Uliwahi kulilia mapenzi?

Uliwahi kulilia mapenzi?

Bora ninyi mnaliaga mkiwa mmebreakup, Mi mwenzenu naliaga nikiwa niko kwenye mahusiano, naliaga nikiwa bado najali, naliaga nikiwa najaribu kila liwezekanalo kuyafanya mahusiano yasife. Ila once nikitangaziwa kuachwa/ nikitangaza kuacha alooooh! Nakuwaga na roho ya jiwe. Silii ndio kwanza naenda kujipongeza kuwa atleast i tried πŸ˜€πŸ˜€

Break up huwa ni hatua ya mwisho kabisa baada yakuwa nimepambana sana, mimi ni king’ang’a jamani. 🀣 ila nikishakubali yameisha, Weeeee!

Ujana bwana! Bora nilishapita.
 
Jana tu nimelia. Nilikuwa nahisi kuanza kumchoka mwanamke wangu. Nilikuwa namtafutia visababu nimuache ila hakujaa. Akaja kujaa majuzi. Alifanya kosa la kupekua simu yangu kwa siri, akapiga picha vitu alivyokuwa na mashaka navyo akakaa kimya.

Zimepita siku kama tatu akaniita kwa unyenyekevu tu na kuanza kuniuliza,nilimtukana sana kwa kunipekua, na nilidhamiria itakuwa ndio sababu ya kumpiga chini kwakuwa nilihisi simpendi kama mwanzo. Aliniomba msamaha ila nilikaidi kabisa na kumpa maneno makali, ikumbukwe siishi nae.

Nimekuja kulia baada ya yeye kuniandikia sms ndefu sana akisema leo (ambayo ndio jana) kuwa ndio amepanda gari anaondoka kabisa kwakuwa nimegoma kumsamehe, ila akanikumbusha kuwa ananipenda sana. Kaamua kuondoka na kurudi kwao na kazi kaacha alipokuwa anafanyia. Nilihisi uongo japo roho ilianza kuniuma. Nikaenda kazini kwake kuhakikisha, sikumkuta na hakuna mwenye taarifa. Ikabd niende anapokaa, nikakuta kweli kaondoka na chumba kaachia.

Nililia sana, nikagundua nampenda ila kibri tu cha kumuona si chochote. Baada ya kumpoteza ndio naona thamani yake. Nilimpigia simu tukaongea, kasema ameamua kurudi kwao tu awe mbali na mm. Tumeshafanya mambo mengi na yeye, zawadi alizonipa, upole, ukarimu na utiifu wake kwangu ndio mambo yanayoniumiza. Rafiki zake walikuwa wakinieleza juu ya jinsi alivyokuwa ananipenda na kunielezea kwao.

Ikabidi nimuombe msamaha kwa kila kitu, nilimwaga machozi. Bahati nzuri amenisamehe na ameniahidi atarudi kwa ajili yangu.

Nimepanga kuishi nae, nimegundua ni mwanamke wa kipekee sana.
well done Mwanaume kamili πŸ‘Š
 
Bora ninyi mnaliaga mkiwa mmebreakup, Mi mwenzenu naliaga nikiwa niko kwenye mahusiano, naliaga nikiwa bado najali, naliaga nikiwa najaribu kila liwezekanalo kuyafanya mahusiano yasife. Ila once nikitangaziwa kuachwa/ nikitangaza kuacha alooooh! Nakuwaga na roho ya jiwe. Silii ndio kwanza naenda kujipongeza kuwa atleast i tried πŸ˜€πŸ˜€

Break up huwa ni hatua ya mwisho kabisa baada yakuwa nimepambana sana, mimi ni king’ang’a jamani. 🀣 ila nikishakubali yameisha, Weeeee!

Ujana bwana! Bora nilishapita.
Pole sana una mahaba mazito..!! Ukipata nafasi ya kupenda PENDA na ukikinai ondoka usigeuke nyuma.!
 
Mi nachangamsha kijiwe hapa wala simaanishi, ila yule jamaa nilimkosea nafsi imenisuta sana ndiomana nilimuacha nikalia kwa huzuni..!! Ila namrudia nimegundua alikuja duniani kwaajiri yangu😜
Vizuri, mrudie innocent man.
 
Sasa hv kdg najiweza mamaa, kwa lishangazi nilikuwa nae mana nlkuwa na maisha magumu huku nawe pia ulikuwa unataka chcht kitu kutoka kwa Mm mpenzi wako. Ila sasa nataka kuwa nawe tuu
Kwahiyo ss hivi umepata pesa?? πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Back
Top Bottom