Uliwahi kulilia mapenzi?

Uliwahi kulilia mapenzi?

Ni siku moja tu nililia siku mama aliponitoka,so nakuona ka kicheche wangu wa zamani ,siku aliporuka hewani.Ngwair mbona huonekani? Vipi hauna TV? Ungekuwa na faida nami ungeniona kwa 3D-Mzee Mangweha.
 
Nililia nilivyomuacha mwanaume aliyenipenda sana’a baada ya kugundua alinidanganya kuhusu uhalisia wake.!!!
Nilikudanganya kwa sababu nilikupenda Sana na sikutaka kukupoteza mana Ungejua uhalisia wangu ungenikataa Ila mpaka sasa bado nakupenda sana na nafasi yako kwenye moyo wangu bado ipo.
 
kitu gani kilikutoa machozi, kukubaliwa, kukataliwa, kupewa au kuporwa mpenzi wako?

kipi kilikuliza? 🐒
Jana tu nimelia. Nilikuwa nahisi kuanza kumchoka mwanamke wangu. Nilikuwa namtafutia visababu nimuache ila hakujaa. Akaja kujaa majuzi. Alifanya kosa la kupekua simu yangu kwa siri, akapiga picha vitu alivyokuwa na mashaka navyo akakaa kimya.

Zimepita siku kama tatu akaniita kwa unyenyekevu tu na kuanza kuniuliza,nilimtukana sana kwa kunipekua, na nilidhamiria itakuwa ndio sababu ya kumpiga chini kwakuwa nilihisi simpendi kama mwanzo. Aliniomba msamaha ila nilikaidi kabisa na kumpa maneno makali, ikumbukwe siishi nae.

Nimekuja kulia baada ya yeye kuniandikia sms ndefu sana akisema leo (ambayo ndio jana) kuwa ndio amepanda gari anaondoka kabisa kwakuwa nimegoma kumsamehe, ila akanikumbusha kuwa ananipenda sana. Kaamua kuondoka na kurudi kwao na kazi kaacha alipokuwa anafanyia. Nilihisi uongo japo roho ilianza kuniuma. Nikaenda kazini kwake kuhakikisha, sikumkuta na hakuna mwenye taarifa. Ikabd niende anapokaa, nikakuta kweli kaondoka na chumba kaachia.

Nililia sana, nikagundua nampenda ila kibri tu cha kumuona si chochote. Baada ya kumpoteza ndio naona thamani yake. Nilimpigia simu tukaongea, kasema ameamua kurudi kwao tu awe mbali na mm. Tumeshafanya mambo mengi na yeye, zawadi alizonipa, upole, ukarimu na utiifu wake kwangu ndio mambo yanayoniumiza. Rafiki zake walikuwa wakinieleza juu ya jinsi alivyokuwa ananipenda na kunielezea kwao.

Ikabidi nimuombe msamaha kwa kila kitu, nilimwaga machozi. Bahati nzuri amenisamehe na ameniahidi atarudi kwa ajili yangu.

Nimepanga kuishi nae, nimegundua ni mwanamke wa kipekee sana.
 
Back
Top Bottom