Uliwahi kuishi chumba, hostel au nyumba moja na room mate ambae si muungwana, weka kisa chako hapa

Hostel ya mtu binafsi room tulikua tunakaa mtu mbili.Homeboy wangu aisee alikuwa na makiu na mali imevuka mikoa kumfuata .Nikaone sio case nimwache amalize makiu.Ila niliishi kama mwehu[emoji3][emoji3][emoji3]
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] mie siwezi ningewaambia waende guest khaaaaaah!!!!
 
Je sisi tulio ishi kwa watu alaf hao wenyeji wetu wakawa washenzi tunaandika wapi?
 
We ni chizi muombe bro msamaha ndugu wa damu unamtimua kisa demu mtu ambae unaweza kumuelekeza akikosea bila aibu yoyote yani uzinguane na damu yako kisa ugali na mayai alichokifanya ni kukupunguzia mzigo alikua anajiongeza ungemwambia tu we ulikua na chuki na bro tu shubaamiti
 
Hahaha kitu nimejaliwa ni kuona mbali mkuu, uliza huyo bro yupo wapi now, yaani kuna wale ndugu ambao ni pasua kichwa utamfungulia biashara hii ataharibu, utamweka pale ataharibu, ndo huyo kakaangu sasa na kusema ukweli mm siwezi kumvumilia mtu wa aina hiyo maana mm mwenyewe Nina maisha yangu ya kuyaangalia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…