Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Baba yako anauza ng'ombe ili alete ng'ombe nyingine shulee🏃♂️🏃♂️💭💭💭Baadhi ya walimu kuanzia Shule ya Awali na Msingi,Sekondari na hadi Chuo wamekuwa na tabia ya kutamkia watoto maneno makali na yenye kukatisha tamaa.
Mojawapo ya Maneno hayo ni kama “Hutaweza kufanikiwa hata siku moja”.
Wakati mwingine maneno hayo huwafanya wanafunzi kujiona wanyonge na kukata tamaa katika masomo yao na kusababisha baadhi yao kushindwa kutimiza ndoto zao.
Lakini katika hali isiyokuwa ya kawaida wanafunzi wengi wakimaliza masomo baadhi yao hufanikiwa na kuajiriwa katika Taasisi, idara, Mashirika na sehemu nyingine kama hizo.
Walimu hufika kuhitaji msaada na kuwakuta wanafunzi wao waliowatamkia maneno makali wakitoa huduma katika sehemu hizo.
Wakati mwingine husaidiwa lakini pia wakati mwingine hukutana na Vikwazo kutokana na yale waliyoyatenda nyuma.
Walimu tujifunze tuache kuwa wakatili na kutoa kauli kali kwa Mtoto ili kesho yenu iwe Bora zaidi.
Neno hilo ubaya wake uko wapi? Huoni uko hai ukikumbuka maneno ya mwalimu?Niliambiwa nisipo angalia nitakufa na ukimwi😁