Uliwahi kutamkiwa neno gani baya na Mwalimu wako?

Uliwahi kutamkiwa neno gani baya na Mwalimu wako?

realMamy

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2024
Posts
3,925
Reaction score
8,853
Baadhi ya walimu kuanzia Shule ya Awali na Msingi,Sekondari na hadi Chuo wamekuwa na tabia ya kutamkia watoto maneno makali na yenye kukatisha tamaa.

Mojawapo ya Maneno hayo ni kama “Hutaweza kufanikiwa hata siku moja”.

Wakati mwingine maneno hayo huwafanya wanafunzi kujiona wanyonge na kukata tamaa katika masomo yao na kusababisha baadhi yao kushindwa kutimiza ndoto zao.

Lakini katika hali isiyokuwa ya kawaida wanafunzi wengi wakimaliza masomo baadhi yao hufanikiwa na kuajiriwa katika Taasisi, idara, Mashirika na sehemu nyingine kama hizo.

Walimu hufika kuhitaji msaada na kuwakuta wanafunzi wao waliowatamkia maneno makali wakitoa huduma katika sehemu hizo.

Wakati mwingine husaidiwa lakini pia wakati mwingine hukutana na Vikwazo kutokana na yale waliyoyatenda nyuma.

Walimu tujifunze tuache kuwa wakatili na kutoa kauli kali kwa Mtoto ili kesho yenu iwe Bora zaidi.
 
Back
Top Bottom