Uliwahi kuishi chumba, hostel au nyumba moja na room mate ambae si muungwana, weka kisa chako hapa

Uliwahi kuishi chumba, hostel au nyumba moja na room mate ambae si muungwana, weka kisa chako hapa

Hostel ya mtu binafsi room tulikua tunakaa mtu mbili.Homeboy wangu aisee alikuwa na makiu na mali imevuka mikoa kumfuata .Nikaone sio case nimwache amalize makiu.Ila niliishi kama mwehu[emoji3][emoji3][emoji3]
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] mie siwezi ningewaambia waende guest khaaaaaah!!!!
 
Je sisi tulio ishi kwa watu alaf hao wenyeji wetu wakawa washenzi tunaandika wapi?
 
Mimi nilimtimua kakaangu kabisa, alifeli katika mitikasi yake akanambia dogo nataka nije hapo nicheki upepo haujakaa sawa mie poa, hapo ndani nina unga Michele na dagaa kauzu kama kilo hivi.

Basi akaja tukavipiga vyote vikaisha mwanangu, braza hajawahi changia chochote hata tukitaka kubadili mboga utasikia dogo vp leo unatoa kitu cha dagaa tena chukua hata mchicha mwanangu natoa hela yangu tunapika, akapata ishu sasa akawa anawahi kurudi kama saa11 keshafika mimi ndo mpaka saa2.

Nilishangaa nilipokuta kanunua mayai yake mawili kakaanga na unga wake robo kasonga ugali keshakula kitambo miguu kwenye sofa anacheki TV, nikaingia jikoni na mm, sikumuuliza wala nn, hiyo hali ikaendelea kwa wiki mfululizo, nikaona huyu mpumbavu kumbe hajanijua.

Hiyo siku nimerudi nakuta keshakula kama kawaida nikamwambia bro wewe huwezi kuishi na mtu, kwann dogo, wewe tunakaa wote lakini kila kitu unajifanyia cha pekeako basi kama vp we nenda kaendelee na maisha yako mi hapa naona tutazinguana, akamaindi sana.

Mind you siku chache zilizopita nilimwambia toka kidogo shemeji yako anakuja hatutachelewa basi akanijumlishia bwana akapiga simu kwa ndugu wote ooh lumbitisa ananifukuza kwake kwaajili ya demu wake nikasema hapa sirudi nyuma, nikakaza akaondoka, mpaka leo mahusiano yetu hayapo vizuri.
We ni chizi muombe bro msamaha ndugu wa damu unamtimua kisa demu mtu ambae unaweza kumuelekeza akikosea bila aibu yoyote yani uzinguane na damu yako kisa ugali na mayai alichokifanya ni kukupunguzia mzigo alikua anajiongeza ungemwambia tu we ulikua na chuki na bro tu shubaamiti
 
We ni chizi muombe bro msamaha ndugu wa damu unamtimua kisa demu mtu ambae unaweza kumuelekeza akikosea bila aibu yoyote yani uzinguane na damu yako kisa ugali na mayai alichokifanya ni kukupunguzia mzigo alikua anajiongeza ungemwambia tu we ulikua na chuki na bro tu shubaamiti
Hahaha kitu nimejaliwa ni kuona mbali mkuu, uliza huyo bro yupo wapi now, yaani kuna wale ndugu ambao ni pasua kichwa utamfungulia biashara hii ataharibu, utamweka pale ataharibu, ndo huyo kakaangu sasa na kusema ukweli mm siwezi kumvumilia mtu wa aina hiyo maana mm mwenyewe Nina maisha yangu ya kuyaangalia
 
Back
Top Bottom