikikumbuka naumia sana
Kwahiyo na jitihada zote hizo bado ww ni mtumwa dah maisha hayako fair kabisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…